Dr. Magufuli ni Rais bora wa karne

Dr. Magufuli ni Rais bora wa karne

Kama mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yangu, kwa muda wa mwaka mzima nimejitahidi kufuatilia nyendo na uzalendo wa kiongozi wetu ndugu Dr. Jemedari, Mzalendo, na mwana maendeleo John Pombe Magufuli na kuja na jibu ambalo sioni wa kumlinganisha naye tangu tupate uhuru. Ndugu Magufuli nimeweza kumtofautisha na wengine waliotangulia kwa mambo kadhaa yafuatayo,

UTAWALA BORA
-Rais wetu amejitahidi sana kuweka utawala bora wa kupigiwa mfano. Amejitahidi kuwajengea uwezo na ujasiri wote walio chini yake kuanzia viongozi wenzie mpaka wananchi. Kwa sasa wote tunatembea huku tukijiamini. Viongozi wana ujasiri wa kukemea jambo lolote ambalo lipo kinyume na maslahi na manufaa kwa maendeleo ya nchi. Kipindi cha nyuma wenye hela walikuwa wanaogopeka ila sasa kila mtu anamheshimu mwenzie bila kujali wadhifa na uwezo wa mtu kifedha. Kwa hili amepata alama 100

UCHUMI-KILIMO
-Dah hapa ndio sijui niseme nini. Kila unapogusa unafurahi na kutoa machozi ya furaha. Viwanda lukuki vimejengwa na vinaendelea kujengwa, tutake nini wananchi. Umeme ndio huo, ni mwendo wa stigler gorge kwa kwwnda mbele. Hakuna maendeleo bila nishati wezeshi ya kuchachafya maendeleo. Watu wanafiki wanasema mbona hajawekeza kwenye kilimo kukuza viwanda, wamesahau kwa ukizungumzia kilimo unazungumzia jambo kubwa sana.

Niwape tu uelewa nini maana ya kilimo, kilimo kina matawi matano ambayo ni yafuatayo
-Sayansi ya udongo
-Mifugo
-Kilimo cha mazao
-Agromechanics(Mashine za uzalishaji)
-Agroeconomics(Uchumi wa kilimo)

Sasa katika hayo matano kiongozi wetu ameyafanyia kazi ipasavyo, wanasayansi wanafanya tafiti kila siku ni udongo gani unafaa kwa zao gani, majosho kwa mifugo yamejengwa mengi, mashine za kilimo zimetolewa kodi, mbolea zimepewa ruzuku, na pia anajitahidi kudhibiti bei za mazao ili wakulima wanufaike kama kwenye korosho. Nini tunataka zaidi ya hili

UCHUMI-NISHATI
-Hapa wenyewe mmeshuhudia stigler gorge, rea pamoja na miradi mikubwa ya umeme pale kinyerezi na mradi mkubwa wa umeme kwenda kanda ya kati.

UCHUMI-USAFIRISHAJI
-Barabara zisizo na idadi na kilometa za kutosha zinaendelea kujengwa, huku tumeanza mradi wa kuboresha reli ya kati, huku SGR inaendelea na ujenzi. Hivi watanzania tumelogwa na nani tushindwe kuelewa hili jambo dogo. Wote tutakuwa na ahueni, mwenye kupanda ndege ATCL inaendelea kuimarika, wenye kupanda treni ndio hivyo. Tanzania itakuwa kama kijiji, muda mchache unafika uendako

UCHUMI-ELIMU
-Bila elimu hakuna Taifa. Elimu bure ndio hiyo, shule zinazidi kuboreshwa kuanzia za zamani hadi za kipindi cha kati. Vyuo vikuu vimefurika wanafunzi kwa sababu ya wengi kupata mkopo. Huu ndio wakati wa Taifa kuinuka kielimu.

