Dr. Kigwangallah unapotea, tafuta staili nyingine

Dr. Kigwangallah unapotea, tafuta staili nyingine

Watanzania wanataka maendeleo ila hawapo tayari kuendelea. Watanzania ni watu wa sababu sababu kila siku kwenye kila kitu

Mtz ukimpa Kazi ndani ya week atafiwa na ndugu zake wote hadi majirani ili asije kazini. Sahizi mnaongeza na kadhia ya usafiri ili msifike au mchelewe kazini. FYI kuna watu sio mawaziri au wakurugenzi ila wanafika kazini on time.

Ukiomba Kazi na kukubali masharti ya Kazi kuchelewa kazini sababu ya foleni sio sababu otherwise acha Kazi vijana waingie. Acheni uvivu na sababu zisizo za msingi

Huwa nasema Kazi anayofanya mkenya mmoja inahitaji watz watatu au wazimbabwe saba
 
Mbona mnamlaumu sana huyu waziri? Tatizo hasa ni nini?
 
Mtoa mada umetoa maoni yako nasi tunayaheshimu, ila ulipogusia sheria za kazi nikahisi unaenda kutueleza ni vipengele gani Dr Kigwa kakiuka bahati mbaya sana na wewe huzijui sheria za kazi, kwani sheria za kazi zinabadilika zenyewe tu bila kufanyiwa amendments? Dr. Kigwa unahisi anayo mamlaka ya kuzibadilisha sheria za kazi peke yake anavyotaka? Nimekusifu sana ulivyozungumzia BUSARA kutumika na sio sio nguvu nyingi, Dr. Kigwa alikosa busara kidogo tu(approach haikuwa nzuri). Pia ulishajenga negative attitude kwa Dr. tayar kwani unazungumzia uwezo wa kufikiri wa Dr. ukimjulisha na chama chake chote
 
Kinachofanya hawa mawaziri wafanye hayo maziara yao ya kushtukiza ni Kutafuta Kick kwenye jamii ili waonekane wanafanya kazi, wale wavivu wa kufukiri huishia kushangilia hovyo bila kutafakari kwa kina kwa nini wafanyakazi wanachelewa!
*Naunga mkonyo hoja yako mkuu*
 
Aisee!
Assumption ni watumishi wote wapo dar au?
Sijaskia watoto wa shule wakibadilishiwa muda wa kufika shuleni.
Changamoto zipo lakini kumbukeni kuna watumishi mikoani wapo kwenye mazingira magumu zaidi na wanajitolea kwa moyo kuhudumia wananchi.
Hoja ya kuboresha mazingira ya kazi ina mashiko na inatakiwa izungumziwe kwa uzito wa pekee sio kama ya kutetea kutowajibika

Umenena vema,mazingira ya kazi yaboreshwe
 
Mtoa mada nakubaliana na wewe kuwa busara iliyotumika ni duni sana na ni kiashilia cha nidhamu ya woga ya kutaka kujionyesha unafanya kaxi! Mambo kama haya yanajibu swali kwa nini JPM alipata shida na kuchelewa kutangaza baraza lake la mawaziri maana pamoja na chama chake Kuwa Na
wabunge wengu lkn si watu WA kutegemea kabisa! wengi ni vuvuzela tu
 
Wewe ndio hujui kwamba sheria hata kama imepitwa na wakati kama haijafutwa inaendelea kutumika kama ilivyo! Pili wewe unadhani Dr kigwangala ana uelewa mdogo angeweza kuwa dactari, mbunge na hatimae kuwa Waziri? Acheni hizo na kwa maelezo yako inaonesha huji kuwa Waziri ni overall in charge wa wizara yake kifupi ni kwamba ndio msimamizi wa kuona sera za chama chake zinatekelezwa na watumishi wa umma ndani ya wizara husika.

Duh hatari sana HIVI KUWA WAZIRI NDIO KUJUA KILA KITU AU KUWA NA UELEWA MKUBWA? UNACHEKESHA NDUGU, ILA C KOSA LAKO PENGINE NI MFUMO WA KUTETEANA
 
Mkuu umenena.Ingawa kuna pumba zinatiririka humu ila nime ku ''appreciate' umetoa mtazamo mzuri ingawa ndani ya hilo loop pia kuna watu wanalitumia kwa uzembe wa makusudi kabisa.Mie nakumbuka nikiwa mdogo hata staff busses zilikuwa kibao kwa taasisi nyingi za serikali achana na nyumba ambazo zimeuzwa kwa taratibu zao waheshimiwa .Leo hii taasisi ni chache sana zenye staff buses.Hata uwepo wa staff buses kwa kiasi fulani unapunguza kero za barabarani kwa watumishi pia.
 
