Dr. Maua Daftari ahukumiwa na mahakama ya Rufani

Waziri Wasira nae aliingiza sijui vigae bila kulipa ushuru, mchaga mmoja akamwingiza town, sijui kesi yake imefikia wapi!
Nafikiri hawa akinamama wawili nao waliingia deal la kutokulipa kodi likawatokea puani ndo wakaanza kugeukana!
 
  • Waziri Daftari Maua alitaka kununua vifaa hivyo huko nchi za nje bila kulipa kodi!
  • Waziri Maua Daftari alitaka kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchi za nje hadi Dar bila kulipia ushuru wa forodha.
  • Waziri Maua Daftari Maua alitaka kuingiza vifaa hivyo bila kulipa ushuru wa forodha Tanzania.
Utapeli wa kutolipa kodi kwa marafiki wasio na diplomatic immunity = conflicts of interests!

I concur with you 100 percent. These are part of chronic problems with our leaders. A minister using immunity vested on him/her to enter into street business like this is very shameful. She is suppossed to take full responsibility and resign immediately when this case was brought to court.
 
Leadership is a talented thing, you can't just brought someone you know as your primary school mate into leadership! Now haya sasa ndio matatizo yake unawezaje kumpa uwaziri a person with no manner! yako wapi yale maadili ya uongozi yaliyosimamiwa na hayati Mwalimu JK! 15 years back when Mwalimu was campaigning for Ben he said, Am qouting him".... I can't just sit on the fence and leave my country to the dogs..." end of couting. I can see mwalimu fought to his last drop of blood so that he can leave behind committed leaders, but today we all witnessing that effort go to drain! JK na uongozi wake wote are just bunch of shameful people!
 
Soory I meant to say JK na uongozi wake are just a bunch of SHAMELESS people with no manners at all!
 
Nani anajua historia ya huyo mlalamikaji Fatma Salimini? Hebu jaribuni kuchunguza yake na utaona huyu mama ni wa aina gani tangu enzi ya gazeti ya Fahari. Dr. Maua ameingizwa mkenge na mtoto wa mjini na yeye akatumbukia kwenye shimo.

Siyo kwamba namtetea Dr. Daftari lakini hukumu iliyokwenda kwa amount kubwa yote hiyo bila ya kuwa na ushahidi wa maandishi (kwa kuaminiwa) mimi naona haikukaa sawa hata kidogo. Hiyo value imepatikana vipi na hasa kwa dhahabu na vyombo vyengine?

Wataalamu wa sheria naomba mutuelimishe kuhusu hili.

Mama Salmini wa Mlandizi? tumejaribu kuelezea sana sakata hili kwenye thread fulani ndani ya JF... ila mwisho naweza sema upole na ushamba wa Dr Maua umemponza kwani hakujua kuwa rafiki yake ana tabia nyingi zaidi ya ile waliyokuwa wameizoea........, Dr alifikiri Mlandizi ni mikorosho tu kumbe sio na sasa kalizwa kimjinijini na aliyedhani kuwa ni swahiba yake, ogopa sana yule mama ni mafia anayejua anafanya nini kwa kila step anayopiga
 
Hili kwa bongo linawezekana pekee.
Hivi amesha tangaza NIA?
Anaweza teuliwa tu nasikia hapo magogoni jamaa wanapo takaa kupitisha jina wanafumba macho kidole kitakapo dondokea ndo huyo huyo bahati yake inakuwa imemdondokea, lakini najua atakata rufaa kujisafisha.
 
Jamani

Mahakama ya Rufani Tanzania imetoa ukumu ya Naibu waziri Maua Daftrai kumlipa mdeni wake 100.7M aliyemtapeli.

Je kwa hili anastahili kubaki waziri. Kosa ni wizi wa kujiaminisha.

Huyu mama anaidhalilisha taaluma...
 
Mama Salmini wa Mlandizi? tumejaribu kuelezea sana sakata hili kwenye thread fulani ndani ya JF... ila mwisho naweza sema upole na ushamba wa Dr Maua umemponza kwani hakujua kuwa rafiki yake ana tabia nyingi zaidi ya ile waliyokuwa wameizoea........, Dr alifikiri Mlandizi ni mikorosho tu kumbe sio na sasa kalizwa kimjinijini na aliyedhani kuwa ni swahiba yake, ogopa sana yule mama ni mafia anayejua anafanya nini kwa kila step anayopiga

Nakubaliana na wewe Ngisibara, ushamba wetu mara nyengine ndio unaotuponza.
 
