MAkosa yake ya zamani hayawezi kufutika.
Ila ni wazi kila mtu ana makosa yake. Mtu msafi ni mtoto mdogo ambaye hataweza kazi yoyote, wote sie hapa tuna historia fulani.
Anyway, aliosema ni mazito sana, anaonekana yuko frustrated sana, na alikuwa kama ndio kapata mahali pa kutolea upepo. God bless Makwaiya.
LAkini kwa umbeya tu pamoja na mambo mazito sana aliosema, kama mie ningekuwa CCM, lazima ningekuwa na kalamu na karatasi natake note kwa ajili ya utekelezaji.
Kiukweli baba na babu zetu walifanya kazi kubwa bila ubinafsi kujenga nchi na kutusomesha kwa kodi na majasho yao, hawakulimbikizia (wengi waliokuwa kwenye madaraka) hio ilikuwa faraja na chanzo cha mshikamano.
Kumuogopa kiongozi kulitokana na majukumu, na sio mapesa alionayo kinyume na sasa.
vikao vilikuwa vya kujadili utekelezaji wa mipango, sasa mhhhh!!!
mkundi yalikuwa ya kimtazamo wa uelekeo wa nchi,
Lakini jamani naomba kumjua huyo katibu mkuu aliesemwa kuwa anajulikana kuwa ni mwizi