DPP na Rufaa Butu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP na Rufaa Butu...

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Aug 15, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Mheshimiwa Eliezer Feleshi,amewasilisha Kusudio la kukata Rufaa dhidi ya Hukumu ilimweka huru Prof. Costa V. Mahalu na Bi.Grace Martin. Hii inamaana kuwa Jamhuri itakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi,Ilvin Mgeta pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

  Kama Jamhuri,ikiwa na muda wa kutosha wa kuthibitisha shtaka pale Kisutu,ilishindwa kufanya hivyo,itaweza kuthibitisha Mahakama Kuu? DPP haoni kuwa kama hana ushahidi wa kutosheleza,Rufaa hii itagharimu fedha za walipakodi wa kitanzania bure? Kimsingi,naiona Rufaa ya DPP kama ni butu.Hatahivyo,Mahakama Kuu itatupa jibu kamili siku itakapofika...
   
 2. zethumb

  zethumb JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 606
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  nimesoma hukumu ya Mhe. Mugeta, kwa kweli reasoning yake ni ya hali ya juu sana katka kesi hii. jamhuri kwenye kesi walitumia circumstantial evidence kuprosecute kesi hii, wakidai kukiukwa kwa baadhi ya taratibu ndani ya wizara ya mambo ya nje na katiba na sheria, utajiuliza nani wa kulaumiwa hapo, Mahalu aliyekuwa Italy au maofisa wa wizara husika? kingine, eti kulikua na mikataba miwili katika ununuzi moja ya milion1 na ushee na nyingine 3 na ushee kwa hiyo wakaona jamaa kutumia hii ya 3 na ushee kaweka kibindon million mbili, nadhan na ninawashauri ofisi ya DPP na TAKUKURU iwe na mpango madhubuti ya kufanya utafiti wa kina katka kila kesi inayopeleka mahakani na si kukurupuka na ushaidi wa kimazingira.
   
Loading...