Dr.Kimei:VAT itakatwa kama ilivyopitishwa na Bunge

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,106
114,714
Akihojiwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar,Mkuu wa CRDB Dr.Kimea amesisitiza kuwa wao wanakata VAT kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya 2016!Katika mahojiano hayo Dr.Kimei ameweka ngumu kuwa wanatekeleza kilichopitishwa na bunge na si vingine.Aidha ameeleza kuwa tozo itaendelea mpaka pale sheria itakavyosema vinginevyo.Kodi hiyo itakuwa kama walivyotoa katika matangazo yao.Chanzo:Channel 10 Taarifa ya Habari Saa 1
 
Yuko sahihi kabisa.

Hili swala sasa linaweza kutinga Mahakamu Kuu Kitengo cha Biashara.Na hili likitokea,itabidi tozo hii isitishwe mpaka kesi ya msingi iishe(sijui watafungua Escrow account mimi sijui) na benki ikishinda kesi basi serikali itabidi itafute namna nyingine ya kufidia hii kodi.

Tusubiri kanuni zitungwe makato yaanze alafu tutaona hii issue inaiishaje.

Muda utaongea.
 
Akihojiwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar,Mkuu wa CRDB Dr.Kimea amesisitiza kuwa wao wanakata VAT kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya 2016!Katika mahojiano hayo Dr.Kimei ameweka ngumu kuwa wanatekeleza kilichopitishwa na bunge na si vingine.Aidha ameeleza kuwa tozo itaendelea mpaka pale sheria itakavyosema vinginevyo.Kodi hiyo itakuwa kama walivyotoa katika matangazo yao
Sasa ni kama ilivyo pitishwa na bunge kupitia mabadiliko ya sheria au kama sheria ya fedha inavyo sema?

Mbona kama unataka kulazimisha kimei kuwa amesema unachopenda?
 
Inashangaza kuona mambo ya kisheria watu wanaleta porojo za kisiasa
 
Hapo sasa
ImageUploadedByJamiiForums1467915441.800321.jpg
 
Battle lines are being drawn!
Kama TRA waliboronga waanzishe mchakato wa kurekebisha sheria hiyo na kukubali wamekosea.
 
Ina maana hawa wawakilishi waliopitisha hiyo bajeti waliielewa kweli au waliburuzwa tu kit kutekeleza ile sera ya hapa kazi tu? Mungu atusaidie sana
 
Sheria ya fedha ilipitishwa na bunge na haijabatilishwa bado. Kimei yupo sawa usipende kusikia unapenda kusikia
 
Sasa ni kama ilivyo pitishwa na bunge kupitia mabadiliko ya sheria au kama sheria ya fedha inavyo sema?

Mbona kama unataka kulazimisha kimei kuwa amesema unachopenda?
eti huyu ni lawyer,lawyer uchwara!kuna ambacho hakijapishwa na bunge?
 
Nyumbu kama kawaida yao wanakimbilia kupotosha habari.

Ukweli ni kwamba Dr Kimei amekubalina na hoja ya Kidata na serikali kwa ujumla.
 
VAT kwa huduma za utalii ni sawa ila sio kwa huduma za benki. tena kamishna alisisitizia makampuni ya utalii yatoze. hahaha! wapiga kura wameguswa, watawala wanaogopa kukosa. #MwendokasiUchwara noma!
 
Akihojiwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar,Mkuu wa CRDB Dr.Kimea amesisitiza kuwa wao wanakata VAT kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya 2016!Katika mahojiano hayo Dr.Kimei ameweka ngumu kuwa wanatekeleza kilichopitishwa na bunge na si vingine.Aidha ameeleza kuwa tozo itaendelea mpaka pale sheria itakavyosema vinginevyo.Kodi hiyo itakuwa kama walivyotoa katika matangazo yao
Usipotoshe hajasema hivyo!
 
Nyumbu kama kawaida yao wanakimbilia kupotosha habari.

Ukweli ni kwamba Dr Kimei amekubalina na hoja ya Kidata na serikali kwa ujumla.

tuseme ni hivyo, sawa! watakachofanya ni kuongeza gharama za huduma kufidia. na hutatambua ni wapi watakugusa! hahahaha!! raha sana
 
Back
Top Bottom