Dr FERDINAND MASAU- NI NINI TUMEPOTEZA KAMA TAIFA

Fue Fue

Senior Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
107
Reaction score
128
Kwasasa Hayati Dr F Masau alikuwa daktari bingwa wa maswala ya moyo hasa upasuaji. Alianya masomo yake katika chuo kikuu kishiriki muhimbili, intern KCMC, halafu China kwa ajili ya elimu zaidi. Dr masau alikwenda Marekani TX kwa ajili ya fellowship na mafunzo zaidi jijini Houston TX na alifanya practise zake Texas Heart Insitutes (THI) ya jijini Houston ikiwa ni kati ya hospitali kubwa na maarufu za moyo ndani ya Texas Medical Center ambayo inabeba mkusanyiko mkubwa wa mohospitali maarufu duniani na kuwa kama kijiji kikubwa ndani ya jiji la houston. Texas medical center inaleta karibu kila taifa na watu wake kutibiwa jijini houston watu maaru, viongozi wa mataifa na wafanyabiashara kwa ajili ya matibabu.

Dr F Masau alikuwa akiandikwa sana kwenye journal za Texas Medical Center kama Dr anayekubalika sana ndani ya THI miaka ya 2000, 2001 wakati huo akiwa bado anapractice nao. THI na madaktari wenzeka kwa kukubali uwezo wake, uadilifu wake na mapenzi yake na nchi walikubali kumsaidia kuanzinisha kitengo cha moyo Tanzania.

Makatari wale walijitahidi kumkusanyia vifaa na kumwahidi wataalamu wa dharura kwa ajili ya kustabilize kitengo cha moyo. Nia yao kubwa ilikuwa ni kukiambatanisha kitengo cha moyo na Hospitali ya taifa Muhimbili. MNH wakakataa kwa shinikizo la wafanyabiashara wa kupeleaka wagonjwa nje nakumbuka wakati huo lion club pamoja na baadhi ya hospitali za binafsi.

Akajitahidi kwenda KCMC, Mikocheni Hospital, TMJ nk ila hospitali nyingi alikumbana na ugumu ama wa majengo, utawala au ubinafsi. Dr Masau akaweza kuongea na Dr Jaffar wa TMJ mikocheni akakubali kuwekeza pale kitengo chake hicho cha moyo.

Mmiliki wa TMJ alijua kuwa angeweza kumshawishi Dr akameza kile kitengo. Iliposhindikana alimfukuza Dr ndani ya Jengo. Nakumbuka tayari team wa wataalamu kutoka Texas Medical Center ilikuwa imefika tayari kwa kuanza kuhudumia wagonjwa wa kwanza ambao tayari walikuwa kwenye foleni. Sitakaa kusahau siku ile, vifaa vilifunguliwa kutoka theater usiku kucha na kurudishwa kwenye contena. Safari ya kukodisha jengo ikaanzia hapo.

Dr F Masau namwita mzalendo wa kweli, usiku mmoja nimekaa naye na wale madaktari kutoka Texas nakumbuka walimwambia utaratibu huku kwenu mgumu sana, mlolongo nimrefu mpaka ufanikiwe, kwanini usirudi Texas ukaendelea na kazi, Dr akawaambia hii ndiyo nchi yetu itanichukua hata miaka kumi kufanikiwa ila nitakuwa nimeacha sehemu ya kuanza hata kama nitakauwa sipo.

Taifa limepata hasara kubwa, taifa la vipofu na viziwi , taifa lisilojua maana ya wataalamu na utaalamu. Dr Masau alipata marafiki adimu sana kwenye taifa linalokuwa duniani ambapo kama tungelikuwa na viongozi wanaopenda afya zao, za ndugu zao na wajukuu zao kamwe wasingemgeuzia mgongo Dr Masau kwa tamaa ya kupeleka wananchi Appolo ili kupata cha juu.

Texas Heart Institutes ni kati ya hospitali zenye uzoefu wa muda mrefu sana maswala ya Moyo. Kwa ushirikiano na hiki kitengo, kwa kutumia THI-Tanzania tungeweza kuzalisha wataalamu wengi sana wa maradhi ya moyo kuanzia mabara, Nurse, dakatari, nk. Utaalamu na udhoefu huu ambao tungeupata kwa kufanya kazi, semina, mafunzo endelevu na kubadilishana utendaji. Tatizo nchi ilimwangalia mtu mmoja Dr Masau na kuwa na wivu naye. Isngekuwa rahisi kitengo kile kuendelea kama serikali haitoi msaada. Kitengo kama kile Texas serikali inakipata msaada mkubwa sana wa kifedha kutoka kwenye bajeti yake.

