Dr.kitine yanaweza kumpata yaliompata kolimba?

Dr.kitine yanaweza kumpata yaliompata kolimba?

mkute

Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
80
Reaction score
12
Wimbi la mparanganyiko wa ccm linazidi kushika kasi kila kukicha,baada ya mtoto wa mkulima kuwataka viongozi wastaafu kutumia vikao kueleza mawazo yao.Agizo hilo limepuuziwa baada ya mmoja wa viongozi wastaafu Dr Hans Kitine kukiponda wazi wazi chama hicho.Akiongea ktk kipindi kinachorushwa na Channel ten cha Je tutafika? Kitine amesema kuwa ccm IMEPOTEZA MWELEKEO maneno yaliowahi kumgharimu aliewahi kuwa katibu mkuu wa ccm wakati huo marehemu Horace Kolimba.Swali langu kwa great thinkers je Dr kitine atasalimika kweli kwa hiyo kauli? maana ukweli unauma!
 
Kwani uongo? Au kosa ni neno limesemwa na nan.ni kwel tena tunasisitza,imepoteza mwelekeo na dira.haina haiba tena kwa wananch.
 
dr. kitine hawamuwezi huyu ndo alikuwa boss wa TISS hawa akina othman kawatrain yeye kitu nzito huyu
 
Ukweli mchungu lakin ni tiba, kwanii hata mgema si huwa anakwea mnazi mwenyewe au wanafiri huwa ana msubiria jirani, "hawana lolote na tena wao si chochote wajipangee..."
 
Wakimuua sisi mashahidi, hawatakuwa na pa kutokea!
Alichoongea ni ukweli, na ndicho tunachosisitiza kila siku hapa JF, na tunaongea mchan a kweupe, mbona hawatuuwi sisi?
 
Wakimuua sisi mashahidi, hawatakuwa na pa kutokea!
Alichoongea ni ukweli, na ndicho tunachosisitiza kila siku hapa JF, na tunaongea mchan a kweupe, mbona hawatuuwi sisi?
kaka unataka wakuue?
 
CCM.... bado mwingine ... Who's next Mkapa, Mwinyi, Malecela or ...
 
Kwa kifupi huyu jamaa alikuwa bosi wa mtoto wa mkulima enzi hizo na kwakuwa ile shughuli hakuna kustaafu basi bado ni bosi wake mpaka leo!!! :smash:
 
Kama kawiva alishindwa vipi kucoverup scandal yake hadi wakamlipua mnasifia mijitu kishabiki.ama mlikua bado kindergaten hamjui alifanyaga nini
 
nilimwangalia nikapata picha moja; NI MZALENDO WA KWELI NA MWENYE UCHUNGU NA MWELEKEO, SI WA CHAMA TU, BALI NA NCHI
 
Dr. Kitine atasalimika sana sio kwa sababu hawamuwezi, bali kwa sababu yeye tayari ni spent force, not dependable, doesn't matter any more, only barking dog, seldom bite na ukizingatia kwa umri wake hata hayo meno ya ku bite hana!.

Kina Kaduma wamesema, Warioba amesema, Butiku amesema, Salim Amesema, Kisumo amesema, Lowassa amesema, Sumaye naye kasema, nani amesikia?. No body anasikiliza sauti za spent force, CCM inasikiliza sauti za vijana, energetic na dependable kuchukua nchi!.
 
nakumbuka alivyotumbukiza benzi baharini ili kufuta ushahidi.........walahi kitine ni mwamba....hawamuwezi huyu mzee hata kidogo.....ngumu sana..
 
Na Jenerali Imran Kombe alikuwa nani?

nae alikuwa huko tiss....na alikuwa boss na walimpoteza kwa kuwakandamiza wale wa chini na kuunda makundi yasiyo na mpango....alinyanyasa sana watu yule jamaa...then wakasema isiwe tabu ukasukwa mpango kabambe then akapotezwa...
 
Wakimuua sisi mashahidi, hawatakuwa na pa kutokea!
Alichoongea ni ukweli, na ndicho tunachosisitiza kila siku hapa JF, na tunaongea mchan a kweupe, mbona hawatuuwi sisi?

Mh! I doubt this, what about, Stan Katabalo, Gilman Rutihinda, Steven Kibona, Horace Kolimba, Imrani Kombe, Edward Sokoine, Koplo Rashid Lema e.t.c.
 
tusifikirie kuhusu mambo ya kuwawa kwani si rahisi kitine auwawe kwani kama ingekuwa rahisi basi wangemmua mchungaji munishi aliyetumia GTV wakati wa uchaguzi kuwashambulia ccm hadharani mmoja kwa moja bila kuficha chochote pamoja na kumwandama kila mahali ila ss watanzania tulituma maoni kwa munishi kuwa yeye asiogopekwani kama watammua basi watanzania watakuwa mashahidi kuwa ccm ndio wanaohusika
 
nae alikuwa huko tiss....na alikuwa boss na walimpoteza kwa kuwakandamiza wale wa chini na kuunda makundi yasiyo na mpango....alinyanyasa sana watu yule jamaa...then wakasema isiwe tabu ukasukwa mpango kabambe then akapotezwa...

lakini alikuwa ameshastaafu tayari, kwa hiyo revenge? how is revenge justified? ''freewheeling justice''!?
 
Wimbi la mparanganyiko wa ccm linazidi kushika kasi kila kukicha,baada ya mtoto wa mkulima kuwataka viongozi wastaafu kutumia vikao kueleza mawazo yao.Agizo hilo limepuuziwa baada ya mmoja wa viongozi wastaafu Dr Hans Kitine kukiponda wazi wazi chama hicho.Akiongea ktk kipindi kinachorushwa na Channel ten cha Je tutafika? Kitine amesema kuwa ccm IMEPOTEZA MWELEKEO maneno yaliowahi kumgharimu aliewahi kuwa katibu mkuu wa ccm wakati huo marehemu Horace Kolimba.Swali langu kwa great thinkers je Dr kitine atasalimika kweli kwa hiyo kauli? maana ukweli unauma!

mawazo ya ama kupandikiza uwoga na vitisho kwa wengine.kuwafumba midomo wasiseme ati kwa kisingizio cha 'yatawakuta ya kolimba'. kila nafsi itaonja mauti...wanaotisha wenzao na wanaotishia wenzao.

kila mtu na aseme bila woga. kwani wanaokwenda kwa babu na wasiokwenda wote watakufa.

tujadili vifo vyetu. tusijadili vifo vya wengine kana kwamba sisi tutasalimika na mauti.
 
Back
Top Bottom