Dr Levy: Ali Kiba ni dozi ya kutwa mara tatu

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,183
Ukimfunika kukata mauno atakushinda kutunga. Ukimfunika umaarufu atakutesa kwa sauti. Ukimsumbua kuhonga media yeye atakuumiza kwa kutojisumbua na hizo media. Ni kama kumpenda mwanamke ambaye hajui kama unampenda.Na mbaya zaidi hata hisia juu yako hana. Utaumia sana.

NdIo Ali. Hata mashabiki wake wanampenda kuliko yeye anavyowapenda. Anachofanya ni kuwapa kile alichopewa na Mungu. Sauti. Watu wanadata naye.

Wakati watu wengi sana wakimsifia kwa sauti ambayo anayo yeye tu ktk dunia hii. Kuna kitu wanakisahau. Ana tofauti sana katika tungo zake.

Sikiliza Mapenzi yana Run Dunia. Anamuimbia mapenzi mwanaume mwenzake. Ngumu sana mwenye akili ya kisoda kuelewa ule wimbo. Mchizi anamuimbia mchizi wake ngoma la mapenzi afu lina bamba mbaya. Hata R. Kelly na wenzake akili hii waliikosa.

Dem kaenda kwa Ali kumshitakia ujinga wa bwanaake. Of coz watoto wa kike wanapenda faraja. Ali akampa faraja.

Mchizi kugundua kaamua kumtosa mtoto. Mtoto kaamua kutangulia mbele ya haki. Alimpenda mchizi wake ila Ali alimpa faraja tu baada ya ushauri. Hata mimi ningemfariji kwa namna hiyo mtoto mzuri.

Kasikilize hilo ngoma ukiwa na akili timamu usichanganye na mawazo ya hali ya Wema Sepetu kwa sasa. Hutaelewa alichoandika Ali.

Kiba siyo wa nchi hii

Kinachofanywa na computer yeye anakitoa kwenye koromeo lake.
Kuna sauti kutoka kooni kwake ni ya pekee kuliko upekee wenyewe.Hawezi kusema ila Diamond na wenzake hicho kitu kinawaumiza sana.

Ali hajui kujitangaza. Ndo maana hata gari anayotumia haijulikani.
Ali hajui kiki. Ndo maana huwezi kumsikia akiongelea issue zake na madem zake. Hajui kujiongeza ndo maana husikii ana nyumba au shilingi ngapi kwenye account zake za bank.

Na ni ngumu kumkuta news room za udaku. Vyote hivyo hana lakini bado anawaumiza kichwa kundi kubwa la watu.

Katikati ya magwiji wa hizi kazi.

Fella,Tale na wenzao.Sallam muweke kando hajui fitna za game hili.
Pamoja na lundo la hao watu Alibbado anasimama nao katika mstari mmoja.
Ogopa sana.


Heshimu.

Hana anachowaweza zaidi ya lile koo lake na akili ya kuandika kinachotakiwa kuandikwa.
Hapa siyo suala la team flan.Ukweli uko wazi kuwa kuna upinzani wa wazi na wa siri kati ya Kiba peke yake na Diamond na watu wake. Huwezi kusikia management ya Ali ikimuongelea Diamond.Ila ni rahisi zaidi kusikia management ya Diamond ikiongea jambo la Kiba.
Ndo ukweli.

Watu wanaomzunguka Diamond huwezi kushindana nao hata kwa nusu saa.Game la muziki liko vyumbani mwao.Linawatii kuliko askari wa Dar mbele ya Makonda.Lakini Ali kaendelea kuwepo kwenye kilele bila kutumia nguvu.Alichonacho Ali kwenye koo angekuwa nacho Diamond dunia ingesimama.

Ni kama Ronaldo angekuwa na kile alichonacho Messi katika miguu yake.

Mashabiki wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na Diamond mitandaoni,wakati Kiba anawauliza wadogo zake vilipo viatu vyake vya michezo akacheze football bondeni pale Jangwani.

Diamond anajituma sana na muziki wake.Ali anatufanya tuamini kuwa muziki ni burudani na ufanywe kiburudani.
Wakati soko la muziki likilazimishwa liwe na muziki unaochezeka.Ali alikuja na ngoma kama Mac Muga ambao hauchezeki na siyo wa mapenzi na alikuja na ngoma ya Mwana ambayo sio wa mapenzi wala sio club bagger.ukakamata vibaya sana.
Kasikilize Karim.

Utagundua kuwa Kiba ni zaidi ya biti na promo.

Imeandikwa na mkongwe Dr.Levy Baba ubaya
 
mzaramo yote ulo andika kama usingetaja jina la Diamondi ningekuona wa maana sana, lakini kutokana na ulivyo andika ni ushabiki tu mapenzi niue, ukimpenda mtu mwenye chongo waweza chukua siku mzima kumsifia, utasema lile sio chongo ni mbwembwe tu, mara yale ni manjonjo tu, sasa unaanza kusema lakini yeye ni bora kuliko fulani mwenye kengeza, mapenzi ni mapenzi bwana, na ukae kujua kila mtu kaumbwa na udongo wake, alicho nacho kiba diamond hana na alicho nacho diamond Kiba hana, Kuna vitu katika musiki Kiba hata afanye nini hawezi mfikia Mondi na Mondi nae vilevile kuna vitu hawezi mfikia Kiba.

Cha muhimu ukiwa shabiki au mpenzi wa Kiba, achana na mambo ya Mondi, na ukiwa shabiki au mpenzi wa mondi achana na mambo ya Kiba.
 
Aise tuzo 16 za kimataifa nikizifahamu naanza kumuunga mkono
Niliwahi argue na mtu kuhusu awards za east africa tv, yeye huyo bwana alikuwa anasema zile award ni za kimataifa kwamaana tv ni ya east africa, mi nikamwambia east africa jina tu, Kenya wala uganda hakuna mwenye kuijua hiyo Tv labda wabongo waishio huko, sasa Rwanda , Burundi na Sudani ndo kabsaaaa. Kwa Tanznaia hii yenyewe ni Tv ya kidarisalama zaidi, hata ukiangalia washiriki na washindi na category zenyewe zilikuwa za kidarisalamu tu.
 
Back
Top Bottom