Dr. John Pombe Magufuli Tena

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Magufuli alipuka tena

headline_bullet.jpg
Aapa ni lazima kuvunja mabango
headline_bullet.jpg
Asema hakuna mtu wa kumzuia

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuacha ubabe kauli ambayo juzi aliirudia kwa mawaziri na makatibu wakuu mjini Dodoma katika semina elekezi, Waziri huyo amepania kwa vyovyote iwavyo ni lazima abomoe mabango yote ya biashara ya barabarani. Magufuli aliendelea kuwasha moto huo jana safari hii akisema hakuna wa kumzuia kuondoa mabango hayo kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi. Alisema kuanzia sasa wenye mabango wasipoyaondoa kwa hiyari yao watayaondoa kwa nguvu kwa kuyavunja vunja.
Akizungumza jana kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, Dk. Magufuli alisema hakuna wa kumzuia kutekeleza wajibu huo kwa sababu anachokifanya ni kufuata sheria inayolinda barabara.

Waziri Magufuli alipinga utetezi uliotolewa hivi karibuni na kiongozi mmoja wa Halmashauri (hakumtaja) kuwa mabango hayo yanaongeza kipato kwa kukusanya kodi. Alisema hakuna ushahidi wa jambo hilo kwani fedha zinazokusanywa zimekuwa zikiishia mikononi mwa watu binafsi na wala serikali hainufaiki na chochote. “Mkakati wangu utabaki palepale hauwezi kubadilika, ni lazima mabango yataondolewa ili kuweka barabara zetu salama na safi, haiwezekani barabara zijengwe kwa mabilioni ya pesa halafu mtu anakuja kuharibu kwa kuweka mabango,” alisema Dk. Magufuli.

Hivi karibuni Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alikaririwa akipinga hatua hiyo kwa kueleza Halmashauri yake inapata mapato mengi kutoka kwenye mabango hayo ya biashara, fedha ambazo zinatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli alipingana na maelezo hayo kwa kusema kuwa kama kweli kiongozi huyo anaeleza ukweli juu ya jambo hilo, atoe mchanganuo wa jinsi fedha za mabango zilivyotumika na sio kusema kinadharia.

