Dr MAGHUFULI ANAEPAMBANA NA WAGOMBEA WENYE UWEZO MDOGO(DHAIFU)
Episode 2
Dr Maghufuli , ni kiongozi mwanasiasa na mwanasayansi nguli ambaye naamini atachaguliwa kwa kishindo kuwa Rais Wa 5, ataweka historia katika nchi za kiafrika na Tanzania kupata Rais mwanasayansi .
Dr Maghufuli , ni kiongozi mpole kimuonekano na mkali kimaamuzi hasa kwa manufaa ya taifa
Dr Maghufuli , ni kiongozi Wa ndoto za watanzania wengi katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi Wa kati( upper).
Dr Maghufuli, ni kiongozi aliyewekeza kwenye mioyo ya watanzania hasa kujitolea kuwatumikia kwa Moyo wote watanzania pindi apatapo nafasi ya kuwatumikia
Dr Maghufuli, ni chaguo la mungu kwa kipindi hiki kwani uteuzi wake Dodoma ulijidhihirisha uwepo Wa nguvu ya mungu ,
Dr Maghufuli, ni kiongozi ambaye ni mfuatiliaji kwa kile anachokiagiza mfano ni kutembelea mizani ya kupima magari wakati Wa usiku jambo lililopelekea kujua madhaifu ya mizani na rushwa iliyokithiri hali iliyopelekea kubadilisha wafanyakazi zaidi ya 400 , na kuweka wataalam zaidi
Dr Maghufuli, ni kiongozi mwenye maono ya mbali na msimamizi mzuri sana Wa katiba na sheria za nchi hali ambayo , wakati Wa uuzaji nyumba za serikali ambapo baraza la mawaziri chini ya Rais mkapa na Waziri mkuu wake Frederick Sumaye na mawaziri wote waliridhia kuuza nyumba za serikali kwa mujibu Wa sheria na kuanza kujenga nyumba mpya,
Dr Maghufuli, ni kiongozi anaesimamia maamuzi yaliyokwisha pitishwa na vikao vya maamuz ikiwemo sheria husika , mfano ni meli ya samaki
Dr.Maghufuli ni kiongozi anaependa heshima yake na nchi yake mwenyewe , hivyo tutegemee majirani zetu na nchi wafadhili kutuhwshimu na kutuogopa kwani msimamo wetu utakuwa wazi kama nchi
Dr Maghufuli, ni kiongozi ambae watanzania sio tu wanamwamini Bali pia wana imani na rekodi yake ya utendaji, uadilifu na uzalendo Wa nchi, ingekuwa kunatolewa zawadi ya waziri bora katika utendaji serikali ya awamu ya nne , Dr maghufuli angeibuka kwa asilimia isiyopungua 95%
Dr Maghufuli, ndiye muarobaini Wa mfumo na matatizo ya CCM ya muda mrefu ,na endapo atateua timu ifuatayo afanye nayo kazi upande Wa CCM na Ikulu
TIMU YA KAZI NDANI YA CCM NA IKULU
1 . Makam Mkiti bara , hii nafasi inamfaa zaidi Makongoro Nyerere, huyu nguli Wa siasa za jukwaani na kivitendo ni kiongozi anayechukia rushwa kwa vitendo na mafisadi hivyo ataisafisha CCM na kuirudisha CCM yenye heshima kubwa na kwa ushawishi wake ataweza pia kumshawishi Dr slaa arudi CCM na kwa Mara ya kwanza CCM itazaliwa upya tena katika misingi yake ya wakulima na wafanyakazi
2 Katibu Mkuu,-Dr Emmanuel Nchimbi, huyu ni mjumbe Wa muda mrefu kwenye kamati kuu nafikiri kuliko mwanaccm yeyote kwa sasa , japo aliteleza kwenye kwa tamko lake kipindi cha kamati kuu huko Dodoma , anatakiwa apewe cancelling ya kutosha na kumuweka sawa ikiwemo kwenda mafunzoni ndani na nje ya nchi ili akitumikie chama vizuri
3 Abdurahman Kinana , huyu ni Katibu mkuu aliyeirudishia CCM thamani yake , kwa kuwa umri umeenda na alikuwa katangaza kustaafu siasa, inatakiwa kianzishwe kitengo au idara ya kuwafunza makatibu Wa CCM na yeye awe Mwalimu wao kwani kaperfom vizur katika changamoto nyingi , pia awe mshauri Wa CCM .
4 , Philip Mangula , huyu anatakiwa aende ikulu kuwa mshauri wa mambo ya kisiasa , kwani anaifaham siasa vyema pia ni muadilifu , mzalendo na mfia chama na nchi na wala sio Mtu,
5 Dr Salim Ahmed Salim, Aende ikulu kuwa mshauri Wa mambo ya kiserikali , huyu ni moja ya kiongoz muadilifu, mzalendo na asiye na makuu, pia ni nvuli Wa uongoz Wa kimataifa na pia Waziri mkuu mstaafu ,
WAPINZANI WA Dr MAGHUFULI KWA UJUMLA WAKE
Wapinzani wake, ni viongozi mangwini ambao ,uwezo wao sio mkubwa Bali kuzungumza uongo ( hadaa)
Wapinzani wake, ni viongozi waliojipambanua kwa uchafu zaidi ikiwemo ufisadi mkubwa toka waingie kwenye siasa
Wapinzani wake, wamejipambanua kwa usaliti Wa mambo yenye maslahi kitaifa ikiwemo Muungano
Wapinzani wake, wameonekana ni waroho Wa madaraka na sio waroho Wa kutatua umasikini na kulinda rasilimali za watanzania
Wapinzani wake, wamejipambanua kama wafitini, wachochanganishi, na wanaoamini katika uwezo Wa pesa haramu
Wapinzani wake, wamefeli katika mambo mengi na kushindwa kuaminika popote pale
Wapinzani wake , wanaagenda binafsi iliyojengeka kikanda,kidini ,kikabila na mwisho wake ni kuleta mpasuko Wa kitaifa na machafuko yatakayohatarisha iman ya nchi, hili limejidhirisha kwa wao wenyewe kusalitiana ,
Ubinafsi, na chuki ndio falsafa yao.
" Dr Maghufuli mteule Wa mungu, ambaye hakuwahi kuuota urais kama mfalme Daud na Suleiman ambao hawakuwahi kuuota ufalme Bali kwa Mapenzi ya mungu yote yalitimia kama yatakavyotimia kwa Dr maghufuli oktoba 25"
MWISHO.