Dr Hamis Kigwangalla haeleweki ndani ya CCM

Muheshimiwa,

Huoni kama ungefanya kazi nzuri zaidi ukiwa hospitali ? kwakuwa nchi yetu ina uhaba wa wataalam ambao wengi wamekimbia nje na wengine kama wewe wamekimbia fani zao na kuishia kukaa bungeni?
 
Precise Pangolin,

Nakushukuru. Naomba nikujibu kwa ufupi tu kwamba, nimetoka Nzega kabla ya Bunge na nilipokuwa kule nilizunguka jimbo zima.

Pili: Model ya kuongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi ninayoipigia jaramba hapa niliishaitekeleza Nzega kwenye kilimo cha pamba na alizeti na imeonesha (kwa miaka mitatu sasa) mafanikio makubwa. Masomo niliyopata naona ni vema nikayafanyia uraghibishaji yakatekelezwa kitaifa, kwa faida ya watanzania na nchi yetu. Ninaongea kitu ninachokijua in theory na pia pragmatically.

Nachofuraia kwako ni hicho upo karibu,na unajibu hoja hao wengine ni porojo na siasa za kwenye internet waje huku kwenye siasa za majukwaaji na siasa za moja kwa moja.Kazi nzuri.
 
Mimi sitii kambi yoyote katika hizo kambi zenu. Mimi nafanya kazi ya wananchi kwa kadri ninavyoona inafaa! Na kama kuna jambo lina maslahi ya chama, nitalitekeleza kulinda na kujenga chama changu, period!

Kuhusu hoja zangu; ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi na ile ya makazi kutumia dhamana ya hazina za wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii, nilishasema kuwa nitashirikiana na wabunge wenzangu ili kuijenga nchi yetu. Kwangu mimi haijalishi kama nitajulikana kwa sababu ya ajenda hizi ama vipi, mimi ninachofia hapa ni kuona tunafanikiwa kuleta mabadiliko tarajiwa kwa nchi yetu.

Kiongozi ni lazima utokane na watu na uwatumikie watu hao, hivyo ni lazima ufikie matarajio ya watu, na si vinginevyo hata mara moja!

Safi sana bwana Hamisi
Sasa tunaomba utudokeze, Mwenyekiti wako alikuwa anategemea au kama bado ana mpango huo alikuwa anategemea kutumia njia gani kuzalisha Ajira milino tano kwa vijana kama alivyoahidi mwaka 2005 sababu toka kipindi hicho hatujamsikia tena japo kutupa kauli za kutufajiri kuhusu jambo hili sababu wengi wetu tunajua amefail asilimia zaidi ya 98% kwa hili moja peke yake.

Au kama unatofautiana naye, uwe wazi kwamba unatofautiana na mpango uliuokuwepo, utueleze na mapungufu yake yalikuwa ni nini hadi sio tu ukashindwa kutekelezeka bali ikashindikana hata kutake off.

Ama sivyo utueleze kwamba mpango mzima ulifanikiwa na sasa mnasonga mbele, ukisema haya na huo uwe mwisho wako
wa kusema sema juu ya swala la ajira kwa vijana

Ama utueleze kwamba siasa ni mchezo mchafu, hapa pia, ukimaliza tu huo pia uwe mwisho wako wa kusema sema sio juu ya swala hili la ajira peke yake bali na mengine yote sababu maandishi yako kwa wengi wetu humu JF hasa kwa jinsi tulivyo na machungu na hayo mashati yenu ya kijani huwa ni kama vile mnatutukana sisi wenyewe, wazazi wetu na watoto wetu na watoto wao na watoto wa watoto wao na marafiki pamoja na majirani zao.
 
Shule waliyotowa Mwanzisha thread (ingawa kidogo ameongeza chumvi), Members kama Mubi, Kulwa nk ni changamoto nzuri sana kwa Wabunge wote ambao wanawakilisha majimbo ya vijijini.

Msimu wa maembe Sikonge yanaoza tu kumbe China ni mali. Kilimo cha Pilipili kwa kiangazi huku Sikonge, watu wangeliweza kujivunia kilo kibao ila wanakaa tu wanakunywa kahawa....... ahhh, wengine hata kahawa hawana ila kusubiri tu Bibie apike ugali kwa Nswalu (Lami) na jamaa anauchapa huku akisubiri jioni akapate Wanzuki.......

Ninaamini Mbunge/Wabunge watalifanyia kazi hili swala.

Asiishie tu kwenye Pamba ambapo yeye ana kiwanda. Iende zaidi hadi kuwasaidia vijana wawe na mashamba yao na viwanda vyao vidogovidogo au mashamba yao kuzalisha bidhaa hizo tumewekewa juu......

