Dr. Mashinji mpaka sasa ndio Katibu Mkuu bora wa chama cha siasa nchini

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,701
2,000
Nimeweka kichwa cha habari hicho sio kwa sababu sina sababu ila nataka kuweka facts hapa kuwa ni kwanini Dr.Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kipindi cha miezi minne mpaka sasa ambayo amekaa ofisini na mambo ambayo yamefanyika kwa kipindi hicho cha miezi minne Naweza kusema kuwa ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha siasa kwa sasa hapa nchini.

Nasema amekaa kwa miezi minne tu kwani aliingia ofisini rasmi mwezi Juni 2016, na tangu alipoingia mipango na mikakati ambayo miminimeona ikifanyika kwa ufundi mkubwa ni kama ifuatavyo;

1. Alipoingia tu aliibadilisha Secretariat ya Makao Makuu- na kubadilisha baadhi ya wakurugenzi na wengine kuachwa kabisa na wapya kuteuliwa jambo ambalo tunashuhudia utendaji kazi za kila siku na mipango mbalimbali ikiendelea kufanyika --nitaeleza mipango hiyo hapo baadaye kidogo. Amekifanya chama kuwa taasisi imara zaidi kwani sasa ile tabia ya kila mtu kuwa msemaji wa chama inatoweka -hii naamini ni mipango ya Dr.Mashinji

2. Aliweza kuwaratibu Wabunge wake na wa UKAWA katika kuendesha mapambano mbalimbali ndani na nje ya Bunge mnaokumbuka sakata la BUNGE LIVE! UDOM nk , kiasi kwamba mipango mbalimbali ilifanyika na kuweza kuitetemesha nchi ,

3. Bunge la Bajeti , alionyesha umahiri wake kwa kuwaratibu wabunge wa CHADEMA kuigomea bajeti ambayo leo wabunge wa CCM wanalia hakuna fedha za kwenda kukagua miradi wakati walipitisha kwa mbwembwe kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila kamati kwa ajili ya ziara , sasa sijui zinatosha nauli au posho.....Ila kwa kuwa CCM hawana katibu mkuu imara hakuweza kuliona hilo na kuwasimamia wabunge wake waweze kuisimamia serikali.

4.UKUTA - mara baada ya bunge kupitisha bajeti yake kwa nguvu kubwa hakuishiwa nguvu na mbinu bali aliweza kuratibu chama chake na kuja na operation kabambe iliyojulikana kama UKUTA na kwa kweli joto la UKUTA halijawahi kutokea katika historia ya mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza hapa nchini.

UKUTA bado unaendelea kwa sababu ni mapambano ya kifikra na sio tukio la siku moja na wanachama wa UKUTA wameendelea kuongezeka kila siku , wapya kabisa ni walionyimwa mikopo ya Vyuo Vikuu ambao ni maelfu , hawa ukiwatangazia tarehe watatoka kwani hawana tumaini tena . Ni kazi ya Dr.Mashinji hiyo.

5.Ameanzisha mkakati wa kukitambulisha chama Kimataifa zaidi na aliongoza jopo la viongozi wenzake kwenda katika mataifa mbalimbali kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kidomokrasia nchini , jinsi ambavyo utawala wa sheria unaminywa nk.....La kujifunza ni kuwa anatambua kuwa Tanzania sio kisiwa na hivyo inahitaji kushirikiana na mataifa mengine mbalimbali Duniani.

6. Kadi mpya za Kilectroniki - Huu nao ni ubunifu wa Dr.Mashinji , ameweza kukishauri chama chake utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake na pia kuweza kujipatia kipato cha uhakika, ni jana tu Mbowe alitangazia taifa kuwa mkakati huo utaweza kukiingizia chama zaidi ya shilingi 13 bilioni kwa mwaka , sasa utamlinganisha na nani kwenye kubuni vyanzo vya mapato? Naambiwa wanachama tayari wameshaanza kusajiliwa kwa mfumo huu mpya silently .....

7.Ziara za viongozi wakuu ngazi za chini- ni juzi tuu Viongozi wote wakuu na wajumbe wa kamati kuu kwenda kuzungumza na viongozi wa ngazi za chini kwenye majimbo mbalimbali nchini na jana walimaliza kanda ya kati Dodoma - Mipango hii mizuri ya kuwakutanisha viongozi wakuu na wale wa chini kwenye majimbo yao ni kitu ambacho hakikuwa kikifanyika huko miaka ya nyuma ila chini ya Dr.Mashinji imewezekana -utamlinganisha na nani?