Nakumbuka niliwahi kumweleza wakati waziri mkuu Fredriki Sumayi jinsi wao na serikali yake wanavyomnyanyasa Dr Masau kuhusu kodi ya vifaa vile ambavyo yeye kapewa msaada nikamwuliza atatoa wapi fedha za kuvitoa wakati yeye anasaidiwa?? Nikamwambia sumayi wagonjwa ambao seriali yake inaweza kuwapeleaka Apollo ni wachache mno ikilinganishwa na wanaokufa bila hata kujulikana wanaumwa nini. Nikamwambia kusaidia watanzania wataalamu kuja hapa nchini na serikali kuwatambua kama nchi tutaokoa fedha nyingi sana za kuwapeleka nje. Mgonjwa mmoja kupeleka india fedha yake inaweza kutibu kumi hapa nyumbani. Wataalamu hawa wakipewa ushirikiano mzuri wakawezeshwa tutamaliza tatizo la afya in about 20 years.

Tanzania nchi pekee isiyothamini utaalamu wa mzawa , ujuzi wa mzawa, na uwajibikaji wa mzawa. Tunapenda na kuthamini vya kuja bila kujua huwa vinaondoka.

Tujenge utamaduni wa kuamini wataznania wanauwezo na wengi ni wazalendo wa kweli kwa nchi zao. Wapo wasomi wengi sana na wazuri nje ya tanzania ila hawako Tayari kurudi Tanzania kuleta utaalamu wao. Dr Masau angekuwa bolozi mzuri sana wa kushawishi cream ya nchi nje kuamini thamani yao ndani ya nchi yao.

Tusingekubali kuzima utaalamu wake kwa tamaa za posho za India.

Nitakukumbuka daima Dr F Masau.

[video=youtube_share;Ntr0Xo8yR4I]http://youtu.be/Ntr0Xo8yR4I[/video]

Mei 16, mwaka huu, saa 12:00 jioni, nilipata ujumbe wa neno moja kwenye simu yangu ya kiganjani ukisomeka, ‘amefariki'.

​Nilikuwa nikitokea kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Nikataharuki! Sikujua mara moja aliyefariki ni nani wala aliyenitumia ujumbe huo kwa kuwa namba hiyo haikuwa kwenye kumbukumbu nilizozihifadhi kwenye simu yangu.

Niliamua kupiga simu iliyotumika kunitumia ujumbe huo. Simu iliita na mara, sauti kutoka upande wa pili ikasema, ‘rafiki yako Dk. Masau!'

Nikamuuliza nini? Naye kumbe alikuwa ameshakata simu, alikuwa na sauti ya uchungu mkubwa na hakuweza kuongea zaidi

Hata hivyo, nilimfahamu kwa sauti yake, alikuwa ni Damas Magessa ni mtoto wa kaka wa Dk. Ferdinand Masau.

Nilijikuta nikijenga taswira ya fikra hii, kwamba ‘hakika nchi hii, wazalendo hawana maisha'.

Dk. Masau, ambaaye jina lake la ukoo ni Magessa, alipewa jina Masau kwa kuwa lilikuwa jina la babu yake.
Ninamfahamu tangu 1999, akiwa anafanya kazi nchini Marekani katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Texas (THI).

Hiyo ilikuwa ni baada ya kwenda kuongeza mafunzo zaidi pale Texas Medical University.

Mimi ni miongoni mwa wanahabari tuliofanya kazi naye katika hatua za mwanzo kabisa za uanzishwaji wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo hapa Tanzania.

Wakati ule nikiwa Mwandishi wa gazeti la kila siku la The Guardian, gazeti dada la NIPASHE.

Nilipata `tipu' kuwa TMJ wanapanga kuanzisha huduma ya upasuaji wa moyo hapa nchini, na kwa kuwa wakati huo tuliandika habari za wagonjwa kupelekwa nchini India kwa upasuaji wa moyo, nikaona ni habari ninayopaswa kuifuatilia kwa kina.

Nilikwenda TMJ nikaonana na Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Jafferj Mohammed Tayeb, katika mahojiano naye alisema ni kweli mwaka 2000 walipanga kuanzisha upasuaji wa moyo hapo hospitalini kwao lakini kwa kushirikiana na Watanzania wanaofanyakazi hiyo Marekani.

Niliona ni ndoto, nikaomba mawasiliano yao kwa maana ya namba za simu ili wanithibitishie, hakunipa namba bali alinipa anuani ya barua pepe ya Dk. Masau.

Nikamwandikia na kujitambulisha kwake sambamba na kuujua ukweli wa habari ya uanzishwaji wa upasuaji wa moyo hapa nchini.

