Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,492
- 2,361
Uwezo wake wa kubadili upepo ndio umenifanya kutafuta kujua Dr. Josephat Gwajima ni nani na ni mtu wa aina gani. Labda ngoja niwakumbushe kidogo.
1. Kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 ailimchukua saa moja na nusu tu kuwasaidia UKAWA wasizame kutokana na tuhuma za Dr Slaa
2. Mwaka jana CCM walitaka kuleta mizengwe kumkabidhi chama Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, aliposimama kulizungumzia hilo ndipo CCM wakaanza kukimbizana na kuharakisha makabidhiano
3. Sakata la Mkuu wa mkoa wa dar Mh. Paul Christian Makonda kudaiwa kufoji vyeti. Kabla ya Mch Dr. Gwajima kuongea hili jambo lilishaanza kukosa nguvu, lilianza kupoa na hatimae lingefutika kabisa na kubaki historia, kitenda cha yeye kuongea limeanza upya na kwa kasi kubwa hadi kutishia nafasi ya Makonda na mustakabali wake wa kisiasa.
4. Sekeseke la madawa ya kulevya, aliposimama kuonge na vyombo vya habari tu ilionekana ni zoezi la kukomoana na likapoteza nguvu pamoja na kukosa mvuto japo alitumia maneno ya kawaida sana
Hiyo ni baadhi ya mifano michache inayoonyesha uwezo wake wa kubadili hali ya mambo. Hii imenipelekea kujiuliza huyu bwana ni nani?
Nimejaribu kugoogle sijapata historia yake, nakumbuka kuna andiko la [HASHTAG]#yericko nyerere[/HASHTAG] akimtaja kama jasusi wa kiwango cha juu sana (Kaka [HASHTAG]#yericko nyerere[/HASHTAG] kama hutojali naomba link ya andiko lako).
Kama kuna mtu ana CV ya Dr. Gwajima naomba aiweke pia kama kuna mtu anaweza kutusaidia kujua Dr. Gwajima ni mtu wa aina gani atusaidie.
(Angalizo: Lengo la mada hii ni kujifunza na si vinginevyo)
Karibuni kwa michango