8.Kazi ya kawaida ya kuitisha vikao vya kikatiba kama kamati kuu na Baraza Kuu ameifanya sana katika kipindi hiki na kwa taarifa wale ambao hawajui ukiitisha kikao cha Kamati Kuu nyaraka zote zinaandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu.----kwa kuwa mimi sio mjumbe huko yawezekana nisijue sana juu ya ubora wa nyaraka husika ila naamini kwa vichwa vilivyomo mle ndani huwezi peleka nyaraka dhaifu ukavumiliwa .

Mafanikio mengine nitaomba muongezee kwani mimi nakumbuka haya, na hii ni kazi ya miezi minne tu hivi akikaa miaka 7 kama Dr Slaa itakuwaje kwa mipango kama hii?

Ikumbukwe kuwa kazi ya Katibu Mkuu ni kukiratibu Chama na sio kuwa mtu wa kupayuka kila siku , anatakiwa kuratibu na kuendesha chama , yeye ni Injini inapaswa kusukuma mifumo yote iweze kwenda , anaweza akalaumiwa kwa sababu watu walishazoea kuwa na Katibu Mkuu mgombea Urais ambaye alikuwa anajiprofile so wakiona wa tofauti wanafikiri amelala .

KINANA.
Niulize swali hivi tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Katibu Mkuu wa CCM Kinana amefanya kazi ipi moja ya kujenga chama chake ?

Kinana ameshindwa hata kuitisha vikao vya kikatiba vya chama chake , hivi nani anakumbuka mara ya mwisho kamati kuu ya CCM kuitishwa chini ya uongozi mpya ?

Kinana ameshindwa kwenda kukagua uhai wa chama , ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wa uhuru kwa zaidi ya miezi sita na walilalamika hadharani ......Madeni yamemzidi kiasi kwamba amezua msemo maarufu mtaani kwa sasa wa [HASHTAG]#KUNYWA[/HASHTAG] MAJI MWANANGU...

Dr.Mashinji kwa maoni yangu ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha Siasa Nchini kwa sasa na ushahidi nimeweka hapo juu , mwenye maoni tofauti aje na ushahidi kupinga hizi facts .

Naomba kuwasilisha , tupingane bila kutukanana.....ndio Maturity hiyo.
 
Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
923
1,000
hakuna kitu kama hicho , hakuna hata fact moja hapo...
Masihinji ndiyo katibu wa hovyo kweli kwa vyama vya kisiasa Tanzania wakati wa mashinji tumeshuhudia mambo ya ajabu kutoka chadema kama yafuatayo
1.Wabunge wa chadema kugomea vikao vya bunge kisa Naibu spika na katibu mashinji yupo..
2. Wabunge wa chadema hasa mwenyekiti kutoa tuhuma za wabunge wa ccm bila kupeleka takukuru na kusubiri huruma ya Rais kuingilia sakata hilo.
3. Kutafuta Udhaifu wa serikali kwa tochi hii ikumbukwe pale mbuge Lema alipo taka kuharibu mkutano wa mkuu wa mkoa Arusha.
4. Madiwani wa chadema kususia vikao halali vya halmashauri na kupoteza kiti cha umeya.
5. Chama hakina hoja tena kwenye jamii sasa zaidi ya kudandia hoja za matukio na kuambulia viroja
6. Chama kuingilia vyama vingine vya siasa kumbuka mbowe anatangaza kutomkutambua mwenyekiti wa CUF .
7.Chama kukosa ushawishi wenye tija hasa kwa kuwakilisha miswaada mbalimbali yenye tija na taifa kama Enzi za Slaa.
8.Kuendesha oparesheni UKUTA bila mkakati matokea yake ukuta ukaanguka milele.
KUNA MENGI NIANZE NA HAYO
 
Masaningala

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
543
225
Ukilinganisha na CCM, Chadema ipo mbali na ina mikakati mingi. Mkakati wa CCM ni moja tu, nao ni, kutumia vyombo vya dola kuhalalisha mambo yaende. Na hii, sio kosa lao (CCM), ni uzee unaowakabili, na uzee sio dhambi maana hauepukiki. Chadema, ambayo sasa hivi imefikisha miaka 24, bado ni mbichi na tutegemee mikakati mingi na pevu kwa ajili ya kujipanga kuongoza nchi muda si mrefu kuanzia sasa. Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu, sii sahihi kulinganisha mzee (CCM) wa miaka 62 ambae alibadilisha jina toka TANU na kuitwa CCM (1954-2016) na kijana (CDM ) wa miaka 24 mwenye damu mbichi alinaekomaza fikra zake kuangalia mbele akiwa na ndoto ya kuendana na fikra zinazoendana na maendeleo ya sayansi na technojia. Tofauti na CCM ambaye amepoteza uwezo wa kuona mbali zaidi ya kuangalia miaka ya nyuma kama rejea ya maamuzi. Huku kila mara akiwa na maneno ya rejea: " ........ wakati wa uhuru tulikuwa na ...." au anapoishiwa na hoja utamsikia: "........... Hata Mwalimu Nyerere alisema ..........." Kwa ujumla hana hoja mpya. Amezeeka huyo, sio kosa lake. Ni lazima ajikongoje kwa kutumia fimbo (vyombo vya dola). Linganifu sahihi ya CDM ni watoto waliozaliwa mwaka moja, yaani, CUF, NCCR, TLP, n.k. na sio CCM na CDM.
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
5,439
2,000
Nimeweka kichwa cha habari hicho sio kwa sababu sina sababu ila nataka kuweka facts hapa kuwa ni kwanini Dr.Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kipindi cha miezi minne mpaka sasa ambayo amekaa ofisini na mambo ambayo yamefanyika kwa kipindi hicho cha miezi minne Naweza kusema kuwa ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha siasa kwa sasa hapa nchini.

