Dr Kafumu anusa kushindwa kesi ya Uchaguzi Igunga, amkataa Jaji......

Hii ni Habari katika Habari Leo Jumamosi

MBUNGE wa Jimbo la Igunga, Dk Dalaly Kafumu (CCM) amesema hana imani na Jaji Mary Shangali kuendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye, dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.

Akisoma barua ya Dk. Kafumu mbele ya mahakama hiyo jana, Wakili wa Mbunge huyo, Anthony Kanyama alisema kuwa mteja wake hana imani na Jaji huyo kwa kuwa baadhi ya maamuzi yanakwenda ndivyo sivyo.

Akibainisha sababu za Dk Kafumu kutokuwa na imani na Jaji huyo huku akisoma barua yake ni pamoja na kudaiwa kuwatukana na kuwadhalilisha mashahidi wa upande wa utetezi akitoa mfano shahidi (DW14), Mahakama kuchukua nafasi ya mawakili wa mdai kwa kuwahoji maswali mashahidi wa mdaiwa badala ya kutaka ufafanuzi juu ya maelezo yao.

Akiendelea kusoma alisema sababu nyingi ni Jaji kuwa mkali pasipo sababu kwa mawakili wa utetezi kila walipohoji mashahidi wa upande wa mdai.

Sababu nyingine imeelezwa kuwa kitendo cha mawakili wa upande wa utetezi kunyimwa nakala ya mwenendo wa shauri mara tu usikilizaji wa kesi kwa pande zote kukamilika ili kuwasaidia kuandaa hoja za majumuisho.

Akimalizia kusoma barua hiyo kwa niaba ya Dk Kafumu, wakili Kanyama alisema kuwa kutokana na hali hiyo mashahidi wake muhimu wamekataa kuja kutoa ushahidi kwa kuogopa kudhalilishwa. Nje ya Mahakama hiyo, Dk Kafumu alisema:

“Sijashinikizwa maamuzi haya ni kutoka moyoni mwangu sina imani na Jaji huyu kwani nimepoteza kabisa imani na yeye kuendelea kusikiliza shauri hili na kwamba kwa ujumla wake naona haki haitatendeka kabisa kwa dalili hizo za waziwazi zilizokwishajionesha naomba shauri hili lisikilizwe na Jaji mwingine.’’

Naye Profesa Abdallah Safari, Wakili wa Kashindye ambaye katika uchaguzi mdogo aligombea kwa tiketi ya Chadema, alisema kuwa maombi hayo si ya msingi kwa Dk Kafumu huku akitoa mifano mbalimbali ya kesi kama hizo na kuongeza kuwa kama wanaona hali ni mbaya, wasubiri wakate rufaa mara baada ya kesi hiyo kuhukumiwa.

Baada ya kupitia pande zote mbili na kusoma kwa muda Jaji huyo alitupilia mbali ombi hilo la Dk Kafumu na kusema kuwa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kwa kufuata taratibu na kanuni za kimahakama.

Jaji huyo alisema hakuna sababu za msingi zilizotolewa na maelezo yanayolalamikiwa yanaweza kufanywa katika rufaa na kutaka Mahakama iachiwe uhuru wa maamuzi pasipo kuingiliwa kwa maamuzi hayo na kuongeza kuwa kesi hizo zina gharama kubwa kwa uendeshwaji wake.

Alisema maamuzi hayo hayajabainisha kama mshindi ni nani katika kesi hiyo kwani bado ushahidi unaendelea kusikilizwa kwa mjibu madai na upande wa serikali.

Kesi hiyo itaendelea Mei 21, mwaka huu huku mashahidi wanne wa majibu madai watatoa ushahidi huo akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi.

MY TAKE: Ni wazi Dr Kafumu ameona mambo yanakwenda sivyo ndivyo kwake, lakini tusijipe moyo huenda ikawa kama Segerea.


Jaji huyu ni mnazi mkubwa wa Chadema na alishaapa kwamba Kijani safari hii itamtambua. Huyu mama ana undugu na Freeman Mbowe. Kwa staili ile ile ya Lema na Rwakibalila, mama anataka kumlaza Dr. Kafumu.
 
Mkubwa mmoja juzi kadai viongozi wengine wanafikiria kwa kutumia matumbo yao. Tusisahau hawa Majaji nao ni viongozi.
 
Jaji huyu ni mnazi mkubwa wa Chadema na alishaapa kwamba Kijani safari hii itamtambua. Huyu mama ana undugu na Freeman Mbowe. Kwa staili ile ile ya Lema na Rwakibalila, mama anataka kumlaza Dr. Kafumu.
Mbopo, kama kawaida yako umekosa mshipa wa aibu ukaamua kuleta uwongo wako bila shida!
 
Kwahiyo Dr.Kafumu anaogopa kufomuliwa na mwl. Kashindye! awe mpole tu kwani inawezekana hiyo ni janja ya nyani ili atuzuge na baadae matokeo yawe ya kushangaza.
 
Hamna kesi hapo. Huyo jaji na Kafumu wanacheza tamthilia ya kutuzuga watanzania
hawa jamaa ni wanaakili sana kwanza wanataka watuaminishe kuwa jaji yupo upande CDM hafu badae watageuza kibao kwenye hukumu CDM wakilalamika wataambiwa jaji alikuwa upande wao so they have to take care things is like game.
 
km ndivyo basi yale mabilioni na vuruguza igunga zilikuwa za nini?Hau jamaa na chama chake hawakuona mbali?Pr. Safari si wa taratibu atwabana vibaya na hata wakitengua matokeo wananchi wana kitu ambachi ni biased kichwani.So ikiwa public tuu tayari kushinda CCM ni damage zaidi ya kushindwa.Mazingira yote si favourable kwao.
 
Back
Top Bottom