Unaweza kaba koo taasisi kubwa za kidini zenye hadhi kubwa kama TEC na CCT? Pigana vita kote usisigee hizo taasisi kama CHADEMA inataka ipigwe chini nzima nzima uchaguzi 2015 pamoja na huyo Tundu Lisu isogeze vita zake kwenye hizo taasisi.Hizo taasisi ni moto wa kuotea mbali hasa kwa wanasiasa uchwara.
Huyo Padre katima na huyo mwingine wa CCT ni watu wadogo sana CCT na TEC hata kama waliiiona list ya wajumbe walioteuliwa katika hatua za awali haikuwa ndio fainal viongozi wa juu ambao ni maaskofu walikuwa na uwezo wa kuweka majina mengine tofauti na hilo la DR.katima na mwenzie yaliyopendekezwa bila kuwajibika kurudisha feedback kwa huyo Dr.KATIMA kwa kuwa kwa mfumo wao hawajibiki kwa junior.
Sasa kama huko mbele kwa mbele hakuona jina lake mtu wa kumwuuliza sio Tundu Lisu na hiyo kamati au Raisi .Na Chadema WAJIFUNZE Kuwasiliana na wakubwa wa taasisi za kidini kama raisi anavyofanya wakiiga staili hii ya tundu lissu ya kuwasiliana na kuchukulia serious hoja ya mtu mdogo wameisha.Raisi alichosema ni sahihi anajua alikopata majina.
Pole Tundu lISSU ULIYEPATA majina kwa DR.katima.
Tusihukumu bila ushahidi.
Je, ikithibitika Jk ndio muongo,mnafiki na mzandiki utasema nini?
Kwanini watu hamuhoji ukimya wa hizi Taasisi?
Nasi tusiwe wanafiki!
TEC huwa hawatoi matamko ya hovyo hovyo kujibizana na wanasiasa
Jiulize kwanini Tundu hajagusia kiini cha kuitwa muongo alipoitisha "press"?
Dr.Kitima ni miongoni mwa watu ambao mara kwa mara huwa anaalikwa Star tv katika vipindi mbalimbali na niseme ukweli tu huwa navutiwa sana na michango na kauli zake kwenye vipindi anavyoalikwa na kwakweli siku zote huwa anakuwa "outspoken".Mara nyingi anakuwa ni mtu wa kuikosoa serikali bila woga wala hofu,naamini wale ambao huwa mnamfuatilia katika luninga mtakubaliana nami.
Lakini ninachoshangaa ni kwanini mpaka leo yuko kimya juu ya sakata hili la Kikwete na Tundu Lissu kuhusu uteuzi wa mjumbe wa TEC kwenye tume ya katiba.Dr.Kitima ndie alietajwa na mh.Lissu kuwa aliiambia kamati ya bunge ya katiba,sheria na utawala kuwa mtu alieteuliwa na Raisi kuingia katika tume hiyo hakupendekezwa na TEC.
Sasa Dr. unashindwa nini kusema hadharani juu ya hili?
Hata hivyo,inawezekana hawezi kuongea bila idhini ya TEC kuhusu jambo hii.
Itakuwa ni jambo la ajabu Taasisi ya kidini kushindwa kusema ukweli au kuficha ukweli.
Watanzania tuachane na Jk na Lissu na badala yake tuzikabe koo hizi Taasisi.Haiingii akilini kuwajadili Tundu Lissu na Kikwete bila kuhoji ukimya wa hizi Taasisi.
Kitu kingine cha kujiuliza ni mbona hawakuhoji uteuzi wa wajumbe hao mara baada ya majina ya wajumbe wa katiba mpya kutangazwa??!!
Wee hujui kitu,unamjua Kitima?au unafurahi kumuona akiendesha harakati?Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuandika kipuuzi kama ulivyoandika hapo! Hivi wewe unamfikia dk Kitima hata kwa punje? Je unamfikia Lissu hata kwa nukta? Acha ushabiki wa akili za juha... Ukweli utakuweka huru.. Acha kuwa -----...
Kamaliza kazi yake ya VC chuo kikuu SAUT Mwanza kapewa post mpya Morogoro.
sasa nakutukana kama lusinde kule bungeni tayari nimekutukana.
Tundu muongo, mnafik, mzandik.
...hahahaaa kweli kamanda lisu kawashika pabaya,mmeambiwa,mmesikia,mnadhani,labda,huenda,nahisi...
Bila shaka mnafurahia ukimya huu ili mtu wenu asiumbuke!
Hakuna siri chini ya jua!
Ni swala la muda tu kabla hatujamjua ni nani mnafiki,muongo na mzandiki.
Tundu muongo, mnafik, mzandik.
"Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."
"... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu."
TEC hawajawahi kifanya kazi kwa shinikizo la jf wala CDM,CCM,CUF na yeyote yule wakiona inafaa watatoa tamko au unawesa pia ukamshauri pia Lissu akaenda ofisi za akatuletee huo ushahidi