Ngereja! Ni kweli Dr Limbu hajawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani, lakini, tafuta kumbukumbu zako za mwaka 2002 uone nani alikuwa waziri wa maji na nani alikuwa naibu wake, hapo ndo utakuja ukanushe kuwa Limbu hajwahi kuwa naibu waziri wa maji chini ya ENL.
ENK, heshima mbele, inaonekana hujui nini kinajadiliwa hapa, na hili linaweza kuwa si kosa lako, masuala ya mm kumjua au kutomjua baba yangu yanahusiana nini na upumbavu wetu wana Magu!
Unaweza kuwa na uhuru wa kuandika hapa lakini si haki yako ya kutaka kujifanya mtaalamu wa DNA, binafsi nimekuchukulia kama binadamu mwenye haki zote lakini anafaa kupuuzwa, nimepuuzia yote uliyoandika kwani lengo hapa la mdau Ichobela (Ilungu, Nyanshimba-Yichobela- Kinango haha haha) lilikuwa ni kuonesha namna gani huyu jamaa tangu amekuwa mbunge ahajafanya lolote la maana si kwa watu wa Magu mjini pekee bali hata kwa walio pembezoni, mwalinha, sagani etc. Kikubwa hapa, kama wewe ni mkazi wa Magu na unadhani kumtetea limbu ni kutoona alichofanya, pole.
Tuone labda sasa kwa kuanzishwa huu mkoa wa Simiyu na kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo wa magu, kunaweza kuwepo na mabadiliko, tusubiri tuone