“Hakuna pesa za mabango zilizojenga barabara, kama zipo watuonyeshe basi hata moja tuone kuliko kueleza tu kwa maneno, hizi pesa wanajilipa posho tu, hivyo nasema kimya kingi kina mshindo na hivi karibuni mtaona mambo yangu," alisisitiza.
Katika kipindi hicho, Waziri Magufuli alieleza mafanikio ya Wizara yake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara pamoja na kutafuta njia za kuzilinda ili zisiharibiwe kwa muda mfupi.
Alisema katika kuhakikisha matumizi ya barabara yanakwenda vizuri, wameimarisha kitengo cha upimaji wa uzito kwa kuwaongezea posho na mishahara watumishi ili kuwafanya waepukane na vishawishi vya kupokea rushwa.
Alimpongeza Rais Kikwete kwa kutoa kipaumbele katika ujenzi wa barabara zote zinazounganisha mikoa, wilaya na nchi jirani kwa kiwango cha lami. Alisisitiza wizara yake itaendelea kusimamia miradi hiyo pamoja na kuendelea na msimamo wa kutowalipa pesa makandarasi wasiofuata mikataba na sheria za nchi.
Juzi akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema uvivu, uzembe, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, vitendo vya utovu wa uadilifu kama vile wizi, ulevi wa kupindukia, uzinzi, majigambo, ubabe, uonevu na dhuluma ni miongoni mwa mambo yanayomfanya kiongozi apoteze sifa za kuwa kiongozi.
Aliwataka viongozi hao kuwa mfano mwema kwa wananchi kwa matendo.
Hivi karibuni Waziri Magufuli alijikuta akifungwa ‘gavana’ baada ya kutangaza bomoabomoa kubwa katika barabara kuu zote nchini kwa watu aliosema wamevamia eneo la hifadhi ya barabara.
Kutokana na operesheni hiyo, Wakala wa Barabara (Tanrods) waliweka alama za X kwa nyumba zote zilizoko kwenye eneo la hifadhi ya barabara kwa nia ya kuanza kuzivunja.
Kutokana na mkakati huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa ziarani mkaoni Kagera, mbele ya Magufuli alitangaza kusitishwa kwa bomoa hiyo, na kutaka wakuu wa mikoa wafanye thathmini ya kina juu ya madhara ya bomoa hiyo na kujua kwa hakika ni nyumba ngapi hasa zitahusika na ni kwa jinsi gani serikali itasaidia.
Kauli ya kupinga mpango wa Magufuli pia ilitangazwa na Rais Kikwete alipotembelea Wizara ya Ujenzi, akiwataka watendaji wa wizara hiyo kuacha kuwa wababe na kuwataka waendeshe operesheni ya bomoabomoa kwa kuwa na sura ya utu, kama vile kuwapa watu muda wa kutosha kubomoa nyumba zao na pale serikali ilipowasababisha watu kuangukia kwenye hifadhi ya barabara ni lazima wananchi wafidiwe.
Miaka ya katikati ya tisini akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Magufuli alisimamia operesheni ya bomoabomoa kando kando ya barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam kuanzia Ubungo hadi Mbezi Luis. Operesheni hiyo ilirudiwa tena na Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2000-2005. Maelfu ya watu waliathirika na operesheni hiyo, huku wengine wakirejea kuwa masikini wa kutupwa kutokana na kuvunjiwa nyumba pekee walizokuwa wanamiliki bila kulipwa fidia yoyote.
Wamiliki wa mabango nchini wamekuwa na malumbano na Tanroads juu ya nia ya kutaka kuvunja mabango yao, na mara kadhaa wamejaribu kuwasiliana nao kutafuta njia mwafaka wa kufikiwa kwa utekelezaji wa uondoaji wa mabango hayo, lakini mara zote wamekwama.
Wadau hao wanapinga uamuzi wa jumla jumla wa kubomoa mabango yote, wakitaka kuweko na ukaguzi ili kubaini ni lipi halitakiwi au limekaa sehemu isiyofaa kwa nia ya kujipanga upya, lakini Tanroads wamekuwa wakikataa kwa maelezo kwamba ni lazima mabango yote nchi nzima yabomolewe kwanza ili kuanza upya.

Source IPPMEDIA: Home
 
****** atasema ubabe umezidi..hakuna mtu anavunja sheria kama ******
 
kwa kweli sijawahi kuona waziri msanii na wa ovyo kama huyu! alipokuwa mifugo na uvuvi, kazi yake ilikuwa kuchoma moto nyavu nchi nzima, karudishwa ujenzi nataka kubomoa mabango, hivi huyu anazijua vizuri kazi anazopaswa kufanya mtu mwenye cheo cha waziri?
 
Ndiyo kazi aliyokabidhiwa na JK. JK hajalalamika alisema apunguze kasi hadharani hatujui walichoongelea wao wenyewe
 
Mbona alipoambiwa aangalie na ubinadamu hakujibu au ni kwa sababu hatukumteua kuwa waziri anaweza kutamba kwa uongo na maigizo?!
 
Dr Magufuri nakumbuka ktk dakika zako 45 uligusia utengenezwaji wa barabara ya Lami kutokea manyon had kigoma kupitia Tabora,ikiwezekana ubabe wako wote hebu uuelekeze huko,kwan utabarikiwa na Mungu kupitia shukuran za wana Tabora na Kigoma,hata chama utakisaidia sana kupunguza matusi ya wapinzani.
 
wacheni afanye huohuo ubabe,sometimes wananchi tunajiamulia mambo na kuingia kwenye maeneo yasiyotakiwa kujenga! tujizoeshe kufwata sheria
 
mi hapo sioni kosa ni vizuri abomoe mabango yote ili mandhari ipendeze, wenzetu wanaweka mabango kwenye vituo vya mabasi/daladala na kwenye shopping malls si tunaweka kwa barabara na hii yote ni kutokana na asili yetu ya uchafu na ubinafsi. Utakuta mtu anakula muwa akiwa kwa daladala anatupa maganda barabarani au maji chupa anatupa barabarani ukiangalia hakuna dustbin ni uchafuzi tu wa barabara.