  • Waziri Daftari Maua alitaka kununua vifaa hivyo huko nchi za nje bila kulipa kodi!
  • Waziri Maua Daftari alitaka kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchi za nje hadi Dar bila kulipia ushuru wa forodha.
  • Waziri Maua Daftari Maua alitaka kuingiza vifaa hivyo bila kulipa ushuru wa forodha Tanzania.
Utapeli wa kutolipa kodi kwa marafiki wasio na diplomatic immunity = conflicts of interests!

Diplomatic immunity? Hivi mawaziri wana diplomatic immunity inayowaruhusu kuvunja sheria za uliipaji wa ushuru wa forodha? Tatizo ninaloliona ni kwamba watu tumekuwa tukihalalisha mambo katika akili na vichwa vyetu kwa kudhani kwamba ndivyo yanavyotakiwa yawe. Sidhani kwamba kuna diplomatic immunity inayoruhusu Mtanzania wa cheo chochote kile aingize vitu vinavyopaswa kulipiwa ushuru nchini bila kulipa ushuru unaotakiwa.
 
Bibi Ntilie na wasomaji wengine:

Nilitumia maneno hayo ya "diplomatic immunity", kidogo niliteleza! Nilikuwa na maana ya wenye visa za ki-balozi kuwa na ruhusa ya kununua vitu na kuvisafirisha bila ya kulipia malipo ya kodi na ushuru wa forodha! Maneno halisi ni "diplomatic tax-exemptions"!

Mchakato ni kama hivi:

Mosi, kuwatumia maafisa wa ubalozi husika kununua vitu hivyo na kuvisafirisha bila kulipia kodi au ushuru wa forodha.
Pili, kama angekwenda yeye, angeweza kupewa fomu za kujaza ("diplomatic tax-exemptions forms") kuwa vinunuliwavyo ni vya kibalozi na halafu kuvisarisha bila kulipia kodi au ushuru.
Tatu, vifikapo hapo Dar es Salaam, inategemea ni nani anakwenda kuvipokea...kama ni afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, kwa mfano, angeweza kwenda na kopi ya vilivyonunuliwa na kudai kuwa vifaa hivyo vina diplomatic tax exemptions!

Huyu mama alitenda kosa...na majambo haya, pengine, tunazidi kuyapalilia na kuayarutubisha Tanzania...Tazama, hata watuhumiwa wengine bado wanaedelea kutinga bila kutengwa, hadi hapo tuhuma zao zisafishike, kama akina Chenge, Mramba, na kadhalika!
 
Jamani

Mahakama ya Rufani Tanzania imetoa ukumu ya Naibu waziri Maua Daftrai kumlipa mdeni wake 100.7M aliyemtapeli.

Je kwa hili anastahili kubaki waziri. Kosa ni wizi wa kujiaminisha.

umepata wapi hizo habari?
 
This is very interesting, hivyo hii case ni ya miaka na imeshajuulikana kama yule mama wa Mlandizi ni longo longo, Kusema kweli Mama Fatma Salimini ndio aliyomuuingiza mjini Dr. Maua. Kwani nani asiyejua kama Fatma Salimini ni Tapeli wa mji mzima huyu mama ametapeli watu wengi sana. As far as I can see huu ni ujinga mtupu kama Dr. Maua amefanya hii kitu kweli asingekuwepo hapa, Huyu mama kati ya miongoni wa matapeli usimuingize kwenye hesabu Angalia maisha yake anayoishi yeye na familia yake then judge by yourself. Kama Fatma Salimini ana hizo milioni mbona anapita kutapeli kila kona ya mji? basi angekua na maisha mazuri tu. Ujinga huu tupeni habari za maana.
 
Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Fatma alikuwa akimdai Dk Daftari Sh.210,092, 400 alizompa ili amnunulie vifaa mbalimbali kati ya mwaka 1994 na 1997, lakini mlalamikiwa hakufanya hivyo.

Vitu hivyo ni pamoja mashine ya kusindika matunda kutoka nchini Afrika Kusini, ungo (dish) la satellite, kutoka Uingereza, gari pamoja na vito vya dhahabu.

Mbali na pesa hizo taslimu, pia mlalamikaji alikuwa akimdai Dk. Daftari pesa za vitu mbalimbali alivyovichukua kwake kama vito vya dhahabu, mabati ya kujengea nyumba na milango ambavyo pia hakurudisha.

Mlalamikaji pia alikuwa akimdai mlalamikiwa pesa kiasi cha Sh200 milioni kama fidia kwa kuvunja makubaliano hayo, ambazo kwa jumla zilikuwa takribani Sh410milioni, ikiwa ni pamoja na gharama uendeshaji wa kesi hiyo.

Katika hukumu yake Jaji Kalegeya alieleza kuwa licha ya mlalamikiwa pamoja na mumewe kukataa madai hayo katika utetezi, walionekana kuwa ni matapeli.

NInachoshangaa ni nukuu ya hukumu ya kumuunganisha Dk Daftari na mumewe.,ingawa kwenye daily news sijaona,..hata hivyo

http://swahilitime.blogspot.com/2008/05/mh-maua-daftari-afiwa-na-mumewe.html
http://swahilitime.blogspot.com/2008/05/mh-maua-daftari-afiwa-na-mumewe.html</H3> SASA Kwa wana Sheria mtujuze ,.je ni sahihi kutoa hukumu kwa watu wawili mume na mke,huku ikijulikana kuwa mmoja hayupo duniani?
ni ombi tu wazee
 
hivi jamani twende Mbele na Kurudi Nyuma...Hivi utampaje mtu Million500 akununulie vitu hivyo bila maandishi yoyote? yaani pesa hizo na vitu vilivyotajwa hapo Juu, km Kweli huyu Dada Fatma ana hizo pesa kwanini asisafiri yeye mwenyewe kununua?..maana mtoaji ndio anaumia zaid mali yake kupotea kuliko mpokeaji...

hivi normally ktk kesi kama hakuna ushahidi wa Kimaandishi, Hukum inawezaje kamilika...?

Kingine Mawaziri wetu nao wanatakiwa kuwa makini sana...if possible kila mwenye madaraka ili kuweza kulinda heshima yako na heshima aliekuchagua na Wananchi pia walikuchagua kuwawakilisha.Njaa zingine noma.
 
Chuma,
Mkuu wangu verdict imeshasomwa na mama yetu Ghasia amehukumiwa kama ni TAPELI haijalishi kama yule mama alimpanfisha mkenge au laa.Huyu ni waziri mzima, msomi ambaye mahakamani ana kila advantage dhidi ya huyo Mama. Sote hapa hatukuwepo mahakamani na nina hakika maswali yote haya yaliulizwa. Kwa kila napoitazama picha hii inaonyesha wazi mama yetu alichemsha na hakika mahakama imemsetiri kiasi walichoweza. Ifike wakati tuziheshimu mahakama zetu kwani huyo Mama Salmin sidhani kama anaweza kutapeli hadi sheria..

Wapo watu wengi sana wanaaminiana tena kwa fedha zaidi ya hizo pasipo maandishi. Viongozi wengi wanachukua deal kama hizo pasipo maandishi kwani maandishi ni ushahidi tosha wa kiongozi kuvunja hata sheria ya nchi. Ukimtuma Mkandara hapa bila shaka utahitaji maandishi lakini kwa viongozi wengi wanakwepa kujulikana wanafanya mission town kwa commission kupitisha au kuleta mizigo ya watu binafsi kupitia ofisi zao.
 
Na wewe na mimi. Ulikuwepo?
Ushasema hatukuwepo wewe na mimi, halafu unaniuliza nilikuwepo tena. Wewe na Mkandara ndio mnaojulikana hamkuwepo. Hiyo mahakama gani ya mtu mbili tu, hakimu na mtuhumiwa, imekuwa gesti?
 
Alaaaah! kama wewe ulikuwepo pia umekuwaje iwe mahakama ya mtu mbili? mkuu mama yetu TAPELI ndio hukumu iliyotoka iwe sababu ni Tsh 1 au millioni. Inasikitisha kiongozi wa nchi kukutwa ana makosa ya Conning na bado yupo madarakani.....Only in Tanzania.
 
Back
Top Bottom