Dk. Masau akanijibu maswali yangu. Nikaandika habari kwa mara ya kwanza kwenye The Guardian ya kuanzishwa kwa upasuaji wa moyo hapa nchini.

Dk. Masau alifikia uamuzi wa kuanzisha Tanzania Heart Institute (THI) ambayo ilipata usajili kwa mara ya kwanza nchini Marekani na kuamua kutaka kufanya kazi na TMJ, baada ya kuishauri Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa takribani miaka mitano bila mafanikio.

Dk. Masau alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Muhimbili mwishoni mwa miaka ya 80, alipata mafunzo ya uzamili kwenye fani ya upasuaji wa moyo katika Chuo Kikuu cha Hubei nchini Uchina.

Mwaka 1994, ndoto yake ilikuwa ni kuanzisha idara ya upasuaji wa moyo ndani ya Muhimbili na mradi wake ulihusu uanzishwaji wa upasuaji wa moyo nchini Tanzania, ndani ya Muhimbili.

Kwa maelezo yake kwangu , serikali ya China (wakati huo) ilikubali kusaidia uanzishwaji wa idara hiyo, lakini aliporejea nchini wazo lake hilo lilikataliwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, Profesa Maselle.

Ndipo alipoomba nafasi ya masomo zaidi nchini Marekani baada ya kupata tangazo la nafasi hiyo ya masomo ya fellowship.

Mwaka 1996, alipata mafunzo chini ya Profesa Denton Cooley, mwanzilishi na Mpasuaji Mkuu katika taasisi ya magonjwa ya moyo ya Texas.

Profesa Cooley na wenzake ndiyo waliofanya upandikizaji wa moyo kwa mara ya kwanza nchini Marekani.

Dk. Cooley aliiandikia serikali ya Tanzania, juu ya kuwapo kwa Dk. Masau anayefanya fellowship katika eneo la upasuaji wa moyo hapo Texas na haja ya kumuunga mkono.

Wakati huo Waziri wa Afya alikuwa Dk. Aron Chiduo (marehemu), lakini Dk. Cooley hakujibiwa.
Ndipo mwaka 1999, Dk. Masau aliamua kusajili Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Tanzania (THI) akiwa huko Marekani.

THI baada ya kusajiliwa nchini Marekani, serikali ya Marekani iliipatia msamaha wa kodi mara moja, hivyo wakaanza kukusanya vifaa vya upasuaji na vifaa vingine vya tiba.

Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa, alikuwa anafanya ziara nchini Marekani, hivyo Dk. Masau kwa kushirikiana na Profesa Cooley, walimwandikia Rais kumwomba kuitembelea THI.

Barua hiyo haikuwahi kujibiwa, na hata jitihada za kupitia kwa Balozi David Mokawago (wakati huo) hazikuzaa matunda.

Ndipo Dk. Masau alirejea nyumbani na kuona namna ya kuunganisha nguvu na baadhi ya hospitali za ndani.

Alifanya mazungumzo na hospitali ya Tumaini, Kairuki na TMJ. Ni TMJ pekee iliyomkubalia kufanya kazi naye.

Mwaka 2000, Dk. Masau alirejea rasmi nchini kuanza uanzishwaji wa taasisi hiyo kwa kushirikiana na TMJ. Hapo ndipo vita ya ana kwa ana ilipoaanza rasmi.

Wakati huo niliacha kazi ya uandishi wa habari nikaajiriwa na THI kama Afisa Uhusiano wa kwanza, ikiwa ni Novemba mwaka 2000.

Vita ya kwanza ilikuwa ya kutoa vita vya upasuaji wa moyo bandarini, vifaa hivyo vilikuwa vimefutiwa kodi zote.

Hapo, hoja ilikuwa kama kweli THI ni shirika lisilo la kiserikali kwanini ishirikiane na TMJ ambayo ni hospitali binafsi?

Maswali haya yalikuwa ni ya msingi na kwamba serikali isingeweza kutoa msamaha wa kodi kwa `staili' ile.

Tulikaa chini tukawashawishi haikuwezekana, ikatubidi kutafuta jengo letu wenyewe na baadaye tukapewa msahama wa kodi.

Dk. Masau alikuwa si mtu wa kukata tamaa, ingawa wakati huo kazi kubwa ilikuwa kupata vibali vya kufanya upasuaji wa moyo hapa nchini.
Ikagundulika kuwa hakuna miongozo ya kutoa kibali kwa hospitali maalumu kama hiyo, kwa hiyo harakati zote zikakwama, ilituvunja moyo sana, Dk. Masau akaonekana kama anakata tamaa, lakini unamwona kabisa anajikaza ili mambo yaende.