Mtoa mada kamwe sikubaliani nawe. Najua kuna changamoto nyingi na kubwa ya nyumba na makazi kwa watumishi wa serikali. Sawa. Lakini ndiyo waachwe tu wafike kazini muda wanaotaka wao? Anayeshindwa kutimiza wajibu wake kwa wakati uliyopangwa na anaona kwa changamoto zilizopo kamwe hawezi kumudu kukabiliana nazo na akawahi kazini aache kazi. Narudia tena aache kazi.
 
Ushauri wa bure kwa Dr. Kigwangala na mawaziri wapya wa JPM, utendaji kazi wenu ujielekeze zaidi kwenye;
1) Kupunguza/Kuziondoa kabisa kero za wananchi hasa wa kipato cha chini, kama Rais JPM alivyokwishajipambanua
2) Kupunguza/Kuondoa kabisa ubadhirifu, matumizi mabaya na yasiyo ya lazima ya mali na fedha za umma
3) Kuboresha utendaji kazi, kuongeza ufanisi eneo la kazi na kuongeza mapato kwa taifa.
4) Kubuni/kuweka mikakati ya jinsi ya kufikia nambari 1, 2 na 3 kuboresha hali ya maisha ya watanzania.

NA ISIWE
1) Kujikweza na kujijengea umaarufu kupitia vyombo vya habari
2) Kuwatisha au kuwajengea hofu wananchi waogope badala ya ninyi kuwa kimbilio lao kuja kwenu
3) Kugeuka kuwa kero kwa wananchi

Mswali:
Je ziara za kushtukiza kwa Tabibu J J Mwaka imetatua karo gani? na imefikia kwa kiasi gani vigezo vya hapo juu?
Je, zoezi la kuwahi ofisini na kufungia wafanyakazi nje ya geti limetatuta kero gani za wananchi?
Je, kwanini kila ziara za 'kushtukiza' kunakuwepo waandishi wa habari? Wao wanajuaje kwamba kutakuwepo na ziara?




Maswali:
Je zi
 
Hivi mbona Private Companies watu wanafika saa mbili kamili au moja na nusu ofisini na jioni wanatoka saa 11?

Government wanatakiwa wawahi pia, na ofisi zao nyingi wanatoka saa 9 na nusu au saa 10 na nusu.

Cha muhimu tu ni kwamba serikali iboreshe mishahara ya wafanyakazi wao ili waendane na soko la private companies (ukichukulia pia kwamba safari za nje zimepunguzwa), ifikie sehemu mtu awe anaweza ku-move kutoka serikalini kwenda private na vice versa kutegemeana na ufanisi wa mhusika.

Maana ilishazoeleka kwamba mtu aliyeko serikalini hawezi kuendana na kasi ya private companies, hili lifutike watu tufanye kazi na tulipwe accordingly.
 
ivi inaruhusiwa mtu kulala ofisini? maana isiwe taabu kuliko kuikosa kazi bora nijillalie zangu mzigoni!
 
Jmn Kwanza Mi Naomba Kuuliza, Maana Nimejaribu Kuweka UZI Humu NIMESHINDWA Kabisa!! Sasa Mwenye Jibu Anisaidie Jmn!! Hivi Rais Anaweza KUMTEUA Mtu Kuwa Na Wkt Huo Huo KUMTEUA Kuwa WAZIRI Na Kumwapisha Kuanza Kazi Yake, Kabla Ya BUNGE Kuthibitisha Ubunge Wake Kwa Kumwapisha Pale BUNGENI!!!!?? Hii Imekaa Vp Kisheria!!??
 
Sisi hawa mawaziri hatukuwataka maana ni mizigo.

Jamani hakuna shule ya sekondari inahitaji head prefect? Yupo mwenye sifa lukuki anaitwa Dr Kigwangalla. My young brother Kigwangalla, behave as a MINISTER please.
 
Back
Top Bottom