Dr. Kigwangallah unapotea, tafuta staili nyingine

makaptula

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
200
66
Nimesoma Maelezo ya Dr namna alivyojitetea kwa kufanya ziara zake za kushtukiza.

Nimegundua yafuatayo cha kwanza kabisa Dr
Uelewa wake ni Mdogo sana katika masuala yakisheria.
Amegusia swala la sheria za kazi na amekiri kuzipitia nakujirizisha kisha kuchukua hatua.

Hapo Dr na udocta wake ameshindwa kugundua kwamba sheria hii imepitwa na wakati na si hilo tu ameshindwa kugundua ni nani anayepaswa kufunga mageti pale mtumishi anapochelewa.

Kwanin nasema imepitwa na wakati ni kwasababu wakati sheria hii inatungwa kwanza kabisa watumishi Wa umma wengi wao walikuwa wanaishi kwenye nyumba za serikali zilizo Karibu na maofisi yao.

Pili wakati sheria hiyo inatungwa hakukuwa na foleni za barabarani na mambo mengine lukuki.
Ameshindwa gundua kwamba serikali yake ndo chanzo cha haya yote.

Kwanin nasema serikal yake ndo chanzo cha haya yote ni kwasababu.
Moja wenyewe ndio walioshiriki kuuza nyumba za serikali na kuwaacha watumishi wakiishi kama kunguru mwitu.

Pili serikali yake imeshindwa kuboresha miundombinu nakutatua kero za msongamano Wa magari barabarani nk nk.
Pili Dr ameziirisha kwamba uwezo wake Wa kufikiri ni Mdogo sana kwanin nasema hivi.

Moja, Haiwezekani Leo hii unamfananisha waziri au mkurugenzi Wa taasisi na mfanyakazi Wa kawaida. Kwanin ? Kwanza kabisa mawaziri na wakurugenzi huwa hupewa usafiri na madereva.

Wengi wao hawategemei usafiri Wa daladala ambao ni kero kubwa, mfanyakazi wakawaida hata kukodi baiskeli imuwaishe kituoni hana leo hii unamfananisha na waziri au mkurugenzi ambaye amewezeshwa kwa kila kitu, kuanzia usafiri, mafuta mpaka dereva.

Pili, Leo hii ukisema unaamka SAA kumi usiku ili uwahi saa moja na nusu hapo kuna shida kidogo kwanini.

Kwanza kabisa ingempasa kujua heografia ya makazi Wa DSM ikoje,wengine wanaishi tabata, wengine gongolamboto nk huko Kuna changamoto nying sana likiwemo swala zima la vibaka, kutopata usafiri kwa wakati nk no.

Dr kama ni mtu mwenye busara na hekima angekaa na wafanyakazi wake ili ajue nin sababu ya wao kuchelewa kisha aangalie ni namna gani anaweza tatua hiyo kero na si kushtukiza au kufunga mageti.

Namfananisha na Nyumbu Wa kreta anayetazama anapokwenda na si anapotoka hata kama anapokwenda kuna simba basi atalazimisha kupita mwishowe anakuwa kitoweo kwa simba.
 
Acha awanyooshe wamezidi uvivu

Wanaowai kazini kwani wao hawapendi kuchelewa?

Wanyooshwe tu
 
Semina elekezi.
Sasa hivi wanatapatapa kutafuta umaarufu wakati hali ya mwananchi wa kawaida bado ni tete.
 
Dr. Kigwa namuunga mkono kuhusu dhamira yake lakini nakataa approach yake. Mimi ningekuwa yeye kazi yangu ni kudeal na KM tu ambae ndio bosi wa watumishi. Pili mchambuzi nimekusoma na nimekuelewa sana. Asante kwa maoni yako.
 
Dr. Kigwa namuunga mkono kuhusu dhamira yake lakini nakataa approach yake. Mimi ningekuwa yeye kazi yangu ni kudeal na KM tu ambae ndio bosi wa watumishi. Pili mchambuzi nimekusoma na nimekuelewa sana. Asante kwa maoni yako.
Dc Julius Mtatiro
 
Last edited by a moderator:
Umeongea vizuri mleta mada isipokua kwenye sheria tu, it seems wewe pia ni mbumbumbu wa sheria... sheria haipitwi na wakati hadi ibadilishwe, kwahiyo ndugu yangu kama hiyo sheria aliyoipitia ndio ilinayostand, basi hakuna ujanja

Labda ibadilishwe, au iwe imebadilishwa
 
Mwacheni waziri hafanye kazi. Kama wanashindwa kuwai waache kazi kwani kuna watu kibao wanatafuta kazi. Wafanyakazi wanatakiwa wawe wabunifu, pangisha nyumba yako iliyo tabata halafu tafuta nyumba ya kupanga karibu na kazini.
 
Wewe ndio hujui kwamba sheria hata kama imepitwa na wakati kama haijafutwa inaendelea kutumika kama ilivyo! Pili wewe unadhani Dr kigwangala ana uelewa mdogo angeweza kuwa dactari, mbunge na hatimae kuwa Waziri? Acheni hizo na kwa maelezo yako inaonesha huji kuwa Waziri ni overall in charge wa wizara yake kifupi ni kwamba ndio msimamizi wa kuona sera za chama chake zinatekelezwa na watumishi wa umma ndani ya wizara husika.
 
Jerusalem kuwa dr, kisha mbunge then waziri haimaanishi unajua kila kitu mkubwa.
 
Kigangwala hana kazi ya kufanya au labda hakuielewa job description yake vizuri au labda ni kichwa boksi.Nimependa approach za Prof Muhongo na Charles Mwijage.Wa kwanza ameanza kufanya Kazi,na wa pili yupo kimya amejichimbia chimbo akipanga mikakati mizito ya namna ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,wizara yake ahitaji matamko na ziara za kushtukiza bali inahitaji mipango bunifu hasa kwani sekta hii iko nyuma sana hapa Tanzania.
 
Mwacheni waziri hafanye kazi. Kama wanashindwa kuwai waache kazi kwani kuna watu kibao wanatafuta kazi. Wafanyakazi wanatakiwa wawe wabunifu, pangisha nyumba yako iliyo tabata halafu tafuta nyumba ya kupanga karibu na kazini.

Mkuwa si kila sehemu waweza pata nyumba ya kupanga Karibu na offisi yako.
Vile vile tambua ya wafanyakazi wametofautiana vipato hawawezi pangisha sehemu mbili kwa Mara moja.

Stail yake kwa sasa imekuwa ya ki old school atafute stail nyingine, vinginevyo anajichoresha
 
Aisee!
Assumption ni watumishi wote wapo dar au?
Sijaskia watoto wa shule wakibadilishiwa muda wa kufika shuleni.
Changamoto zipo lakini kumbukeni kuna watumishi mikoani wapo kwenye mazingira magumu zaidi na wanajitolea kwa moyo kuhudumia wananchi.
Hoja ya kuboresha mazingira ya kazi ina mashiko na inatakiwa izungumziwe kwa uzito wa pekee sio kama ya kutetea kutowajibika
 
Back
Top Bottom