Dr. Dalaly Kafumu: Kusema ukweli uamuzi wa Rais katika suala la mchanga utaligharimu taifa baadae

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Mhe.Dr.Dalaly Kafumu (Mbunge wa Igunga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Viwanda na Biashara) ametoa maelezo yafuatayo kuhusu agizo la kuzuia kusafirisha mchanga nje ya nchi;
______________________________________________

Suala la kuhakikisha Tanzania inachenjua madini yote hapa nchini; Mhe Rais yuko sawa kwani ni la kisera; Sera ya Madini ya mwaka 2009 (niliyosimamia utengenezaji wake); kifungu 5.11; policy statement no. 3 inasema hivi: (iii) The Government will collaborate with the private sector, regional and international organisations to strategically invest in smelting and refining.

Kwahiyo mchakato wa kuchenjua mchanga hapa nchini ni matakwa ya kisera lakini shida inakuja tu pale ambapo shughuli hii inaanzishwa kwa haraka na dharura kubwa. Hali hiyo inaweza kuleta uhusiano usio sawa na makampuni ya kimataofa na hata nchi makampuni yanakotoka.

Pia maamuzi haya ya haraka yatatupotezea mapato kama wengine walivyosema. Nia njema na nzuri ya Mhe.Rais ni lazima iendelezwe kwa kumshauri tena Mhe.Rais aangalie namna bora zaidi ya kufikia malengo haya mazuri ya Sera ya Madini ya mwaka 2009.

Washauri wa Mhe Rais - wizara yenye dhamana, tafadhali ni wajibu wenu; na jukumu lenu kumsaidia Mhe Rais juu ya hili jambo jema lenye manufa kwa Taifa letu.

Dr.Dalaly Kafumu
____________________

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Dr.Kafumu ni mtaalamu aliyebobea wa madini. Kwa wale wasiomfahamu vizuri ana shahada ya madini na elimu miamba (B.Sc in Geology) kutoka chuo kikuu UDSM. Ana Stashahada ya juu ya elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Chuo Kikuu UDSM.

Pia ana Stashahada ya Juu ya Uchakataji Madidi (Postgraduate Diploma in Mineral Exploration) kutoka Institute of Aerospace Science, Uholanzi. Ana Shahada ya Uzamili ya madini na elimu miamba (M.Sc in Geology) kutoka Chuo kikuu cha Brussels, Ubeligiji. Na Shahada ya Uzamivu ya madini na elimu miamba (PhD in Geology) kutoka Chuo kikuu cha Brussels, Ubeligiji.

Nimeamua kueleza historia fupi ya elimu ya Dr.Kafupi ili tujue kwamba ni MTAALAMU ALIYEBOBEA kwenye masuala ya madini. Ushauri wake ni ushauri wa kitaalamu na si wa kupuuzwa. Kama JPM anataka kuisidia nchi yetu afanyie kazi ushauri wa Dr.Kafumu.

Kwa lugha rahisi Dr.Kafumu anasema suala la kuchakata mchanga wa madini nchini ni la kisera. Sera ya madini ya mwaka 2009 inaelekeza mchanga unaobaki uchakatwe nchini badala ya kusafirishwa nje. Lakini Dr.Kafumu anashauri kuwa ni vema kuwe na utaratibu mzuri wa kufaniksha jambo hili badala ya "kukurupuka".

"Kukurupuka" kunaweza kuliingiza taifa kwenye hasara. Kwa mfano taarifa ya mgodi wa Geita inaeleza kuwa wanapata hasara ya dola milioni 1 kila siku (zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania) kutokana na mchanga huo kuzuiwa kwenda nje. Pia Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe amesema hadi sasa nchi imeingia hasara ya Trilioni 1.3 kutokana na maamuzi ya kuzuia mchanga huo kusafirishwa.

Sasa unaweza kujiuliza kama kwa siku mbili tumepata hasara ya trilioni 1, mchanga huo ukiendelea kukaa bandarini kwa muda mrefu zaidi ni hasara kiasi gani. Kadri mchanga unavyoendelea kukaa ndivyo hasara inaongezeka zaidi. Je nani atalipa hasara hii?

