Dr Magufuli Baada ya kuapishwa naomba uanze HESLB

Dr Magufuli Baada ya kuapishwa naomba uanze HESLB

Uongo usiofichika...hili neno "Budget exhausted" litawahusu watu wengi sana mwaka huu.
 
Huenda kukawa na habari njema mwaka huu kuliko miaka mingine yote iliyopita, si mnajua danganya toto tena jamani au mmesahau...
 
Mlipewa nafasi ya kusoma bure chuo kikuu mkang'ng'ana na CCM..imekula kwenu..tena naomba mkose mikopo hiyo..na wazazi wazidi kuchangishwa michango ya wanafunzi....
 
we unae lalamika mfuko wa cement ulizia MTWARA MFUKO bei gan alafu waulize ni kwa nn
 
Bodi ya mikopo ni tatizo, lakini wenyewe husema serilali ndio hawawapi pesa kwa wakati.Hivyo amri yako ya kwanza ni kuwataka hazina wapeleke pesa kwenye bodi ya mikopo mapema!
 
Si mliambiwa elimu ya bure mkaikataa sasa mtaisoma namba kwa ushabiki wenu
 
Aanze na bodi ya mikopo kufanya nini.?Subiri bajeti ijayo wewe unafikiri hela zinatoka tu kama kumuomba baba yako na kama umekosa mkopo utaisoma namba nenda musoma utalii kasomee mapishi nahitaji mpishi kwangu!
 
Only in TZ,watu hawataki kusoma bure wanataka kukopeshwa.
 
Aanze na bodi ya mikopo kufanya nini.?Subiri bajeti ijayo wewe unafikiri hela zinatoka tu kama kumuomba baba yako na kama umekosa mkopo utaisoma namba nenda musoma utalii kasomee mapishi nahitaji mpishi kwangu!

Hahahahaha JF bhanaa
 
NAAMINI BOARD WATAFANYA KWELI NDANI YA WIKI HII NA CHUO TUTAENDA

Hii ni kutokana na kusogezwa mbele kwa tarehe ya kuripoti kwa baadhi ya vyuo,hivyo hapana shaka watakuwa wametoa mwanya kwa board kukaa na kuachia walivyotuandalia. Ila tu kwa ushauri wangu,serikali isifanye siasa kwenye Elimu maana sisi watoto wa wakulima ndilo kimbilio letu,our actual asylum,na hatuna jijingine jamani,muwe na huruma na sisi watoto wa hali ya chini.
 
Nawasalimu wote wanajukwaa wenzangu kwanza nianze kwa masikitiko makubwa sana kwa jinsi bodi ya mikopo inavvyo tufanyia sisi watoto wa masikini. Chuo nilicho chaguliwa kinafunguliwa kuanzia jumatatu alafu mpaka hivi sasa sijajua hatma yangu kuhusiana na suala la mkopo. Nina andika haya kwa uchungu mkubwa kwa sababu mwaka uliopita niliahirisha kuingia chuo mara baaada ya kukosa mkopo. Kwa mazingira yalivyo hivi sasa naona pia kwa mwaka huu mambo yatakua ni yale yale kwa sababu mpaka sasa sijui ni tatizo gani linalo wafanya bodi ya mikopo wasitoe majina. Nilikua nategemea watanzania wenzangu wange chagua elimu bure hadi chuo kikuu matokeo yake wamechagua elimu bure hadi kidato cha nne. Hivyo sina budi kua na wasi wasi juu ya hatma ya elimu yangu. Shukrani sana nawasilisha
 
Back
Top Bottom