Tulikuwa tunasubiri vibali vya serikali tuanze kazi Dk. Masau aliteua baadhi yetu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo zaidi yanayohusu tasnia ya tiba kwenye upasuaji wa moyo.

Kwa kuwa tayari kulikuwa na programu zilizokubaliwa kuwaendeleza wataalamu wazalendo katika nyanja zote za tiba ya moyo.

Dk. Masau alikuwa ni mtu wa kujishughulisha kusoma muda mrefu, hivyo alikuwa anawahimiza wafanyakazi wa taasisi kujitafutia elimu kila wanapopata nafasi.

Mwaka 2001, nilipewa kazi maalumu ya kuhakikisha THI inapata kibali cha usajili. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Mama Anna Abdallah aliteuliwa kuwa Waziri mpya wa Afya.

Nikakutana na Mama Anna akanisikiliza, akaahidi kushughulikia suala la kibali hicho.

Kweli baada ya muda mfupi kulifanyika mabadiliko madogo wizarani, Msajili wa hospitali binafsi aliondolewa na kuteuliwa daktari mmoja aliyejulikana kwa jina la Dkt Mng'ong'o.

Baada ya wiki moja, nilikabidhiwa kibali cha kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo.

Nilipofika ofisini nilikuta Dk. Masau anamgeni, sikusubiri itifaki niliingia moja kwa moja ofisini kwake nikiwa nimeficha ile bahasha mgongoni.

Nikamwomba samahani kwa kuingia bila utaratibu, akasema haina shida, nikamuuliza, Dk. hebu buni nimebeba kitu gani?

Akacheka na kusema kwa kweli sina wazo lolote! Nikamwambia cheti cha usajili wa Taasisi ya magonjwa ya moyo nimekileta hiki hapa!

Dk. Masau alinyanyuka huku machozi yakimtoka na kupiga magoti akamshukuru Mungu, baadaye alinyanyuka na kunipa mkono. Hapo THI ikaanza kazi zake rasmi.

Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala, maana yake. Mungu aiweke mahala pema Roho ya Dk. Ferdinand Masau.
 
kifo cha Dk.Masau kinasikitisha unaweza kulia.
 
Inasikitisha sana. Katika hali tuliyofikia, haitatosha kubadilisha viongozi. Itabidi kubadili MFUMO wa uongozi.

Hatuna budi kubadilisha katiba na taasisi muhimu za mfumo wa serikali.

Mwaka 1964 Mwalimu aliunda upya jeshi, na ili kuhakikisha ni jipya kweli akalibadilisha hata jina.

Itabidi kuanza jeshi la polisi upya na hata Idara ya Usalama wa Taifa itabidi iundwe upya, na taasisi hizo zifanye kazi kwa kufuata katiba mpya na ziwe huru.

Majina na idadi za wizara vitabidi viwe kwenye katiba.

Idara muhimu kama jeshi na polisi zitapashwa ziwe huru na viongozi wake wapitishwe na bunge.

Tunachoona hapa kwa Dr Masau ni matokeo ya ugonjwa, sio hasa ugonjwa wenyewe. Itabidi tutibu ugonjwa.

We can summarize the governmental situation in Tanzania as follows: It's broken, it can't be mended, it must be changed.

RIP Dr Masau.
 
Guys,
Nimeisoma hii habari na imeniuma sana yan sana mana kuna dada mmoja was wrkn as mapokez pale na alikua anantel dat hosptal imesaidia watu weng yan weng walikua ni wale tabaka la kutoweza kwenda India ila walifanikiwa kupata tiba,feel sorry for Tanzania and mafisadi wasioipenda hii nchi na hata Sumaye cku hizi anajiweka kua mtu mzuri yl ni mtu alekua mchafu ,yan hate this country
 
Hii habari itupe ujasiri wa kuitoa ccm kwenye uso wa tanzania na dunia,2015 hawarudi kamwe.
 
Hongera Mama Anna Abdallah na Dr. Mng'ong'o! Hakika mnastahili pongezi katika jambo mlilolifanya......Maruhum Dr. Fed hakuwa na cha kuwalipa, lakini mtalipwa na M/Mungu.

Afisa uhusiano wa THI (wa zamani) umeeleza vizuri sana mchakato mzima wa THI kusimama mpaka kupata kibali cha kufanya upasuaji. Je, upasuaji huo mlifanyia chini ya mti? katika makala yako ujaeleza, tungependa kujua mchakato mzima wa majengo ulikuaje (mkataba) na mpaka kufilisiwa kama bado ulikuwepo kazini au ulishamkimbia tayari?
 
Back
Top Bottom