MUBI: Asante sana kwa shule hiyo hapo juu....
 
Thank God leo Kigwangala kuwa muongelewaji humu ndani, lakini kwa upande wangu naomba niungane na wote wanaomataka kigwangala kufanya kazi zake nzega na si kwenye vyombo vya habari au Dar kama alivyoandika location yake, kwa msaada tu ni kwamba Dr hafanyi kazi kwenye jimbo lake bali anafanyia kwenye mitandao ya kijamii ambapo kwa bahati mbaya sana jimboni kwake kuna vibanda visivyopungua viwili tu na idadi ya watu wenye uwezo wa kutumia mitandao hiyo ni wa kuhesabika lakini kibaya zaidi ni kuwa moja ya vibanda hivyo alifungua yeye mwenyewe jirani na nzega motel kwa bahati mbaya akashindwa kumlipa mshahara mhudumu wake anayeitwa Ruhangisa ambaye alipelekea kumtaifisha kompyuta zote baadaya kuogopa mambo yasifike pabaya na internet cafe hiyo kwa sasa inamilikiwa na aliyekuwa msaidizi wake bw Ruhangisa aidha ameajiri watu wawili kama makatibu wake ambao kwa bahati mbaya kila mmoja anadai yeye ndiye katibu hivyo kulazimika kugombea piki piki ambayo mmoja(salum) amegoma kumpa mwenzake(kumotola) kwa hayo hayo yote kigwangala hawezi kufanya kazi nzega hata ziara anayodai kuwa kafanya jimbo zima si kweli kama anabisha athitibishe hapa kwani alifanya ziara kata si zaidi ya kumi baada ya kuona hali mbaya akaahirisha na kukimbili Dar!
Basi kama ni kweli hatari. Lakini pamoja na hayo muhimu kutumia nafasi ya kuuza bidhaa China , ambazo tumebahatika kutolipa ushuru zinapoingia China na pia kuuza bidhaa USA mpango wa AGOA. Sasa tumpe kazi ya huko aliko alete Wataalam toka huko Dar waje Nzega kufundisha jamii either katika production, processing , packaging na tayari kwa kuexport. Ahimize serikali iwe na incubators kwa upande wa Kilimo, madini ziwe Nzega.... utaona mambo hapo. Kila mtu jino jeupe, kuna kazi ya kufanya ahhhh.. safi tu.
 
Shule waliyotowa Mwanzisha thread (ingawa kidogo ameongeza chumvi), Members kama Mubi, Kulwa nk ni changamoto nzuri sana kwa Wabunge wote ambao wanawakilisha majimbo ya vijijini.

Msimu wa maembe Sikonge yanaoza tu kumbe China ni mali. Kilimo cha Pilipili kwa kiangazi huku Sikonge, watu wangeliweza kujivunia kilo kibao ila wanakaa tu wanakunywa kahawa....... ahhh, wengine hata kahawa hawana ila kusubiri tu Bibie apike ugali kwa Nswalu (Lami) na jamaa anauchapa huku akisubiri jioni akapate Wanzuki.......

Ninaamini Mbunge/Wabunge watalifanyia kazi hili swala.

Asiishie tu kwenye Pamba ambapo yeye ana kiwanda. Iende zaidi hadi kuwasaidia vijana wawe na mashamba yao na viwanda vyao vidogovidogo au mashamba yao kuzalisha bidhaa hizo tumewekewa juu......

MUBI: Asante sana kwa shule hiyo hapo juu....
Karibu sana, natumaini wanatucopy na kutuelewa nasi tuombe Mungu waweze kuyafanyia kazi. Muhimu aende kwenye vyuo akafanye interview kwa vijana kufuatana na fani zao ili waweze kufundisha na kusimamia wanavijiji katika uzalishaji wa mazao hayo ya zero tarriff, in this case vijana wanaomaliza watajipatia ajira na ukilinganisha wanakijiji watakuwa wanaingiza USD, na iwe vyema serikali iwe inawarudishia VAT baada ya kuwa yamenunuliwa huko China.Yaani uwepo motisha kuwa ukiuza frozen chicken toes Uchina ile VAT uliyolipa unarejeshewa baada ya USD kuingia kwenye bank account yako...Sisi Afrika hatuli miguu ya kuku, lakini China inauzwa USd 8.5 nusu kilo iliyokaangwa, frozen ni USD 5.7. Kazi kwetu tulale , tulumbane wenzetu wanasonga mbele tu, Heri Wakenya wanauza sana nimeona maccadamia nuts ya Arusha wanayapeleka China ndugu zetu Wakenya , sisi tuko kwenye siasa za malumbani hakuna Action. Let us do something tutoke kwenye tembe engalau basi tuwe mahala pengine safi.
 
