Dr. Lwaitama apewe uenyekiti CHADEMA na kugombea Urais 2020

Mtu akitoa mawazo tofauti na makada wenzake ambao wengi wao ni kasuku hua munaanza kumuamndama. Hapo mnatafuta sbb ya kumvua uanachama.
 
Mtu akitoa mawazo tofauti na makada wenzake ambao wengi wao ni kasuku hua munaanza kumuamndama. Hapo mnatafuta sbb ya kumvua uanachama.
Lazima utaandamwa makamanda hawataki mawazo mbadala.
 
Naunga mkono hoja kuwa Chadema inahitaji mtu mwingine kumkabili Magufuli 2020, ila kwa kwa maoni yangu sio mtu wa type la Lwaitama, kwanza kwa sababu Lwaitama bado sio mwanachama wa Chadema.

Kwa vile tayari tumeishamjua mgombea wa CCM 2020, ni the seating president, ili opposition ilete impact 2020, lazima ilete mgombea ambaye ni Zaidi ya Magufuli, mtu kama Tundu Lissu ambaye ni Zaidi ya Magufuli ndio anaweza kusaidia, kama nilivyoshauri hapa
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

P.
Upo sahihi P.

Lwaitama ni think tank ila bado hajawiva kuwa mgombea.Ni kama Dr Sengondo Mvungi alivyogombea urais kwa tiketi ya NCCR.
 
Igwe wanaJF

Kutokana mambo yalivyo kwa sasa ni wazi Dr. Azavery Lwaitama anafaa kuwa mwenyekiti wa Chadema na apeperushe bendera ya uraisi Chadema mwaka 2020. Kwa hali ilivyo kwa sasa Dr. Lwaitama anafaa kwa vigezo vifuatavyo:

  1. Ni msomi ukilinganisha na makamanda waliopo kwa sasa.Chadema itaepuka mtihani wa ukaguzi wa vyeti na kwa sasa nchi inahitaji wasomi wazuri kama Lwaitama kwani katika mazungumzo yake anaonesha kuwa anaijua dhana ya maendeleo.
  2. Chadema hawahitaji kumsafisha bali watamnadi tu ikumbukwe kwa sasa ni ngumu kumpata mgombea asiye na makando ya ufisadi.
  3. Anatoka kanda ya ziwa.Dr.Lwaitama ni mwenyeji wa kanda ya ziwa.Chadema wanahitaji mtu wa kurudisha ushawishi kanda ya ziwa kama alivyofanikiwa Dr. Slaa.
  4. Atavunja makundi ndani ya chama. Chadema kwa sasa inaugonjwa mkubwa wa ukanda, ukabila, udini, usasa na uzamani. Namuona msomi Dr. Lwaitama akienda kuyatibu.
  5. Ugonjwa wa kuropoka na matusi, pengine Chadema kinashika nambari moja ulimwenguni kwa matusi na kuropoka bila kuwa na akiba ya maneno. Wengi waliowatukana sasa ndio wafalme wao.Hili ni pepo ambalo Dr. Lwaitama anatakiwa kulidhibiti.
  6. Dr. Lwaitama ni "CCM mfu" naam, Chadema inahitaji mtu aliyekulia CCM ili kuwafunda namna ambavyo chama cha siasa kinatakiwa kufanya kazi.Dr.Lwaitama anauwezo wa kutengeneza makada wa chama na sio "makamanda" sina shaka na hili kwani ni mwanafunzi mtiifu wa Mzee Mangula.
Kuna mengi ya kumuelezea Dr. Lwaitama lakini kwa uchache yaliyoorodheshwa ni baadhi ya sifa zake.Nakaribisha michango zaidi japo ninamaliza kwa kusema ili Chadema ipate huduma ya Dr. Lwaitama yapaswa alindwe uhai wake dhidi ya kundi la masultani ambao wao hupambana na yeyote anayeonekana kutaka kutwaa uenyekiti ndani ya Chadema.

Nawasilisha kwa unyenyekevu.
Kwani lumumba wanasemaje
 
Naunga mkono hoja kuwa Chadema inahitaji mtu mwingine kumkabili Magufuli 2020, ila kwa kwa maoni yangu sio mtu wa type la Lwaitama, kwanza kwa sababu Lwaitama bado sio mwanachama wa Chadema.

Kwa vile tayari tumeishamjua mgombea wa CCM 2020, ni the seating president, ili opposition ilete impact 2020, lazima ilete mgombea ambaye ni Zaidi ya Magufuli, mtu kama Tundu Lissu ambaye ni Zaidi ya Magufuli ndio anaweza kusaidia, kama nilivyoshauri hapa
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

P.
Hongera sana Pasco nachekukubali ni kuwa siku zote unapocomment unatoa na evidence
 
Lwaitama sio mwanasiasa ni mpiga makelele hata akiongea hamna proffesionalism anapiga mikele na miyowe hadi mishipa ya shingo inamsimama.Unaona kabisa kuwa anapenda kushinikiza hoja yake ikubalike kwa mikelele .

Pili sio mobilizer yuko tu kama Lowasa ni mtu anayetakiwa kubebwa na chama akiachwa mwenyewe hana uwezo wa kujisimamia mwenyewe kujenga political brand yake

Kuhusu kugombea uenyekiti au uraisi Chadema jibu ni rahisi haiwezekani Lwaitama ni lofa hana hela,Hizo nafasi ni za wenye pesa wanaojua kuzitafuta aelewe kuwa Chadema sio chama cha kijamaa ni cha kibepari hivyo mabepari wenye nazo ndio washika chama na wagombea.Ndio maana hata alipoamua kujiunga na chadema hawakumpapatikia na kumpa publicity kubwa kama akina lowasa,,sumaye,nyalandu na wema sepetu sababu waliona Lwaitama lofa tu ni zigo tu kwa chama.Lwaitama alikosea kujiunga chadema wakati ni lofa
ccm oyeeeeee cuf lipumba oyeeeeee
 
Huyu Mzee namjua tokea akiwa Mwalimu wangu wa somo Fulani chuo kikuu

nakimbuka siku moja mvua ilinyesha Kwa wingi tuko sehem , akavua viatu akakunja suruali akala mdogo mdogo , hahaha

Baadae nkaja kumkuta kagera chuo cha JOCUCo ambako nilienda Kwa shughuli maalumu

Anaweza akawa Rais Ila wa mioyo ya watu kama waliopita,

Ila lwaitama kachoka na mawazo yake nayajua mimi, naungana na Pascal Mayalla

Wafikilien
1. Mbatia
2. Mbowe mwenyewe
3. Zitto kabwe
4. Mnyika
5. Tundu lissu
ccm Ni janga la kitaifa
 
Naunga mkono hoja kuwa Chadema inahitaji mtu mwingine kumkabili Magufuli 2020, ila kwa kwa maoni yangu sio mtu wa type la Lwaitama, kwanza kwa sababu Lwaitama bado sio mwanachama wa Chadema.

Kwa vile tayari tumeishamjua mgombea wa CCM 2020, ni the seating president, ili opposition ilete impact 2020, lazima ilete mgombea ambaye ni Zaidi ya Magufuli, mtu kama Tundu Lissu ambaye ni Zaidi ya Magufuli ndio anaweza kusaidia, kama nilivyoshauri hapa
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

P.
Mtu zaidi ya magufuli ni yule mwenye kumilki bunduki na risasi nyingi, ccm haitaondoka kwa karatasi, muulize keilima upate jibu sahihi
 
Lissu. Ndiye mbabe wa magufuli kisiasa kisheria na kihoja
 
Back
Top Bottom