DPP, Polisi, TAKUKURU hapa ndipo mmetufikisha!

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Juzi Rais JPM, wakati akimwapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Cuba, Balozi Mlowola, alizungumzia mambo mawili yanayoshangaza sana. Kwanza alizungumzia mpango wa kifisadi na upigaji uliopangwa na watumishi wa serikali kupitia mradi wa kuipiga rangi ndege iliyotolewa na serikali kwa Air Tanzania.

Pili aligusia kushangazwa na kitendo cha TAKUKURU kushindwa kumfikisha mahakamani afisa wake mwandamizi 'aliyewaibia' mamilioni ya fedha wafanyakazi wenzake kupitia uuzaji wa viwanja hewa kule Bagamoyo. Siku mbili baadae, mtuhimiwa huyo alifikishwa mahakamani (baada ya Rais kueleza kushangazwa kwake na jiitihada za TAKUKURU kumkingia kifua mtuhumiwa huyo). Ikumbukwe kuwa, suala hilo limesharipotiwa na vyombo vya habari zaidi ya miaka miwili iliyopita! Wafanyakazi wa TAKUKURU walilalamikia utapeli huo kwa wakubwa wao na hata vyombo vya habari. Pamoja na kuwepo malalamiko hayo, inaonekana wazi kulikuwa na jitihada za makusudi za wakubwa wa TAKUKURU kumnusuru mkubwa mwenzao dhidi ya tuhuma hizo za jinai.

Miaka michache iliyopita kulikuwa na tuhuma za utapeli dhidi ya mke wa aliyekuwa Mkuu wa Operesheni wa Polisi. Tuhuma hizo ambazo zilichapwa na Gazeti la Raia Mwema kwa matoleo mfululizo, ziliwanukuu walalamikaji walidai kuwa mke huyo aliwaahidi kuwatafutia kazi Usalama wa Taifa (TISS) iwapo wangemlipa kiasi kadhaa cha pesa. Kwa mujibu wa 'Raia Mwema', Jeshi la Polisi lilikuwa likichunguza tuhuma hizo dhidi ya mke huyo wa Kamishna huyo wa Polisi. 'Raia Mwema' waliongea na walalamikaji na mtuhumiwa na kuchapa habari hiyo ukurasa wa mbele. TISS, Jeshi la Polisi na TAKUKURU hakuchukua hatua zozote dhidi ya mke huyo wa kigogo wa Polisi zaidi ya polisi kumlinda mama huyo kwa manufaa ya mumewe ambaye alikuwa miongoni mwa vigogo wakuu wa Polisi Tanzania. Labda wanasubiri JPM alizungumzie hilo ndipo wamfikishe mtuhumiwa Mahakamani.

Najiuliza, hivi hawa TAKUKURU, Polisi, TISS na ofisi ya DPP hawafanyi kazi zao hadi rais alalamike? Mnakumbuka hivi karibuni 'Majira ' walichapisha barua ya mfanyabiashara wa Tabora akidai kubambikiwa kesi mbaya na Polisi wa Tabora na akaachiwa baada ya Rais mwenyewe kuamua kufuatilia na kuthibitisha uonevu huo wa Polisi dhidi ya huyo raia mwema. Haya masuala yanaonyesha udhaifu mkubwa wa vyombo hivi vya dola vinanavyoaminiwa na wananchi. Ina maana ikiwa malalamiko hayatamfikia Rais vyombo hivyo haviwezi kuchukua hatua?

Nachokiona ni kuwa kuna udhaifu mkubwa katika vyombo hivyo. Umefika wakati wa kuvifanyia overhaul vyombo hivyo na kuviunda upya ili viweze kutimiza wajibu wake kwa umma ipasavyo.

Wakatabahu,
Vv



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom