Dr limbu kweli siasa ni usanii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr limbu kweli siasa ni usanii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ichobela, Mar 24, 2012.

 1. I

  Ichobela JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Dr Limbu,ulipewa unaibu wizara ya maji ukashindwa kuwafikishia maji watu wa jimbo la Magu pamoja na jimbo kuwa kando kando ya ziwa vikitoria,hivi sasa umeanza kuwapiga usanii wananchi kwa ghiriba ya kulalamikia serikali kutowapatia maji wananchi wa jimbo lako!Jamani magamba punguzeni basi kulaghai wananchi.
   
 2. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hivi bado ni mbunge?manake sijamsikia muda mrefu kwenye vyombo vya habari.Nakumbuka aliwahi pia kuwa naibu waziri wa fedha enzi za Mkapa,siyo?
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na bado wananchi watalalamika sana na hakuna atakaye wasikia,kwa nini walimchagua ili hali wakijua alipokuwa Naibu waziri wa maji hakuna lolote alilofanya,akawa Naibu waziri wa Mambo ya ndani yale yale,Naibu waziri wa Fedha hakuna la maana,na Ngongoseke aliwaambia bado wakamchagua Limbu,wakamsusia Ngongoseke aliyejitahidi pale katani kwake akiwa Diwani.Shauri yenu wananchi wa Magu na vijiji vyote pamoja na hiki cha yichobela.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ana damu ya upinzani. Alihaha sana kuutafuta ubunge huyo alianzia CCM akashindwa akaenda NCCR akashindwa akarudi CCM ndio akafanikiwa. Aliingia kwa kotapini atatoka kwa kotapini!
   
 5. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,985
  Likes Received: 20,384
  Trophy Points: 280
  Kinachompatia ushindi huyu dr ni upumbavu wa baadhi ya wana magu na hasa wale wa mjini na kata nyingine ukiondoa kata yake ambayo walimchagua diwani wa upinzani.

  Mijitu ya Magu iko kilometa tisa tu kulifikia ziwa victoria lakini hadi leo inalia shida ya maji na bado inamchagua huyu mbunge ambaye hajaonesha anawakilisha nn!

  Ng'ombe na wali wanaohongwa kule bar ya mlimani ndo vinawagharimu
   
 6. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  sikweli kwamba watu wa magu walimpigia kura huyu mbunge .alishindwa uchaguzi, sema hila za kiccm kumpitisha kupitia riz kikwete na usalam wa taifa ndo waliompitisha.wapiga kura wengi hawakumtaka huyu bwana. ni mtupu sana kichwani na hana jpya zaidi ya ujinga ni mbunge wangu anatoka tarafa yangu , tarafa yake wenyewe walikuwa wanamzomea kila wakati.ndo wabunge wa ccm bana
   
 7. e

  enk Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mzaliwa wa Magu na nakubaliana na maneno yako kuwa mi nio Mpumbavu LAKINI SI MJINGA KAMA WEWE. Chambua na uone Mpumbavu na Mjinga yupiana nafuu. Kuweni na adabu mnapoandika maelezo yenu kutukana hakusaidii kusomeka kwa ujumbe wako bali huonyesha tafasiri halisi ya mtu hasa katika uwezo wa kufikiri. Kwanza we Obe unamjua baba yako alokuzaa!? Kama hujaelezwa basi ni mwana Magu kwa damu (Na kama unabisha kaulize vizuri) So kwa ujinga wako umemtukana Baba yako kuwa ni Mpumbavu. unaiita radhi ya mzazi Usiombe Dunia hii ukakosa radhi ya Mzazi we utahangaika na kulalamika maana mambo yako yatakwa hayaendi kama unavyotaka hadi uombe msamaha na ukubalike. Nakupa pole kwa kukurupuka hadi ukajisahau ukatukana ndugu zako. Kusoma maana yake ni kuondoa ujinga lakini wewe pamoja kupata elimu hiyo walau ujinga haujakutoka POLE SAAAAAAAAANA.
   
 8. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Inaonekana wewe una matatizo ya kumbukumbu. Dr. Festus Limbu hajawahi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, bali alikuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha.
   
 9. U

  Ugweno Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona unajitukana mwenyewe?mjinga akifunzwa anakuwa mwerevu ila mpumbavu daima haelimiki! Duu hii kali kumbe wewe ni mpumbavu na sio mjinga!?!
   
 10. C

  CANCER Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  hakuchaguliwa ila aliiba kura kwa msaada wa jk na alishasema sio mbuge wa mgu mjini ila ni mbunge wa mahaha na nyanhanga walikomchagua
   
 11. I

  Ichobela JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu Ngereja,kabla hajawa naibu wizara ya fedha alikuwa na position gani katika baraza la mawaziri?Mpigie simu Dr. akupe ukweli naona humuelewi vizuri Limbu.Mimi ni mbunge wangu namfuatilia vizuri,kama hujui nikupe kwa kifupi sana.Huyu mheshimiwa alikuta miundo mbinu iliyopigiwa chapuo na kina Mzee Mabawa na Kapunda,pandisha mlima wa Nyashimba utakuta tenki la maji lilojengwa ili watu wa Nyashimba hadi Kinango wapate maji enzi hizo za Jembe na Nyundo.....kakuta miundo mbinu kashindwa kuendeleza kama utahutaji historia nyingine zaidi sema nikueleze yamhusuyo Dr na kupotezea kwake shida za wananchi wake....kama kuna la maana alofanya huyu ndugu yetu tusaidiane ili asilaumiwe bure.....
   
 12. e

  enk Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA UKOMO WA AKILI YAKO UTAONA NA KUJUA NIMEJITUKANA MWENYEWE. Kwa wenye AKILI na ambao si wajinaga kama wewe walishaelewa. INASIKITISHA KIJANA KAMA WEWE UNAJIANIKA HADHARANI KUONYESHA UMBUMBU WAKO ndo shida ya kutosikiliza maelekezo ya Wazazi na kukalia kusikiliza mambo ya vijiweni zaidi ambako mijadala mingi huongozwa na watumiaji wa JANI na wanachokiongea nia maoni yao + JANI = UJINGA. Falsafa ni nyingi shirikisha ubongo wako kikamilifu na usipoelewa uliza uelekezwe ELIMU NI BAHARI.
   
 13. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Unabisha kwa kitu ambacho kiko wazi. Dr. Limbu amekuwa Mbunge kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2000. Katika baraza la kwanza la mawaziri baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 hakuwemo, baada ya mabadiliko madogo mwaka 2002 ndipo akateuliwa kuwa naibu waziri wa katika wizara ya Fedha, Waziri akiwa Bazir Mramba. Hakuwahi kuwa waziri wala naibu waziri kabla ya 2002. Kwenye uchaguzi wa 2005 na 2010 kipindi cha uongozi wa Kiwete hakuwahi kuchaguliwa kuwa naibu waziri wala waziri.

  Wadhifa alio nao Dr. Limbu ukiacha ubunge ni Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba hadi sasa.

  Inaonekana humjui Mbunge wako, pamoja na kujitapa kuwa ni Mbunge wako na unamwelewa. Kama wewe unabisha, na kwa kuwa unajitapa kuwa unamjua sana Dr. Limbu, na historia yake ya kisiasa, weka hapa nyadhifa za uwaziri/naibu waziri alizowahi kushika tangu awe mbunge. Weka mwaka, na wizara alizoshikilia.
   
 14. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umenena kweli mkuu huyo jamaa ni bonge la kilaza maa hata nikiwa nimeenda ukweni pale magu huwa kuna shida kubwa ya maji na wakat huohuo ukitoka nje ukaangalia upande wa kas magharibi unaliona ziwa victoria limejaa kama peshe la mchele.Chadema ongezeni kasi jimbo la magu kwani limbu ameshajichokea zaamani!Magamba bana!
   
 15. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  dogo acha matusi rejea sheria za jf
   
 16. e

  enk Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We umeona matusi!? Rejea ilikoanzia hii mwenzio katukana watu wote wa Magu kwa ktwaita WAPUMBAVU bila kujali mbaya zaidi bila kujua kuwa original ya baba yake mzazi ni Magu. Hivyo sijamtusi bali nilikuwa namkumbusha awe kwenye mstari, hivyo nakuomba mi na wewe tusaidiane kumkumbusha hizo sheria za JF. Tchao
   
 17. mku

  mku Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nyie wasukuma wa ng'ung'umalwa kuna nini mbona mnatukanana hapa? we enk una uhakika gani kuwa JERO hakuwahi kumsikiliza baba yake?
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lile tanki la Maji limejengwa miaka ya 60's baada ya uhuru ili kuwapatia maji wana Magu waliokuwa si zaidi ya elfu hamsini,kwa sasa mji umekua na population imeongezeka lakini huyu Bwana halitambui hilo pamoja na uDAKTARI WAKE, ni mjinga wa mwisho.Alichokifanya cha maana ni alipokuwa Naibu Waziri wa mambo ya ndani alipowapatia vijana ajira ya upolisi chini ya IGP yule mzawa wa masanza Marehemu Michael Mgema kama sijakosea jina.
   
 19. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni mwaka gani Dr. Limbu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya ndani? Kumbukumbu hazionyeshi hivyo. Tuambie ni mwaka upi? maana kumbukumbu zote za mawaziri kwa kila kipindi zipo. Mimi nasema Kabla ya 2002 hakuwahi kuwa na wadhifa wowote wa uwaziri/naibu waziri, na baada ya 2005 hakuchaguliwa kwenye cabinet hadi sasa. Nafasi ya naibu waziri aliyoishikilia ni Naibu waziri wa Fedha mwaka 2002 hadi 2005. Mwenye ushahisi zaidi auweke hapa.
   
 20. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,985
  Likes Received: 20,384
  Trophy Points: 280
  Ngereja! Ni kweli Dr Limbu hajawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, lakini, tafuta kumbukumbu zako za mwaka 2002 uone nani alikuwa waziri wa maji na nani alikuwa naibu wake, hapo ndo utakuja ukanushe kuwa Limbu hajwahi kuwa naibu waziri wa maji chini ya ENL.
  ENK, heshima mbele, inaonekana hujui nini kinajadiliwa hapa, na hili linaweza kuwa si kosa lako, masuala ya mm kumjua au kutomjua baba yangu yanahusiana nini na upumbavu wetu wana Magu!

  Unaweza kuwa na uhuru wa kuandika hapa lakini si haki yako ya kutaka kujifanya mtaalamu wa DNA, binafsi nimekuchukulia kama binadamu mwenye haki zote lakini anafaa kupuuzwa, nimepuuzia yote uliyoandika kwani lengo hapa la mdau Ichobela (Ilungu, Nyanshimba-Yichobela- Kinango haha haha) lilikuwa ni kuonesha namna gani huyu jamaa tangu amekuwa mbunge ahajafanya lolote la maana si kwa watu wa Magu mjini pekee bali hata kwa walio pembezoni, mwalinha, sagani etc. Kikubwa hapa, kama wewe ni mkazi wa Magu na unadhani kumtetea limbu ni kutoona alichofanya, pole.

  Tuone labda sasa kwa kuanzishwa huu mkoa wa Simiyu na kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo wa magu, kunaweza kuwepo na mabadiliko, tusubiri tuone
   
Loading...