Dr Kafumu anusa kushindwa kesi ya Uchaguzi Igunga, amkataa Jaji...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Kafumu anusa kushindwa kesi ya Uchaguzi Igunga, amkataa Jaji......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, May 19, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hii ni Habari katika Habari Leo Jumamosi

  MBUNGE wa Jimbo la Igunga, Dk Dalaly Kafumu (CCM) amesema hana imani na Jaji Mary Shangali kuendelea kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

  Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye, dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.

  Akisoma barua ya Dk. Kafumu mbele ya mahakama hiyo jana, Wakili wa Mbunge huyo, Anthony Kanyama alisema kuwa mteja wake hana imani na Jaji huyo kwa kuwa baadhi ya maamuzi yanakwenda ndivyo sivyo.

  Akibainisha sababu za Dk Kafumu kutokuwa na imani na Jaji huyo huku akisoma barua yake ni pamoja na kudaiwa kuwatukana na kuwadhalilisha mashahidi wa upande wa utetezi akitoa mfano shahidi (DW14), Mahakama kuchukua nafasi ya mawakili wa mdai kwa kuwahoji maswali mashahidi wa mdaiwa badala ya kutaka ufafanuzi juu ya maelezo yao.

  Akiendelea kusoma alisema sababu nyingi ni Jaji kuwa mkali pasipo sababu kwa mawakili wa utetezi kila walipohoji mashahidi wa upande wa mdai.

  Sababu nyingine imeelezwa kuwa kitendo cha mawakili wa upande wa utetezi kunyimwa nakala ya mwenendo wa shauri mara tu usikilizaji wa kesi kwa pande zote kukamilika ili kuwasaidia kuandaa hoja za majumuisho.

  Akimalizia kusoma barua hiyo kwa niaba ya Dk Kafumu, wakili Kanyama alisema kuwa kutokana na hali hiyo mashahidi wake muhimu wamekataa kuja kutoa ushahidi kwa kuogopa kudhalilishwa. Nje ya Mahakama hiyo, Dk Kafumu alisema:

  “Sijashinikizwa maamuzi haya ni kutoka moyoni mwangu sina imani na Jaji huyu kwani nimepoteza kabisa imani na yeye kuendelea kusikiliza shauri hili na kwamba kwa ujumla wake naona haki haitatendeka kabisa kwa dalili hizo za waziwazi zilizokwishajionesha naomba shauri hili lisikilizwe na Jaji mwingine.’’

  Naye Profesa Abdallah Safari, Wakili wa Kashindye ambaye katika uchaguzi mdogo aligombea kwa tiketi ya Chadema, alisema kuwa maombi hayo si ya msingi kwa Dk Kafumu huku akitoa mifano mbalimbali ya kesi kama hizo na kuongeza kuwa kama wanaona hali ni mbaya, wasubiri wakate rufaa mara baada ya kesi hiyo kuhukumiwa.

  Baada ya kupitia pande zote mbili na kusoma kwa muda Jaji huyo alitupilia mbali ombi hilo la Dk Kafumu na kusema kuwa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa kwa kufuata taratibu na kanuni za kimahakama.

  Jaji huyo alisema hakuna sababu za msingi zilizotolewa na maelezo yanayolalamikiwa yanaweza kufanywa katika rufaa na kutaka Mahakama iachiwe uhuru wa maamuzi pasipo kuingiliwa kwa maamuzi hayo na kuongeza kuwa kesi hizo zina gharama kubwa kwa uendeshwaji wake.

  Alisema maamuzi hayo hayajabainisha kama mshindi ni nani katika kesi hiyo kwani bado ushahidi unaendelea kusikilizwa kwa mjibu madai na upande wa serikali.

  Kesi hiyo itaendelea Mei 21, mwaka huu huku mashahidi wanne wa majibu madai watatoa ushahidi huo akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi.

  MY TAKE: Ni wazi Dr Kafumu ameona mambo yanakwenda sivyo ndivyo kwake, lakini tusijipe moyo huenda ikawa kama Segerea.
   
 2. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwanaCDM halisi ila sina imani na mahakama za TZ,labda kesi hizi zipelekwe The Hague kwa Ocampo
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii nayo inaweza kugeuka kuwa kama kesi ya mahanga.
  Hawa majaji hawasomeki kabisa.
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hamna kesi hapo. Huyo jaji na Kafumu wanacheza tamthilia ya kutuzuga watanzania
   
 5. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wana Igunga wanalalama mahindi yaliisha siku ile ile ya uchaguzi. CCM wapelekee mahindi mengine.

  Chadema wapelekeeni weledi
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ukiona hivyo basi ujue wamemfuata Jaji wamuhonge akawatolea nje. Sasa wanakuja na single ya kutokuwa na imani
   
 7. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tuombe Mungu haki itendeke Jaji kutoa hukumu yenye kufuata misingi ya haki ingawa mahakama zetu haziaminiki kabisa
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  CHEUSI CHEKUNDU,JAJI ANAWEZA KUWA NA MSIMAMO MZURI ILA SIKU YA HUKUMU WARAKA WA IKULU NDIO UTAKAOAMUA HIVYO TuSIJIPE MOJO MKUU WA KAYA NDIO JAJI WA KESI HIZI,AKIMALIZA VIKAO VYAKE NA KINA BECKAM ATAKUJA KUTUMA WAKALA IGUNGA NA MAMBO YATABADILIKA KAMA SEGEREA
   
 9. h

  hoyce JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wanataka ajitoe wampange Rwakibalila
   
 10. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  hata mim nahisi kitu kama hicho!
   
 11. K

  KUTATABHETAKULE JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 807
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 80
  Ahh!! Mie napita tu, nikirudi nitasema.
   
 12. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #12
  May 19, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Duh! Nimechoka kabisa na mfumo wa uendeshaji wa kesi katika mahakama zetu hasa katika kesi za kupinga uchaguzi.... Kama mahakama zingefuata haki kiukweli KAFUMU hachomoki ila kwa kuwa hii nchi ni ya kufikilika basi lolote laweza kutokea..............
   
 13. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,287
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huwezi jua labda hapo jaiji na kafumu wanacheza cinema lakini kumbe wako upande mmoja, wanacheza cinema ili akija akitoa matokeo ya kumpendelea kafumu watu wasihoji sana!
   
 14. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Nchi yetu hii imejaa usanii, jk kawa msanii sembuse majaji, muhimu tujiandae na m4c pia uchaguzi wa 2015 vinginevyo itakuwa miujiza
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  wapo wachache wanaosimama kwenye ukweli kama yule wa sumbawanga. huenda na huyu wa tabora ni mmojawao
   
 16. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Rushwa za kugawa mahindi kwa wapigakura wa Igunga na Magufuli kujenga daraja zinatosha kutengua matokeo ya uchaguzi huo!
   
 17. p

  pomoni Member

  #17
  May 19, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tusubiri hukumu na tufuatilie kwa undani mwenendo mzima wa kesi unavyoendelea, hukumu utegemea sana ushahidi unaowasilishwa mahakamani.
   
 18. m

  matawi JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kafumu anaogopa kufumuliwa? Kashindye msamehe huyo ni msukuma mwenzako
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Au kama Arusha. Kesi hizi mbili zimeondoa kabisa Imani ya wananchi wengi kuhusu uhuru wa mahakama zetu. Maamuzi ya kesi hizi mbili ni vice versa. Tusubiri na hukumu ya Ubungo wiki ijayo.
   
 20. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Amsamehe kwa kosa gani?
   
Loading...