Mimi sitii kambi yoyote katika hizo kambi zenu. Mimi nafanya kazi ya wananchi kwa kadri ninavyoona inafaa! Na kama kuna jambo lina maslahi ya chama, nitalitekeleza kulinda na kujenga chama changu, period!

Kuhusu hoja zangu; ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi na ile ya makazi kutumia dhamana ya hazina za wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii, nilishasema kuwa nitashirikiana na wabunge wenzangu ili kuijenga nchi yetu. Kwangu mimi haijalishi kama nitajulikana kwa sababu ya ajenda hizi ama vipi, mimi ninachofia hapa ni kuona tunafanikiwa kuleta mabadiliko tarajiwa kwa nchi yetu.

Kiongozi ni lazima utokane na watu na uwatumikie watu hao, hivyo ni lazima ufikie matarajio ya watu, na si vinginevyo hata mara moja!

Mmh Dokitori, umejieleza vizuri lakini nimeshindwa kuelewa hapo kwenye font nyekundu. Kuna mambo yanaweza kuwa na maslahi kwa chama chako lakini yasiwe na maslahi kwa wananchi waliokuchagua, sasa sina hakika kama hiyo itakaa na kueleweka kwa constituents wako. Kama isingekuwa msuli wa CHADEMA na matakwa ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba, basi tungeletewa kile wabunge wa CCM walikipigia kura kabla ya mabadiliko ya pili.

Naamini CCM ambacho ni chama chako kilikuwa na maslahi kupinga mabadiliko hayo. Sina hakika nasema tena, sina hakika kama Dokitori uko kwenye rekodi kupinga ule uzandiki ambao ulipitishwa na wabunge wengi wa CCM I guess na wewe ukiwemo. Huenda hiyo nayo inaweza ku-prove kuwa unafanya kazi ya wananchi kama uonavyo inakufaa wewe badala ya wananchi/ constituents wako. Unaposema unafanya kazi ya wananchi kwa kadri unavyoona inafaa; nafikiri ungerekebisha kidogo. Naamini kiongozi anatakiwa kufanya kazi ya wananchi inavyofaa wananchi wenyewe na si kiongozi.

Niko tayari kusahihishwa.
 
Mimi sitii kambi yoyote katika hizo kambi zenu. Mimi nafanya kazi ya wananchi kwa kadri ninavyoona inafaa! Na kama kuna jambo lina maslahi ya chama, nitalitekeleza kulinda na kujenga chama changu, period!

Kuhusu hoja zangu; ya ajira kwa vijana na kukuza uchumi na ile ya makazi kutumia dhamana ya hazina za wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii, nilishasema kuwa nitashirikiana na wabunge wenzangu ili kuijenga nchi yetu. Kwangu mimi haijalishi kama nitajulikana kwa sababu ya ajenda hizi ama vipi, mimi ninachofia hapa ni kuona tunafanikiwa kuleta mabadiliko tarajiwa kwa nchi yetu.

Kiongozi ni lazima utokane na watu na uwatumikie watu hao, hivyo ni lazima ufikie matarajio ya watu, na si vinginevyo hata mara moja!

peleka propaganda huko,tatizo lako hauna msimamo.ukipigwa biti na wabunge wenzako unafyata.cheki hawa ghasia alivyo kuchachafya kwenye kikao cha ndani siku ile pale dom.ulijua ubunge basi,tulikuonea huruma wewe kigwangala.sikutegemea pamoja na shule yako uliyonayo ufyate kwa yule mama ambae sizani kama anakufikia kwa shule. Wewe kigwangala ni mtu wa media tu.
 
Dr Hamis Kigwangalla wewe ni mbunge wa wapi? huna ofisi huko nzega acha kukimbilia mambo makubwa onyesha mfano huko kwako watu wana hali mbaya huko nzega ndio utaweza nchi nzima?
acha wivu wa kike... mbona kuna wabunge wengine wanaoongelea maslahi ya taifa. cha maana ni kumshauri tu jamaa aache ukinyonga!!! na hata hoja anazozunguka nazo sasa, si za kwake bali amedandi treni kwa mbele

hakuna tatizo mbunge kuongelea maslahi ya taifa kwa ujumla, ila kuna tatizo mbunge akiamua kubeba vya wenzake na kutungia beats ili kulazimisha hoja ziwe zake
 
Back
Top Bottom