On other hand, migodi kadhaa imetangaza kusimamisha ajira kwa wazawa baada ya mchanga huo kuzuiwa bandarini. Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya kazi za kuchimba mchanga huo, kupembua, hadi kusafirisha zinafanywa na wafanyakazi wazawa. Tayari mgodi mmoja umewafuta kazi wafanyakazi zaidi ya 80 jana kufuatia kadhia hiyo.

Lakini swali la msingi sana tunalopaswa kujiuliza ni je tuna uwezo wa kuchakata mchanga huo ili kupata madini? Inaelezwa kwamba 20% ya vipande vya madini hubaki kwenye mchanga huo. Lakini je tuna uwezo wa kuchakata udongo ili kupata madini hayo?

Mfanyabiashara Zacharia Hans Pope anasema dunia nzima kuna vinu vinne tu vya kuchakata udongo ili kuexcute madini yaliyopo. Hans Popa anasema gharama za kutengeneza kinu kimoja ni karibu bajeti yetu ya mwaka mzima. Yani mwaka mzima tusile, tusivae, tusinywe, tusilipe mishahara, tusiuze, tsinunue, tusizalishe chochote.

Uchumi wa nchi usimame ndipo tuweze kutengeneza angalau kinu kimoja cha kuchenjua udongo utakana na madini. Hans Pope anasema hata tukiweza kujenga kinu hicho, bado hatuwezi kukiendesha. Tunahitaji umeme mkubwa sana ili kuendesha kinu hicho. Tunahjtai angalau nusu ya umeme wote tunaotumia kwa sasa ili kuendesha kinu kimoja.

Kama taarifa hiyo ya Hans Pope ni kweli, maana yake ni kwamba hata tukizuia udongo huo kwenda nje, bado hatuwezi kuchakata udongo huo hapa nchini. Sasa kwanini tunazuia udongo kusafirishwa nje wakati hatuna uwezo wa kuuchakata?

Yani huu wivu wa kuzuia kitu ambacho hatuwezi kukutumia kwa manufaa umetoka wapi? Mbona ni wivu wa ajabu sana? Kuna kisa cha "choyo cha mbwa kwa majani ya ng'ombe." Yani mbwa anapomfukuza ng'ombe asile majani wakati yeye hawezi kuyala. Nadhani kuna haja ya kutafakati upya suala hili.

Vinginevyo tutabaki na mchanga ambao hatuwezi kuufanyia chochote, huku tukiingiza taifa hasara. Mwisho wa siku mchanga utazuia nafasi bandarini na kuzuia mizigo inayoingia kukosa nafasi na kuipelekea bandari kavu ambako ni gharama zaidi. Yani hasara mara dufu.

Hata hivyo naungana na ndugu Exaud Mshana kwamba badala ya kukimbizana na huo mchanga (concentrate) wenye 20% gold tungejikita kwenye 80% extracted gold ili value addition yake ifanyike hapa kwetu. Haya ya kuzuia vifusi vya mchanga wakati hatuna uwezo wa kuextract ni kujilisha upepo. Tuache ubabe usio na manufaa.!

Malisa GJ
 
inamaanisha Baba wa Taifa alipozuia uchimbaji wa madini alikuwa na wivu?
Naona baada ya kupata mgao wao wanaanza kulialia tena. Hawa kina Kafum, zito ndio wametufikisha hapa huko nyuma wakati wanapokea mgao toka kwenye makampuni walikuwa kimyaa kama binti anayetolewa mahari.
 
Kama walifanya Environmental impact assesment vizuri kabla ya kuchimba na kusafirisha haya maconcentrate sina shida kwani ndo uko niliko bobea .Huku kwingine m sihusiki mtajua wenyewe
Kila mtu ajiridhishe kwenye professional yake ndo atoea ushauri
 
Ila wanasiasa wanatufanya mapoyoyo sana..hivi unaposema nchi imepata hasara ya trillion moja na point ndani ya wiki..hivi hizo hela huwa zinaingia kwenye mfuko wa nani?? Mbona makusanyo yetu kwa mwezi kodi sehemu zote za huduma ndio huwa tunafikia hicho kiwango au mi sijamuelewa zitto..ndio maana magu amewazuia hawa wanasiasa kuongea kuongea..he knows them well
 
Back
Top Bottom