Dr. David Livingstone na Henry Morton Stanley Ujiji na Blantyre 1871

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,029
2,000
1549570119615.png
NA
1549570357646.png

Sanamu ya Dr. David Livingstone

Hii picha ya kuchora hapo ni Ujiji inaonyesha Dr. David Livingstone alipokutana na Henry Morton Stanley tarehe 10 November, 1871.

Karibu ya Glasgow kuna kijiji kinaitwa Blantyre hapa ndipo alipozaliwa Dr. Livingstone na kijiji kizima kimefanywa ni makumbusho yake kwa jina la Dr. David Livingstone Memorial.

Nimebahatika kufika hapo na nilipiga picha chache za kumbukumbu.

Leo nilipoona hiyo picha ya Livingstone na Stanley ikawa nimekumbuka Makumbusho ya Livingstone.

Nimefika Soko la Watumwa Mikindani ambako David Livingdtone alipata kusimama pembeni ya soko akiangalia watumwa wakinadiwa lakini katika soko hilo hakuna kumbukumbu yoyote ya kihistoria.

Picha ya mwisho ni Ujiji Livingstone akiagana na Stanley.
Picha hizi nimepiga hapo Blantyre Jumanne, May 21, 1991.

1549571678256.png
 

Attachments

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,290
2,000
Sheikh shukran kwa kumbukizi na picha zenye kufikirisha.
Sisi hatujui kutunza historia zaidi ya kuzibomoa ninaamini miaka 20 ijayo Kariakoo na Posta ya zamani patapoteza kabisa historia ya mji wa zamani kama hatutajitafakari
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom