Dr. Magufuli yuko sahihi na serikali yake, tubadilike

Wasalaam,

Juzi hotuba ya Mh.Rais kuna baadhi ya watu wanaiponda, mimi nashangaaa sana hivi watanzania tukoje? Nchi hii jamani tulifikia pabaya sana kwa serikali kuendeshwa kwa ghiliba, uongo, udanganyifu, unafiki, na kupakaziana bila kuwa wakweli, tukaomba tumpate Rais atakae kuwa mkweli, asiyeogopa lawama za ndugu, marafiki, na wananchi ili tusonge na kutoka tulipo.

Juzi Mh.Rais akiwa Kagera amewaambia wanakagera, waanga wa tetemeko na wananchi kwa ujumla ukweli uliyomchungu na usiopingika kuwa serikali haiko kwa ajili ya mtu mmoja mmoja bali kwa maslahi ya jumla ya wananchi wote.

Sisi watanzania tulikuwa tumezoea sana maisha malaini sana, ya msaada, tegemezi na kulialia na kununa, mfn. mtu akiwa mfanyakazi anakuwa na tegemezi wengi sana mjini na kijijini wote wanataka salary yake ika wengine sasa hawafanyi kazi kisa kaka, dada, mjomba n.k yupo bandari, TRA, TANESCO n.k

Kila mtu sasa afanye kazi na siyo kumtegemea mtu au mambo ya kona kona ili usawa uwepo na nchi isongeee. Nchi inaendelea kwa kuwa na producers wengi, sisi tuna production man-force kubwa ila wategeaje na wazembe.

Ifike wakati sasa ukweli usemwe hata kama ni chungu na ina kera kiasi gani. Awamu iliyopita watu walipenda kusikia uongo na maneno ya kuremba na kubembelezwa.
==========

JAMII LEO


angekuwa mkweli angeanza kusema ukweli wakati wa uchangishaji kuwa pesa zile sio za waathirika mana yeye mwenyewe alidanganya umma kuwa watu wasaidie kuchangia waathirika badala ya miundo mbinu ya umma
 
Hao ufipa wasipinge uhalisia aisee! Mtu ajifunze kujikwamua mwenyewe ndo maana wazungu hawana tegemezi.
Pia serikali ijifunze kutotegemea kodi za wananchi pamoja na misaada ya wahisani nadhani hapo wananchi watajifunza pia
 
Ni bora uambiwe ujitambue kuliko kupewa ahadi za uongo.
U.A.E palitokea mafuliko makubwa magari mengi ya raia na wale ambao sio raia yalihalibika mengine kupotea.
Pamoja na utajili wake hakuna mtu aliyelipwa gari,au kutengenezewa nyumba .bali selikali yao ilitengeneza miundo mbinu mipya kudhibiti hali hiyo.
Lakini Indonesia na Haiti serikali iliwajengea wananchi waliopata matatizo...Pamoja na ilo mbona mnatoa mifano mibaya tu kulinganisha na Tanzania serikali inapokosea...vipi mifano mizuri mfano kuheshimu katiba ya nchi na Demokrasia kama nchi nyingine hamsemi...Pole yenu ambao mnategemea kulinda maovu na makosa ili mpate nafasi au mkate
 
Watu hawana akili...hivi ukijengewa nyumba afu hamna shule...hospitali...barabar unadhani utakua umesaidia familia au jamii

unajua lakini basic human needs? ni sayansi ya la tano tu
1. food
2. shelter
3. clothing

sasa we kuanzia leo acha ujingabna jifunze kwanza vitu vya muhimu kwa binadamu na uache ushabiki shule wangapi hawajaenda wanaishi, hospitali dawa za kienyeji mtu anawezatumia, barabara tunazo mbovu miaka yote, sasa nipe mbadala wa ivyo vitatu
 
Tatizo Magufuli anasema ukweli ambao hautakiwi kusemwa hadharani! Watanzania wamezoea uupindishe kidogo ukweli ndo watakuelewa
Mimi sidhani kama watu wanatatizo na ukweli wa Mheshimiwa, ila kumbuka kuwa si kila ukweli unamanufaa ndani yake! Wala msifikiri kuwa watu wanatamani aseme uongo, lahasha! Watu wanataka atende haki na kumbukeni kutenda haki sio hisani, hiyo ni haki ya msingi!
 
Back
Top Bottom