Nasema amekaa kwa miezi minne tu kwani aliingia ofisini rasmi mwezi Juni 2016, na tangu alipoingia mipango na mikakati ambayo miminimeona ikifanyika kwa ufundi mkubwa ni kama ifuatavyo;

1. Alipoingia tu aliibadilisha Secretariat ya Makao Makuu- na kubadilisha baadhi ya wakurugenzi na wengine kuachwa kabisa na wapya kuteuliwa jambo ambalo tunashuhudia utendaji kazi za kila siku na mipango mbalimbali ikiendelea kufanyika --nitaeleza mipango hiyo hapo baadaye kidogo. Amekifanya chama kuwa taasisi imara zaidi kwani sasa ile tabia ya kila mtu kuwa msemaji wa chama inatoweka -hii naamini ni mipango ya Dr.Mashinji

2. Aliweza kuwaratibu Wabunge wake na wa UKAWA katika kuendesha mapambano mbalimbali ndani na nje ya Bunge mnaokumbuka sakata la BUNGE LIVE! UDOM nk , kiasi kwamba mipango mbalimbali ilifanyika na kuweza kuitetemesha nchi ,

3. Bunge la Bajeti , alionyesha umahiri wake kwa kuwaratibu wabunge wa CHADEMA kuigomea bajeti ambayo leo wabunge wa CCM wanalia hakuna fedha za kwenda kukagua miradi wakati walipitisha kwa mbwembwe kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila kamati kwa ajili ya ziara , sasa sijui zinatosha nauli au posho.....Ila kwa kuwa CCM hawana katibu mkuu imara hakuweza kuliona hilo na kuwasimamia wabunge wake waweze kuisimamia serikali.

4.UKUTA - mara baada ya bunge kupitisha bajeti yake kwa nguvu kubwa hakuishiwa nguvu na mbinu bali aliweza kuratibu chama chake na kuja na operation kabambe iliyojulikana kama UKUTA na kwa kweli joto la UKUTA halijawahi kutokea katika historia ya mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza hapa nchini.UKUTA bado unaendelea kwa sababu ni mapambano ya kifikra na sio tukio la siku moja na wanachama wa UKUTA wameendelea kuongezeka kila siku , wapya kabisa ni walionyimwa mikopo ya Vyuo Vikuu ambao ni maelfu , hawa ukiwatangazia tarehe watatoka kwani hawana tumaini tena . Ni kazi ya Dr.Mashinji hiyo.

5.Ameanzisha mkakati wa kukitambulisha chama Kimataifa zaidi na aliongoza jopo la viongozi wenzake kwenda katika mataifa mbalimbali kueleza kuhusu hali ya kisiasa na kidomokrasia nchini , jinsi ambavyo utawala wa sheria unaminywa nk.....La kujifunza ni kuwa anatambua kuwa Tanzania sio kisiwa na hivyo inahitaji kushirikiana na mataifa mengine mbalimbali Duniani.

6. Kadi mpya za Kilectroniki - Huu nao ni ubunifu wa Dr.Mashinji , ameweza kukishauri chama chake utaratibu mzuri wa kuwatambua wanachama wake na pia kuweza kujipatia kipato cha uhakika, ni jana tu Mbowe alitangazia taifa kuwa mkakati huo utaweza kukiingizia chama zaidi ya shilingi 13 bilioni kwa mwaka , sasa utamlinganisha na nani kwenye kubuni vyanzo vya mapato? Naambiwa wanachama tayari wameshaanza kusajiliwa kwa mfumo huu mpya silently .....

