Dr. Eve Hawa Sinare atangaza Kuhama CCM

Dr. Eve Hawa Sinare atangaza Kuhama CCM

amilyroley

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
621
Reaction score
1,200
Akiongea na waandishi wa habari jioni hii kada wa muda mrefu mpanga Sera na mikakati wa CCM na mshauri wa chama Dr Eve Hawa Sinare ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na UKAWA.

Huyu ni mtu muhimu sana kwa CCM na msomi aliyekuwa anashauri mikakati ya ushindi kwa Jakaya Kikwete katika chaguzi zilizopita.

===========================

MMGM2455.jpg

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Dk. Sinare amesema amefikia uamuzi huo kutokana na CCM kushindwa kutatua matatizo ya vijana na umaskini kwa kutoa huduma bora ya afya, elimu, maji na umeme hata wakishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Dk. Sinare alitangaza hayo juzi jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari.

"Kuanzia leo (juzi, nimejitoa CCM," akisisitiza huku akisema licha ya kujitoa katika chama hicho tawala, bado hajaamua kujiunga na chama kingine chochote cha siasa.

Hata hivyo, Dk. Sinare alisema anaunga mkono mabadiliko ya kweli ndani ya nchi.

Uamuzi wa Dk. Sinare kujitoa CCM unakuja siku chache baada ya aliyekuwa kada wa chama hicho, Balozi Juma Mwapachu, kutangaza kujiengua katika chama hicho na akitanguliwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyetangaza kujitoa CCM, Oktoba 4, mwaka huu.

Dk. Sinare ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kahawa, Mwenyekiti wa kuchunguza matatizo ya vyuo vikuu na Mjumbe wa Bodi ya Mashirika ya Umma ambaye hivi sasa ni Wakili wa kujitegemea, alisema kwa miaka 53 madarakani, elimu nchini ni duni huku viongozi wakichukulia uongozi ni ajira ya kujitajirisha kuliko kuangalia matatizo ya Watanzania.

Alisema kuwa hivi sasa vijana wengi hawana ajira zenye tija wakati viongozi wanajilimbikizia mali na kujilipa mamilioni ya fedha kwenda kuhonga na kununua kura kila inapofika kipindi cha uchaguzi.

Dk. Sinare alisema Serikali ya CCM imewakosea wananchi, kwani kwa miaka yote ilipokuwa madarakani, huduma za afya zimekuwa duni huku viongozi bila woga wakisafiri kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu ya gharama kubwa na hospitali zikikosa dawa.

Alisema huo ni mfumo mbaya uliowekwa na CCM kuwanufaisha viongozi huku wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma bora na uongozi kutoka kwao.

Aliongeza kuwa vyombo vya usalama, Polisi na muundo mzima wa serikali pamoja na mashirika ya umma, yamekuwa yakitumika kukampenia chama tawala.

Aidha, alisema chini ya uongozi wa CCM, kila Mbunge hulipwa mafao makubwa na yasiyo na ulazima pindi Bunge linapovunjwa.

Alisisitiza kuwa mambo yote mabaya yaliyofanywa na CCM na kuifanya nchi kuwa katika hali mbaya, yanahitajika mabadiliko ili kuokoa ufujaji wa fedha za umma ziende kuwahudumia Watanzania.

Chanzo:
NIPASHE

Kwani mburula wa CCM na Masaki walioelekezwa shingo kibla wanajifahamu ? Sana sana wanabubujika vijembe toka wenye chama hadi waishio kwa ruzuku ya chama
 
Mwandosya hawezi kuhama kwa kuwa anajua wazi hata kama akihama hana chake mbele ya KLM Elite ni bora hata CCM watampeleka kumtibu India, huko UKAWA ni KLM tu si unasikia majina yenyewe Sinare huyo ni KLM elite moja kwa moja!

Kingunge, Mwapachu nk watoka sehemu gani Tz? Poleni wakabila lakini mwisho wenu 2015
 
Mwandosya hawezi kuhama kwa kuwa anajua wazi hata kama akihama hana chake mbele ya KLM Elite ni bora hata CCM watampeleka kumtibu India, huko UKAWA ni KLM tu si unasikia majina yenyewe Sinare huyo ni KLM elite moja kwa moja!

haa haa kuwagawa watu kikabila ni kazi ya ccm. nimeshuhudia maghufuli akinadi kwa kisukuma ili kujaribu kupata kura za kabila lake. ni hatar sana..
 
Akiongea na waandishi wa habari jioni hii kada wa muda mrefu mpanga Sera na mikakati wa CCM na mshauri wa chama Dr Eve Hawa Sinare ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Ukawa. Huyu ni mtu muhimu sana kwa CCM na msomi aliyekuwa anashauri mikakati ya ushindi kwa JK katika chaguzi zilizopita.

Sinare huyo ni moja kwa moja mtu wa KLM elite sasa cha ajabu nini si anaungana na akina Kishimba, Nkya, Mbatia &CO.!

Yeye ni sawa kwa maana siyo msukule, shida inabakia kwenu manyumbu wa kutoka Mbeya, Iringa sijui Mwanza au Geita mnashabikia ukawa huko ninyi mnatumiwa kama misukule tu ya kuandamana kupigwa na Polisi lkn cheo ndani ya UKAWA sahauni!
 
Je, huyu ni nani kwenye siasa tulizo nazo...?
Je, aliisha wahi hata kugombea udiwani tu au serikali ya mtaa wake...?
ili walau tumpime kama ana ushawishi (Orator) au mnatuletea watu
kwa tittle za darasani mkidhani watafua dafu kwenye siasa za kibongo...?
 
Sinare huyo ni moja kwa moja mtu wa KLM elite sasa cha ajabu nini si anaungana na akina Kishimba, Nkya, Mbatia &CO.!

Yeye ni sawa kwa maana siyo msukule, shida inabakia kwenu manyumbu wa kutoka Mbeya, Iringa sijui Mwanza au Geita mnashabikia ukawa huko ninyi mnatumiwa kama misukule tu ya kuandamana kupigwa na Polisi lkn cheo ndani ya UKAWA sahauni!

UKABILA HAUTAISAIDIA C.C.M KUBAKI MADARAKANI...
Wewe na wana c.c.m wenzio mtalaaniwa na ukabila wenu...!
 
Back
Top Bottom