Dr. Ayub Rioba na Uchochezi

nyumbatatu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,076
938
Huyu ni Dr Ayub Rioba

Makala hii iliandikwa mnamo mwezi March Mwaka 2011 na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha UDSM kwenye gazeti la Raia Mwema, hivyo nimeona tujikumbushe.

Katika dunia tunayoifahamu vema, hakuna njia ya mkato katika kufikia amani ya kweli. Amani ya kweli haitazamwi katika 'utulivu' unaokuwapo katika nchi.

Tunisia ilikuwa na utulivu. Misri ilikuwa na utulivu. Libya ilikuwa na utulivu. Lakini nchi zile hazikuwa na amani ya kweli. Waliosema ukweli katika nchi zile waliitwa wachochezi. Wengine walipotezwa. Wapo walioteswa sana na damu zao ndizo zinazowatesa watawala wale jeuri ambao walilazimishwa na umma kukimbia madaraka bila kupenda.

Na hakuna kitu hatari kama huu utulivu ambao watawala huusisitiza kila wakati kwa wananchi wao. Utulivu si sifa. In kitu hatari kuliko hata silaha za maangamizi.

Kwanza katika historia ya dunia yetu, hakuna kokote ambako utulivu ulileta maendeleo kwa binadamu zaidi tu ya kuwafanya waishi kama jana na kama juzi. Utulivu hauwezi kufananishwa na ubunifu. Utulivu hauleti mabadiliko. Utulivu ni ubwege. Ni uzubaifu. Utulivu ni kufubaa. Ni uzezeta.

Hakuna kitu ambacho wananchi wa Bara letu wanapaswa kukiepuka kama kujengewa fikra kwamba ubwege ni tunu. Kwamba ukondoo wa kuinamisha kichwa na kukubali lolote likupate bila kujifaragua ni sifa. Utulivu si hulka ya binadamu.

Endapo utulivu ungekuwa ni asili ya binadamu basi Leo hii bado tungekuwa tunaishi juu ya miti. Na huenda tungekuwa pia tunashindana na simba kule porini kuwinda kwa kutumia mikono yetu.

Kinyume cha utulivu ni uchochezi. Nchi nyingi za Afrika zilirithi sheria nyingi tu za wakoloni. Moja ya sheria hizo ni ile inayozuia uchochezi. Wakoloni walikuja kutawala bila ridhaa ya Waafrika. Ushahidi unaonyesha kuwa wakoloni hawakuwachulia Waswahili wetu kama binadamu waliokamilika. Kwa hiyo hawakuona hata maana au umuhimu wa kuwashirikisha katika kupanga mambo mbalimbali ya maendeleo.

Wao (wakoloni) walijua wana akili nyingi kupita Waswahili wetu na hivyo wakaamini walipaswa kutawala kwa nguvu za fikra na silaha zao.

Walipoona wenyeji (natives) wanaanza kuhoji au kupinga mambo ya watawala au kugoma, wakatunga sheria kali zaidi, ikiwemo ya uchochezi.

Uchochezi si kosa la mwenyeji wa Afrika dhidi ya serikali alioyoiridhia yeye iwe madarakani. Na wala uchochezi si kosa la raia wa nchi ya mkoloni dhidi ya serikali yake. Uchochezi ni kosa lililotengenezwa mahsusi na mkoloni kwa ajili ya kumfanya mwenyeji awe mtulivu. Atulie kama maji ya mtungi au kama ananyolewa.

Kwa hiyo wakoloni walitaka kuwepo na amani na utulivu ili waweze kutunyoa vizuri. Walitaka tuwe watulivu ili wapate fursa ya kutunyonya bila bugdha yoyote. Walitishika sana na uchochezi wa aina yoyote uliolenga kuwaamsha watulivu wetu kudai ukombozi wa kweli na kuvuruga mirija yao waliyokuwa wameitandaza kila kona kwa ajili ya kunyonya utajiri wa Bara letu.

Wakoloni wetu wale wale walitambua kuwa utulivu ilikuwa sifa ya majuha. Vizazi vyao vilikwisha kupitia katika utamaduni wa watawala kutaka kila mwananchi awe mtulivu. Wakajifunza kwamba utulivu wao ulikuwa ni mtaji tu wa watawala . Wao , kama wananchi hawakunufaika na lolote.

Walijua kuwa katika historia, wachochezi wengi kama akina Socrates wa Uyunani na wengine (ambao huwa ninawataja sana katika makala zangu) waliuwa ili kupisha utulivu ambao watawala waliuhitaji. "Wachochezi" wale walionekana kama mbu anayesumbua mtu anayetaka kulala usingizi bila bugdha.

Lakini baada ya kubaini umuhimu wa uchochezi (na wachochezi) katika kukuza utamaduni wa kufikiri zaidi, kufikiri kwa umakini zaidi, kufikiri kwa usahihi zaidi, wakoloni wetu walijenga misingi ya kukataa utamaduni wa utulivu kule kwao. Na waliporuhusu tu uchochezi waliona faida zake. Walipata mapinduzi ya kilimo na baadaye mapinduzi ya viwanda.

Na endapo wakoloni wetu wangeendekeza utamaduni wa kupenda na kusisitiza utulivu kule kwao, basi wasingevumbua hata hizo merikebu walizotumia kusafiri kuja huku kututawala. Wakoloni wetu wangeendekeza utamaduni wa utulivu wangebuni vipi silaha kali kama bunduki ambayo wallitumia kutufanya sisi kuwa watulivu ili watutawale na watunyonye?

Afrika ya leo haihitaji utulivu hata kidogo. Afrika iliyo huru inahitaji utulivu wa kazi gani? je, baada ya wananchi hawa kuishi kwa kulazimishwa utulivu kwa miaka mingi tokea enzi za utumwa si kweli kwamba sasa watu wetu wanahitaji uchochezi? je, si kweli kwamba watawaliwa wa Bara hili sasa, kuliko wakati mwingine wowote, wanahitaji akina Socrates wao, akina Fanon wao, na akina Che Guevara wao, ili wapindue fikra, mitazamo na utamaduni wa utulivu ambao umewafunga akili na midomo yao kwa muda mrefu na kwa faida ya watawala?

Watu watulivu si watu wa vitendo. Ni watu wa kutarajia anayewatuliza awatekelezee kila jambo. Katika utulivu hakuna ubunifu. Utulivu unasaidia tu pale mtu au watu wanapokuwa katika mazoezi ya kutafakari na kupumzisha akili, au kusali basi.

Lakini utulivu wa kuvumilia shida zinazotokana na mifumo mibovu ya utawala; utulivu wa kukubali kunyonywa na watawala wababe; utulivu wa kukubali kuburuzwa na kukandamizwa; utulivu wa kukubali kudhalilishwa ; katu si tunu au kitu cha kujivunia ; ni ujuha.

Tulipoingia katika mfumo wa vyama Vingi kwa mara nyingine mwaka 1992 hapa Tanzania, tulifanya hivyo ili kuruhusu utamaduni wa uchochezi. Tulitambua kwamba dunia ilivyokuwa imebadilika tusingeweza kuendelea na utamaduni wa "zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti".

Katika utamaduni wa vyama vingi utamaduni wa uchochezi husaidia kuwapo kwa hoja ambazo watawala hawataki kuzisikia lakini ambazo zinaweza pia kujibiwa kwa hoja nyingine yenye usahihi zaidi wa fikra na watawala wale wale.

Ni katika utulivu tuliokuwa nao toka uhuru ndiyo maana Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere hakumaliza matatizo yote ya Watanzania. Ndiyo maana hata mzee wetu Alhaji Ali Hassan Mwinyi hakumaliza matatizo yote ya Watanzania. Ndio maana hata Benjamini Mkapa hakumaliza matatizo yote ya Tanzania. Na ndio maana hata Rais wetu wa sasa hatoweza kuyamaliza matatizo yote ya Watanzania.

Lakini endapo tutakubali kwa moyo mmoja mfumo wa demokrasia ya vyama vingi (ambao hurutubishwa na utamaduni wa uchochezi) hatuna budi kuwa tayari kwa mabadiliko. Na kinachosababisha baadhi ya matatizo yetu, tena ya msingi , yanaendelea kututesa si kwamba hayawezi kutatulika na Watabzania wengine. La hasha! Matatizo yale yanaendelea kututesa kwa sababu tumeendelea kuamini kwamba fikra zile zile za miaka nenda rudi za kusisitiza utulivu zitatatua matatizo yale.

Ni ndoto . Tena za alinacha. Ili tuendelee , tunahitaji uchochezi zaidi. Tunahitaji namna ya tofauti kabisa za kuangalia utatuzi wa matatizo yetu.
 
Hao ndo wasomi wa Tanzania ni vigumu kusimamia kile wanachoaamini na ambacho wamekifanyia utafiti kwa muda mrefu iwapo tu wamepewa sehemu ya "kumega mkate"
Sasa unajiuliza wenzetu walipoazimia mapinduzi wa viwanda waliruhusu kila wazo yenye kujenga na kukosoa mwisho wa siku wakapata kile walichokiihitaji kwa sisi tunakuwa waoga linapokuja swala la kukosoana? kwa nini tusiruhusu watu watoa mawazo yao hata kama wengine wanaona hayajengi lakini pengine hao ndo wana hoja ya msingi baada ya kipindi fulani ukweli unadhihirika.
 
Sasa hivi amejitoa ufahamu kabisa, lazima atakanusha hili bandiko
 
Kashanyeshwa maji ya kijani,kwa sasa ataruka mita mia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom