Dr. Magufuli ni Rais bora wa karne

Dr. Magufuli ni Rais bora wa karne

same yetu

Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
38
Reaction score
30
Kama mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yangu, kwa muda wa mwaka mzima nimejitahidi kufuatilia nyendo na uzalendo wa kiongozi wetu ndugu Dr. Jemedari, Mzalendo, na mwana maendeleo John Pombe Magufuli na kuja na jibu ambalo sioni wa kumlinganisha naye tangu tupate uhuru. Ndugu Magufuli nimeweza kumtofautisha na wengine waliotangulia kwa mambo kadhaa yafuatayo,

UTAWALA BORA
-Rais wetu amejitahidi sana kuweka utawala bora wa kupigiwa mfano. Amejitahidi kuwajengea uwezo na ujasiri wote walio chini yake kuanzia viongozi wenzie mpaka wananchi. Kwa sasa wote tunatembea huku tukijiamini. Viongozi wana ujasiri wa kukemea jambo lolote ambalo lipo kinyume na maslahi na manufaa kwa maendeleo ya nchi. Kipindi cha nyuma wenye hela walikuwa wanaogopeka ila sasa kila mtu anamheshimu mwenzie bila kujali wadhifa na uwezo wa mtu kifedha. Kwa hili amepata alama 100

UCHUMI-KILIMO
-Dah hapa ndio sijui niseme nini. Kila unapogusa unafurahi na kutoa machozi ya furaha. Viwanda lukuki vimejengwa na vinaendelea kujengwa, tutake nini wananchi. Umeme ndio huo, ni mwendo wa stigler gorge kwa kwwnda mbele. Hakuna maendeleo bila nishati wezeshi ya kuchachafya maendeleo. Watu wanafiki wanasema mbona hajawekeza kwenye kilimo kukuza viwanda, wamesahau kwa ukizungumzia kilimo unazungumzia jambo kubwa sana.

Niwape tu uelewa nini maana ya kilimo, kilimo kina matawi matano ambayo ni yafuatayo
-Sayansi ya udongo
-Mifugo
-Kilimo cha mazao
-Agromechanics(Mashine za uzalishaji)
-Agroeconomics(Uchumi wa kilimo)

Sasa katika hayo matano kiongozi wetu ameyafanyia kazi ipasavyo, wanasayansi wanafanya tafiti kila siku ni udongo gani unafaa kwa zao gani, majosho kwa mifugo yamejengwa mengi, mashine za kilimo zimetolewa kodi, mbolea zimepewa ruzuku, na pia anajitahidi kudhibiti bei za mazao ili wakulima wanufaike kama kwenye korosho. Nini tunataka zaidi ya hili

UCHUMI-NISHATI
-Hapa wenyewe mmeshuhudia stigler gorge, rea pamoja na miradi mikubwa ya umeme pale kinyerezi na mradi mkubwa wa umeme kwenda kanda ya kati.

UCHUMI-USAFIRISHAJI
-Barabara zisizo na idadi na kilometa za kutosha zinaendelea kujengwa, huku tumeanza mradi wa kuboresha reli ya kati, huku SGR inaendelea na ujenzi. Hivi watanzania tumelogwa na nani tushindwe kuelewa hili jambo dogo. Wote tutakuwa na ahueni, mwenye kupanda ndege ATCL inaendelea kuimarika, wenye kupanda treni ndio hivyo. Tanzania itakuwa kama kijiji, muda mchache unafika uendako

UCHUMI-ELIMU
-Bila elimu hakuna Taifa. Elimu bure ndio hiyo, shule zinazidi kuboreshwa kuanzia za zamani hadi za kipindi cha kati. Vyuo vikuu vimefurika wanafunzi kwa sababu ya wengi kupata mkopo. Huu ndio wakati wa Taifa kuinuka kielimu.

MAJI
-Miradi mingi ya maji inaendelea kujengwa. Nyie wenyewe ni mashahidi ndio maana hata wakati fulani kuna mkoa mmoja waliomba mwekezaji wa madini atolewe ili tanki la maji lijengwe.

NB; Hakuna wa kufanana naye kwani mambo makubwa yanafanyika kwa kipindi kimoja ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi. Tunakuombea kwa Mungu uzidi kuimarisha maisha ya wananchi wako

Kutoka CHANGOKO-SAME
MZALENDO KINDAKINDAKI
CCM OYEEEEEE
 
Mkuu Unazungumzia karne Ipi?
Ama kweli "penzi kitovu cha Uzembe"
 
Umeegemea upande mmoja. Ni vizuri ungeoweka na mabaya pia aliyofanya/anayofanya ili uzi ubalance maana yeye ni binadamu anakosea vilevile sio muda wote anafanya mabaya au mazuri. Nikikumbuka aliposema KWANI KWENYE KAMPENI NILIWAAHIDI NITALETA TETEMEKO? hapo huwaga nasema kweli tunae kiongozi mzalendo
 
Halafu ni mbunifu, fikiria amebuni na kutengeneza vitambulisho visivyo na picha, jina wala sahihi ya mhusika na kuwaagiza wakuu wa mikoa wahakikishe wameviuza kwa wamachinga.. Raisi gani ambae amewahi kuja wazo bora kabisa kama hilo.. Tena nashauri katika hiyo bei ya vitambulisho, aweke VAT ili mapato yazidi kuongezeka..
 
Yote mema, kwani kwa hili kuna mtu anateseka
 
Hatujali kama wao wanateseka.. Hapa Rais amebuni kitu kizuri sana..

Atengeneze vitambulisho vingine sasa ambavyo kila raia mwenye umri wa kuanzia miaka 18, ni lazima akinunue kwa ajili ya kutambuliwa.. Imagine kama kitauzwa elfu 10 vat exclusive.. Ataingiza kiasi gani..

Hongera Raisi..
 
Kama mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yangu, kwa muda wa mwaka mzima nimejitahidi kufuatilia nyendo na uzalendo wa kiongozi wetu ndugu Dr. Jemedari, Mzalendo, na mwana maendeleo John Pombe Magufuli na kuja na jibu ambalo sioni wa kumlinganisha naye tangu tupate uhuru. Ndugu Magufuli nimeweza kumtofautisha na wengine waliotangulia kwa mambo kadhaa yafuatayo,

UTAWALA BORA
-Rais wetu amejitahidi sana kuweka utawala bora wa kupigiwa mfano. Amejitahidi kuwajengea uwezo na ujasiri wote walio chini yake kuanzia viongozi wenzie mpaka wananchi. Kwa sasa wote tunatembea huku tukijiamini. Viongozi wana ujasiri wa kukemea jambo lolote ambalo lipo kinyume na maslahi na manufaa kwa maendeleo ya nchi. Kipindi cha nyuma wenye hela walikuwa wanaogopeka ila sasa kila mtu anamheshimu mwenzie bila kujali wadhifa na uwezo wa mtu kifedha. Kwa hili amepata alama 100

UCHUMI-KILIMO
-Dah hapa ndio sijui niseme nini. Kila unapogusa unafurahi na kutoa machozi ya furaha. Viwanda lukuki vimejengwa na vinaendelea kujengwa, tutake nini wananchi. Umeme ndio huo, ni mwendo wa stigler gorge kwa kwwnda mbele. Hakuna maendeleo bila nishati wezeshi ya kuchachafya maendeleo. Watu wanafiki wanasema mbona hajawekeza kwenye kilimo kukuza viwanda, wamesahau kwa ukizungumzia kilimo unazungumzia jambo kubwa sana.

Niwape tu uelewa nini maana ya kilimo, kilimo kina matawi matano ambayo ni yafuatayo
-Sayansi ya udongo
-Mifugo
-Kilimo cha mazao
-Agromechanics(Mashine za uzalishaji)
-Agroeconomics(Uchumi wa kilimo)

Sasa katika hayo matano kiongozi wetu ameyafanyia kazi ipasavyo, wanasayansi wanafanya tafiti kila siku ni udongo gani unafaa kwa zao gani, majosho kwa mifugo yamejengwa mengi, mashine za kilimo zimetolewa kodi, mbolea zimepewa ruzuku, na pia anajitahidi kudhibiti bei za mazao ili wakulima wanufaike kama kwenye korosho. Nini tunataka zaidi ya hili

UCHUMI-NISHATI
-Hapa wenyewe mmeshuhudia stigler gorge, rea pamoja na miradi mikubwa ya umeme pale kinyerezi na mradi mkubwa wa umeme kwenda kanda ya kati.

UCHUMI-USAFIRISHAJI
-Barabara zisizo na idadi na kilometa za kutosha zinaendelea kujengwa, huku tumeanza mradi wa kuboresha reli ya kati, huku SGR inaendelea na ujenzi. Hivi watanzania tumelogwa na nani tushindwe kuelewa hili jambo dogo. Wote tutakuwa na ahueni, mwenye kupanda ndege ATCL inaendelea kuimarika, wenye kupanda treni ndio hivyo. Tanzania itakuwa kama kijiji, muda mchache unafika uendako

UCHUMI-ELIMU
-Bila elimu hakuna Taifa. Elimu bure ndio hiyo, shule zinazidi kuboreshwa kuanzia za zamani hadi za kipindi cha kati. Vyuo vikuu vimefurika wanafunzi kwa sababu ya wengi kupata mkopo. Huu ndio wakati wa Taifa kuinuka kielimu.

MAJI
-Miradi mingi ya maji inaendelea kujengwa. Nyie wenyewe ni mashahidi ndio maana hata wakati fulani kuna mkoa mmoja waliomba mwekezaji wa madini atolewe ili tanki la maji lijengwe.

NB; Hakuna wa kufanana naye kwani mambo makubwa yanafanyika kwa kipindi kimoja ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi. Tunakuombea kwa Mungu uzidi kuimarisha maisha ya wananchi wako

Kutoka CHANGOKO-SAME
MZALENDO KINDAKINDAKI
CCM OYEEEEEE
Huna uzalendo wowote bwege wew unamkejel mh Rais!!!!Hivi kumbe tafsr ya uzalendo awamu hii ni kumsifia rais hata kma anatupeleka kusikojulikana?
 