Shime Pombe hivyo ndivyo inavyotakiwa mi nafikiri wakikupinga uhamie Rwanda bse raisi kama Kagame anahitaji viongozi wanaosimamia sheria na sio wanaovunja sheria kama viongozi wetu wa Tz.
 
Huyu ni msanii mwingine na juu ya hapo ni fisadi nambari one aliyetafsiri vibaya uamuzi wa baraza la mawaziri na hatimaye kuuza nyumba za serikali kwa civil servants wengi kati yao wengine hawakustahili, na hizo nyumba wameishaziuza kwa matajili!! Kama huamini nenda Oysterbay ukaone jinsi magorofa yalivyojengwa baada ya zile zilizokuwa za serikali kuvunjwa!!
 
kwa kweli sijawahi kuona waziri msanii na wa ovyo kama huyu! alipokuwa mifugo na uvuvi, kazi yake ilikuwa kuchoma moto nyavu nchi nzima, karudishwa ujenzi nataka kubomoa mabango, hivi huyu anazijua vizuri kazi anazopaswa kufanya mtu mwenye cheo cha waziri?
utendaji wake hana tofauti na lyatonga mrema utendaji wao ni.kutafuta cheap popularity kupitia magazeti
 
Magufuli is right nchi lazima iendeshwe kwa sheria na sio ubinadamu wala porojo. Mh Rais ndio populist maana anapenda na anaziwezea sana siasa za majukwaani, haikunishangaza alipomdhalilisha Dr J.P. Magufuli ili kujiongezea umaarufu ambao ulikuwa umepungua kiasi cha kukaribia asilimia sifuri.
Mwacheni Magufuli afanye kazi. Mumezoea giza kwa hiyo lazima mwangaza uwaumize macho
 
Magufuli yuko sawa, sikumuelewa baba riz1 kumzuia kufuata sheria kama umejenga barabarani kwanini ubakie ondoa mjengo wako. Kaza buti pombe
 
Magufuli alipuka tena

headline_bullet.jpg
Aapa ni lazima kuvunja mabango
headline_bullet.jpg
Asema hakuna mtu wa kumzuia

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuacha ubabe kauli ambayo juzi aliirudia kwa mawaziri na makatibu wakuu mjini Dodoma katika semina elekezi, Waziri huyo amepania kwa vyovyote iwavyo ni lazima abomoe mabango yote ya biashara ya barabarani. Magufuli aliendelea kuwasha moto huo jana safari hii akisema hakuna wa kumzuia kuondoa mabango hayo kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi. Alisema kuanzia sasa wenye mabango wasipoyaondoa kwa hiyari yao watayaondoa kwa nguvu kwa kuyavunja vunja.
Akizungumza jana kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, Dk. Magufuli alisema hakuna wa kumzuia kutekeleza wajibu huo kwa sababu anachokifanya ni kufuata sheria inayolinda barabara.

Waziri Magufuli alipinga utetezi uliotolewa hivi karibuni na kiongozi mmoja wa Halmashauri (hakumtaja) kuwa mabango hayo yanaongeza kipato kwa kukusanya kodi. Alisema hakuna ushahidi wa jambo hilo kwani fedha zinazokusanywa zimekuwa zikiishia mikononi mwa watu binafsi na wala serikali hainufaiki na chochote. "Mkakati wangu utabaki palepale hauwezi kubadilika, ni lazima mabango yataondolewa ili kuweka barabara zetu salama na safi, haiwezekani barabara zijengwe kwa mabilioni ya pesa halafu mtu anakuja kuharibu kwa kuweka mabango," alisema Dk. Magufuli.

Hivi karibuni Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alikaririwa akipinga hatua hiyo kwa kueleza Halmashauri yake inapata mapato mengi kutoka kwenye mabango hayo ya biashara, fedha ambazo zinatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli alipingana na maelezo hayo kwa kusema kuwa kama kweli kiongozi huyo anaeleza ukweli juu ya jambo hilo, atoe mchanganuo wa jinsi fedha za mabango zilivyotumika na sio kusema kinadharia.