MAJI
-Miradi mingi ya maji inaendelea kujengwa. Nyie wenyewe ni mashahidi ndio maana hata wakati fulani kuna mkoa mmoja waliomba mwekezaji wa madini atolewe ili tanki la maji lijengwe.



NB; Hakuna wa kufanana naye kwani mambo makubwa yanafanyika kwa kipindi kimoja ndani ya miaka mitatu tu ya uongozi. Tunakuombea kwa Mungu uzidi kuimarisha maisha ya wananchi wako

Kutoka CHANGOKO-SAME
MZALENDO KINDAKINDAKI
CCM OYEEEEEE
Mods mpeni hukumu ya life ban huyu mwandishi kwa kunifanya nifurahie kazi nzuri ya Rais Magufuli, kiasi kwamba furaha Yangu imenipa na presha na kwa sasa nimelazwa wodi ya MOI Muhimbili kwa kosa la kuunga mkono juhudi.

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Karibu, unganeni ili mlete ushindani bora kwenye uchaguzi mkuu. Ila mkumbuke CCM ndio atashindwa kwa kutegemea wapiga kura wazalendo. CCM chama bora daima
USA na EU zimesema zitausimamia uchaguzi mkuu!!!.safari hiii imekula kwenu.hapo vipi?!..
icon_lol.gif
icon_lol.gif
icon_lol.gif
icon_lol.gif
 
Nyie minyoo mipya mlioajiliwa juzi juzi kuja huku kusifia ujinga na kuharibu jukwaa letu
 
Kwa mfano umeelezea vema Sana lakin swali unazani watu wote hayo hwayaoni? Nadhan kwa vile wote tuko nchi hii tunaona kwann watu bado wanapinga kwa nguvu zote kwanini? Jiulize piano tena ni wengi sana
 
Kwa mfano umeelezea vema Sana lakin swali unazani watu wote hayo hwayaoni? Nadhan kwa vile wote tuko nchi hii tunaona kwann watu bado wanapinga kwa nguvu zote kwanini? Jiulize piano tena ni wengi sana
Wanaopinga wote sio wazalendo, labda maslahi yao yameguswa kwa kuinyoosha nchi kwenye njia sahihi
 
Hii ndio post mbovu iliyovunja rekodi jf kwa mwaka 2018.unamsifia mwanaume mwenzio ???
 
Hivi ukitaka uitwe mzalendo itakubidi uwe mshabiki wa chama gani cha siasa?
 
Hii ndio post mbovu iliyovunja rekodi jf kwa mwaka 2018.unamsifia mwanaume mwenzio ???
Acha nimsifie, moja ni mwana CCM mwenzangu, mzalendo mwenzangu, na zaidi ya yote ni Rais wangu tena bora wa karne.
 
View attachment 968954
Ni kweli Magufuli ni Laisi bora wa Karne?!
Tatizo la shule kama hizi limesababishwa na wazazi. Watu kumi wanahitaji kijiji na wapewe huduma za jamii zote. Hata ingekuwa marekani bajeti hiyo ni ngumu. Watu wanajiamulia tu tutaishi, wanashawishiwa na waomba kura ombeni kijiji na mwomba kura atapigania. Akishapata kura anawatelekeza. Ndo maana Nyerere aliamua kutukusanya katika vijiji ili iwr rahisi kupata huduma za jamii. Tumesambaratika tena.
 
Tatizo la shule kama hizi limesababishwa na wazazi. Watu kumi wanahitaji kijiji na wapewe huduma za jamii zote. Hata ingekuwa marekani bajeti hiyo ni ngumu. Watu wanajiamulia tu tutaishi, wanashawishiwa na waomba kura ombeni kijiji na mwomba kura atapigania. Akishapata kura anawatelekeza. Ndo maana Nyerere aliamua kutukusanya katika vijiji ili iwr rahisi kupata huduma za jamii. Tumesambaratika tena.
😛😛😛😛😛😛 upo sawa kiongozi
 
Back
Top Bottom