Hakuna aliyetumia muda kuwapamba akina Nyerere, Mandela, Kikwete..
walichokifanya kilionekana na kuwafurahisha wengi..
Tatizo ni kukitakasa kinyesi..
mbona nyinyi watoto mchelemchele kazi mnayo !
tapatalk_1544846262535.jpeg
 
Kama mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yangu, kwa muda wa mwaka mzima nimejitahidi kufuatilia nyendo na uzalendo wa kiongozi wetu ndugu Dr. Jemedari, Mzalendo, na mwana maendeleo John Pombe Magufuli na kuja na jibu ambalo sioni wa kumlinganisha naye tangu tupate uhuru. Ndugu Magufuli nimeweza kumtofautisha na wengine waliotangulia kwa mambo kadhaa yafuatayo,

UTAWALA BORA
-Rais wetu amejitahidi sana kuweka utawala bora wa kupigiwa mfano. Amejitahidi kuwajengea uwezo na ujasiri wote walio chini yake kuanzia viongozi wenzie mpaka wananchi. Kwa sasa wote tunatembea huku tukijiamini. Viongozi wana ujasiri wa kukemea jambo lolote ambalo lipo kinyume na maslahi na manufaa kwa maendeleo ya nchi. Kipindi cha nyuma wenye hela walikuwa wanaogopeka ila sasa kila mtu anamheshimu mwenzie bila kujali wadhifa na uwezo wa mtu kifedha. Kwa hili amepata alama 100

UCHUMI-KILIMO
-Dah hapa ndio sijui niseme nini. Kila unapogusa unafurahi na kutoa machozi ya furaha. Viwanda lukuki vimejengwa na vinaendelea kujengwa, tutake nini wananchi. Umeme ndio huo, ni mwendo wa stigler gorge kwa kwwnda mbele. Hakuna maendeleo bila nishati wezeshi ya kuchachafya maendeleo. Watu wanafiki wanasema mbona hajawekeza kwenye kilimo kukuza viwanda, wamesahau kwa ukizungumzia kilimo unazungumzia jambo kubwa sana.

Niwape tu uelewa nini maana ya kilimo, kilimo kina matawi matano ambayo ni yafuatayo
-Sayansi ya udongo
-Mifugo
-Kilimo cha mazao
-Agromechanics(Mashine za uzalishaji)
-Agroeconomics(Uchumi wa kilimo)

Sasa katika hayo matano kiongozi wetu ameyafanyia kazi ipasavyo, wanasayansi wanafanya tafiti kila siku ni udongo gani unafaa kwa zao gani, majosho kwa mifugo yamejengwa mengi, mashine za kilimo zimetolewa kodi, mbolea zimepewa ruzuku, na pia anajitahidi kudhibiti bei za mazao ili wakulima wanufaike kama kwenye korosho. Nini tunataka zaidi ya hili

UCHUMI-NISHATI
-Hapa wenyewe mmeshuhudia stigler gorge, rea pamoja na miradi mikubwa ya umeme pale kinyerezi na mradi mkubwa wa umeme kwenda kanda ya kati.

UCHUMI-USAFIRISHAJI
-Barabara zisizo na idadi na kilometa za kutosha zinaendelea kujengwa, huku tumeanza mradi wa kuboresha reli ya kati, huku SGR inaendelea na ujenzi. Hivi watanzania tumelogwa na nani tushindwe kuelewa hili jambo dogo. Wote tutakuwa na ahueni, mwenye kupanda ndege ATCL inaendelea kuimarika, wenye kupanda treni ndio hivyo. Tanzania itakuwa kama kijiji, muda mchache unafika uendako

UCHUMI-ELIMU
-Bila elimu hakuna Taifa. Elimu bure ndio hiyo, shule zinazidi kuboreshwa kuanzia za zamani hadi za kipindi cha kati. Vyuo vikuu vimefurika wanafunzi kwa sababu ya wengi kupata mkopo. Huu ndio wakati wa Taifa kuinuka kielimu.

MAJI
-Miradi mingi ya maji inaendelea kujengwa. Nyie wenyewe ni mashahidi ndio maana hata wakati fulani kuna mkoa mmoja waliomba mwekezaji wa madini atolewe ili tanki la maji lijengwe.

NB; Hakuna wa kufanana naye kwani mambo makubwa yanafanyika kwa kipindi kimoja ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi. Tunakuombea kwa Mungu uzidi kuimarisha maisha ya wananchi wako

Kutoka CHANGOKO-SAME
MZALENDO KINDAKINDAKI
CCM OYEEEEEE
AWAMU HII KILA MTU ATAZUNGUMZA LA KWAKE ILA MIMI UPANDE WANGU NAONA KILA KITU KIMESHAHARIBIKA KWANGU

SIONI HATA NINACHOKIPATA ZAIDI YA SHIDA
 
Back
Top Bottom