7.Ziara za viongozi wakuu ngazi za chini- ni juzi tuu Viongozi wote wakuu na wajumbe wa kamati kuu kwenda kuzungumza na viongozi wa ngazi za chini kwenye majimbo mbalimbali nchini na jana walimaliza kanda ya kati Dodoma - Mipango hii mizuri ya kuwakutanisha viongozi wakuu na wale wa chini kwenye majimbo yao ni kitu ambacho hakikuwa kikifanyika huko miaka ya nyuma ila chini ya Dr.Mashinji imewezekana -utamlinganisha na nani?

8.Kazi ya kawaida ya kuitisha vikao vya kikatiba kama kamati kuu na Baraza Kuu ameifanya sana katika kipindi hiki na kwa taarifa wale ambao hawajui ukiitisha kikao cha Kamati Kuu nyaraka zote zinaandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu.----kwa kuwa mimi sio mjumbe huko yawezekana nisijue sana juu ya ubora wa nyaraka husika ila naamini kwa vichwa vilivyomo mle ndani huwezi peleka nyaraka dhaifu ukavumiliwa .

Mafanikio mengine nitaomba muongezee kwani mimi nakumbuka haya, na hii ni kazi ya miezi minne tu hivi akikaa miaka 7 kama Dr Slaa itakuwaje kwa mipango kama hii?

Ikumbukwe kuwa kazi ya Katibu Mkuu ni kukiratibu Chama na sio kuwa mtu wa kupayuka kila siku , anatakiwa kuratibu na kuendesha chama , yeye ni Injini inapaswa kusukuma mifumo yote iweze kwenda , anaweza akalaumiwa kwa sababu watu walishazoea kuwa na Katibu Mkuu mgombea Urais ambaye alikuwa anajiprofile so wakiona wa tofauti wanafikiri amelala .

KINANA.

Niulize swali hivi tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Katibu Mkuu wa CCM Kinana amefanya kazi ipi moja ya kujenga chama chake ?

Kinana ameshindwa hata kuitisha vikao vya kikatiba vya chama chake , hivi nani anakumbuka mara ya mwisho kamati kuu ya CCM kuitishwa chini ya uongozi mpya ?

Kinana ameshindwa kwenda kukagua uhai wa chama , ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wa uhuru kwa zaidi ya miezi sita na walilalamika hadharani ......Madeni yamemzidi kiasi kwamba amezua msemo maarufu mtaani kwa sasa wa [HASHTAG]#KUNYWA[/HASHTAG] MAJI MWANANGU...

Dr.Mashinji kwa maoni yangu ndiye Katibu Mkuu bora zaidi wa Chama cha Siasa Nchini kwa sasa na ushahidi nimeweka hapo juu , mwenye maoni tofauti aje na ushahidi kupinga hizi facts .

Naomba kuwasilisha , tupingane bila kutukanana.....ndio Maturity hiyo.
Umemsifia Mashinji kama ulivyoelekezwa sawa! Umeharibu ulipomfananisha na Kinana. Utalinganishaje chama kilicho madarakani chenye nguvu na vyama vyetu hivi. Hivo kweli unamjua Kinana au humjui. Mashinji kijana wa juzi tu bado ananuka maziwa unamfananisha na gwiji la siasa. Aaaaaah hata kama umetumwa tumia na wewe akili yako. Badala ya kumhimiza Mashinji ajitahidi afikie level za kina Kinana unaanza kumvimbisha kichwa kitu ambacho wala hakitamsaidia. Bado Chadema ipo mbali sana kisiasa. Bado hata haijaweza kuweka misingi ya demokrasia ndani ya chama. Bado. Bado leo hii ukihoji kitu tu ambacho kitawagusa watu fulani utazushiwa wewe ni msaliti. Bado saaana wajameni. Bado wanayumbishwa na mafedha ya wenye pesa. Imagine wale chama kilikua kinasema ni mafisadi leo wako wapi. Wamekumbatiwa na wamesafishwa. No more mafisadi wala watuhumiwa na wala ajenda hizo zilishapigwa marufuku. Tuliambiwa "shut-up". Hapo ni baada ya wageni wale kujua wameshakiweka chama kwapani. Hakuna ujanja. Na hakuna atakayeamini chama hiki tena. Kumbe sera ni utafutaji vyanzo vya mapato. Anyway wajinga ndio waliwao. Na mimi mmojawao lakini sasa nilishazinduka
 
mbandeon

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
1,250
1,500
Yote pumba ila 2 na 3 pumba square, hivi ukisema kuweza kuitetemesha nchi unakusudia nini ? angalau basi moja kati ya hayo unayosema lingefanyika maana naona hadi leo Bunge halionyeshwi live na huyo masinzi wako ameufyata na Ukuta wa biscuit sijawahi kuushuhudia zaidi ya kuja na excuse kama ilivo tabia ya loser.
 
Hapa unastahili buku jero umechangia kiwango cha ChinI sana
 
Top Bottom