"Hakuna pesa za mabango zilizojenga barabara, kama zipo watuonyeshe basi hata moja tuone kuliko kueleza tu kwa maneno, hizi pesa wanajilipa posho tu, hivyo nasema kimya kingi kina mshindo na hivi karibuni mtaona mambo yangu," alisisitiza.
Katika kipindi hicho, Waziri Magufuli alieleza mafanikio ya Wizara yake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara pamoja na kutafuta njia za kuzilinda ili zisiharibiwe kwa muda mfupi.
Alisema katika kuhakikisha matumizi ya barabara yanakwenda vizuri, wameimarisha kitengo cha upimaji wa uzito kwa kuwaongezea posho na mishahara watumishi ili kuwafanya waepukane na vishawishi vya kupokea rushwa.
Alimpongeza Rais Kikwete kwa kutoa kipaumbele katika ujenzi wa barabara zote zinazounganisha mikoa, wilaya na nchi jirani kwa kiwango cha lami. Alisisitiza wizara yake itaendelea kusimamia miradi hiyo pamoja na kuendelea na msimamo wa kutowalipa pesa makandarasi wasiofuata mikataba na sheria za nchi.
Juzi akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema uvivu, uzembe, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, vitendo vya utovu wa uadilifu kama vile wizi, ulevi wa kupindukia, uzinzi, majigambo, ubabe, uonevu na dhuluma ni miongoni mwa mambo yanayomfanya kiongozi apoteze sifa za kuwa kiongozi.
Aliwataka viongozi hao kuwa mfano mwema kwa wananchi kwa matendo.
Hivi karibuni Waziri Magufuli alijikuta akifungwa ‘gavana' baada ya kutangaza bomoabomoa kubwa katika barabara kuu zote nchini kwa watu aliosema wamevamia eneo la hifadhi ya barabara.
Kutokana na operesheni hiyo, Wakala wa Barabara (Tanrods) waliweka alama za X kwa nyumba zote zilizoko kwenye eneo la hifadhi ya barabara kwa nia ya kuanza kuzivunja.
Kutokana na mkakati huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa ziarani mkaoni Kagera, mbele ya Magufuli alitangaza kusitishwa kwa bomoa hiyo, na kutaka wakuu wa mikoa wafanye thathmini ya kina juu ya madhara ya bomoa hiyo na kujua kwa hakika ni nyumba ngapi hasa zitahusika na ni kwa jinsi gani serikali itasaidia.
Kauli ya kupinga mpango wa Magufuli pia ilitangazwa na Rais Kikwete alipotembelea Wizara ya Ujenzi, akiwataka watendaji wa wizara hiyo kuacha kuwa wababe na kuwataka waendeshe operesheni ya bomoabomoa kwa kuwa na sura ya utu, kama vile kuwapa watu muda wa kutosha kubomoa nyumba zao na pale serikali ilipowasababisha watu kuangukia kwenye hifadhi ya barabara ni lazima wananchi wafidiwe.
Miaka ya katikati ya tisini akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Magufuli alisimamia operesheni ya bomoabomoa kando kando ya barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam kuanzia Ubungo hadi Mbezi Luis. Operesheni hiyo ilirudiwa tena na Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2000-2005. Maelfu ya watu waliathirika na operesheni hiyo, huku wengine wakirejea kuwa masikini wa kutupwa kutokana na kuvunjiwa nyumba pekee walizokuwa wanamiliki bila kulipwa fidia yoyote.
Wamiliki wa mabango nchini wamekuwa na malumbano na Tanroads juu ya nia ya kutaka kuvunja mabango yao, na mara kadhaa wamejaribu kuwasiliana nao kutafuta njia mwafaka wa kufikiwa kwa utekelezaji wa uondoaji wa mabango hayo, lakini mara zote wamekwama.
Wadau hao wanapinga uamuzi wa jumla jumla wa kubomoa mabango yote, wakitaka kuweko na ukaguzi ili kubaini ni lipi halitakiwi au limekaa sehemu isiyofaa kwa nia ya kujipanga upya, lakini Tanroads wamekuwa wakikataa kwa maelezo kwamba ni lazima mabango yote nchi nzima yabomolewe kwanza ili kuanza upya.

Source IPPMEDIA: Home

Pombe Hafai Kuwa Hata Katibu Kata Kwani ni Muhasherati Kupindukia.
 
Back
Top Bottom