Dr. Kitila ampa tabu Thabo Mbeki

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dr. Kitila Mkumbo jana alimpa wakati mgumu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.

Hiyo ilikuwa ni katika wakati wa maswali kwa Mbeki baada ya hotuba yake katika ukumbi wa Nkrumah wa UDSM.

Swali la Dr. Kitila lilijikita katika kauli ya Mbeki, wakati akiwa madarakani, kuwa UKIMWI hauenezwi na ngono ila shida na umaskini wa wananchi. Dr. Kitila alimkumbusha Mbeki juu ya kifo cha mtoto wake (wa Mbeki) kilichosababishwa na UKIMWI. 'Unaendelea kusimamia kauli yako?' aliuliza Dr.Kitila

Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki. Na hapo ndipo ukawa mwisho wa maswali kwa Mbeki ingawa swali la Dr.Kitila lilikuwa la pili tu.Prof. Mukandala alimaliza muda wa maswali ghafla

Post Update - Kitila's question:

 
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
kitila alipaswa kujua kwamba Mbeki alivyosema ukimwi ni ugonjwa wa maskini alisema kwa muktadha gani.kwa mfano; wakati mtu anakemea uzembe wa madereva, anaweza kusema "ajali barabarani husababihwa na uzembe wa madereva" sasa hapa haina maana kwamba ni kila ajali itakayotokea itakuwa ni usembe wa dereva lakini kulingana na mazingira ya kauli;kauli inakuwa ni sahihi.Sasa mbeki alipo sema vile. alitaka kuonyesha kwamba umaskini una mchango mkubwa katika kuenea kwa ukimwi;kitu ambacho kina ukweli.
 
Naona huyo muuliza swali aliuliza tu kujionesha kwamba anafuatilia sana mambo ya Mbeki hakuwa na nia yeyote ya kupata clarification kwa faida ya wote.
Lazima utakuwa na matatizo ya uelewa. Msimamo wake ni hatari sana.
 
Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.
 

Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?

*Kama Mkumbo ameuliza kweli suala kwa namna hiyo, ninaelewa kwa nini Mbeki amekataa kulijibu, kwa sababu limekaa kusuta zaidi ya kutaka ufafanuzi........Ila sidhani kuwa Mkumbo ameuliza suala hilo, hivyo lilivyo
 
kitila hapo kweli alikosa busara na alihuliza swali kama sifa flani hivi aonekane nae kahuliza swali ,pia hakukuwa na haja ya yeye kumtaja mtoto wa mbeki kwani ni masuala ya kifamilia...hekiama hana akili finyu huo udokta kapewa kwa njia za panya yaelekea....mgeni akija kwake anaweza kumuhuliza vitu kama hivyo?
 
Kila mtu ana fikra zake juu ya jambo fulani. Sidhani kama Dr. Kitila alikuwa sahihi sana kuuliza hilo swali. Siyo kila kinachosemwa na mwanadamu basi kitakuwa kama anavyodhani au kufikiri. Hata katika sayansi, kuja assumptions nyingi tgu zinatumika!
 
Botswana ni nchi maskini? mbona ukimwi umeshamiri? Wacha kumshabikia Mbeki.

Sababu ya kushamiri ulimwi Botswana ni wafanyakazi wa kwenye migodi hawakupewa elimu ya kutosha na mila na desturi zao zilichangia sana

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kama kiongozi wa nchi ni lazima mtu kama huyo awe na uwezo wa kutoa maelezo yaliyojitosheleza kuondoa sintofahamu kama iliyomkuta Dk Nkumbo
 

Kama Mbeki wakati akitoa statement hiyo hakutoa exceptions, Kitila alikuwa sawa! Kama kiongozi mkuu wa nchi anatakiwa awe makini sana na matamshi yake, siyo kama yale ya watoto wa shule wanapata mimba kwa sababu ya kihelehele chao! Si kweli kwamba watoto wote wanaopata mimba ni kihelehele chao, ndo maana mtoto wa Mbeki akafariki sababu ya ukimwi, Mbeki ana dhiki na umasikini?
 

Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?
 

waambie hawa jamaa wanakuwa wabishi utafikiri nini sijui
 
Mbeki alisema dr kitla alikuwa na wrong information hasa kuhusiana na takwimu alizo zitoa kuwa mtizamo wa mbeki kuhusu ukimwi umesababisha watu wengi kupoteza maisha.Kwa ujumla swali la dakt lilionekana kutowaridhisha wengi na zaidi ya hapo lilihuzunisha wengi na ilionekana watu wapo upande wa mbeki kwa kuonyesha waziwazi kwamba hilo swali ni mwiba kwa mbeki.Licha ya kukataa kulijibu lakn alitoa ufafanuzi nini alikusudia alipotoa kauli hiyo
 
Mtoto gani wa Mbeki aliyekufa kwa UKIMWI?



"Mbeki aliacha kujibu hilo swali. 'I will not respond to that pinching question' alisema Mbeki."

Mbeki knows the answer. Issue yangu hapa ni kuwa viongozi wengi wamekuwa wakitoa kauli ambazo impact yake ni mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…