DPP awatangazia kiama wanaoandika "vijineno" mitandaoni

DPP awatangazia kiama wanaoandika "vijineno" mitandaoni

Hizi ndio habari zinazotamalaki kwasasa tanzania..."kushughulikia". Kila aliyepewa dhamani anaonyesha kipaji cha kushughulikia watu, sisikii habari za kustawisha ubora wa maisha ya wananchi, ni habari za kushughulikiana na ujenzi wa vitu. Sijui wananchi nao wana mpango wowote wa kushughulikia hawa viongozi kwenye chaguzi zijazo au tayari washashughulikiwa na process nzima ya uchaguzi kiasi kwamba hata hamu ya kwenda kuwashughulikia viongozi kwenye uchaguzi imeisha kabisa
Umenena vyema mkuu yaani kila siku zinatungwa sheria kali kwaajili ya kuwazima wananchi
 
Ndio mimi naposemaga ujinga huu utaisha lini? Kuna mambo makubwa ya kitaifa yanahitaji kupatiwa ufafanuzi we uje udili na vijineno na video mitandaoni!!! Nchi hii inawatanzania wangapi? Je wote wanatumia mindao? Yaaaan mimi huwa napataga hasira wakti mwingine
Kwa haya yanayoendelea Tanzania kwasasa hutakiwi kukasirika, utapata magonjwa yasiyoambukiza bure. Njia nzuri ni kuchukulia kama komedi flani,cheka ongeza siku na kuboresha afya. Huyu jiwe bado tunae kwa miaka kadhaa, tuvumilie tu huku tukipigania haki bila kukasirika
 
Angeshughulika na ishu kubwa kama wasiojulikana, rushwa za hongo za chaguzi, mikataba ya miradi mikubwa hivi vitu vidogo vidogo ni kudhalilisha hadhi yake,kama wako serious wangeanza na musiba wa taifa,konki masta, nk ili wamaanishe.
 
Bo
Ndio mimi naposemaga ujinga huu utaisha lini? Kuna mambo makubwa ya kitaifa yanahitaji kupatiwa ufafanuzi we uje udili na vijineno na video mitandaoni!!! Nchi hii inawatanzania wangapi? Je wote wanatumia mindao? Yaaaan mimi huwa napataga hasira wakti mwingine
Bora hata ww umeweza kuongea.
 
Kwa maana hiyo DPP hana kazi yakufanya offcn kwake kama hana kazi si akae kimya
 
Mkurugenzi wa makosa ya jinai amesema atawashughulikia vikali wale wote wanatuma vijineno vya uzushi mitandaoni sambamba na wale wanaopost picha za ngono.

Chanzo: Uhuru!
Kumiliki simu ni hatari sana kwani wakati wowote inaweza kukutia matatani mradi tu umeandika neno dogo lakini wakubwa wakalikuza. Wakati watanzania tunapambana na vibaka mitaani wanaotoboa madirisha yetu usiku bila sisi kupata msaada wa patrol za polisi wao polisi wanatoboa simu zetu kutafuta vineno vidogovidogo! Siku hizi raia mwema ni yule asiyemiliki simu kwani polisi hawana shughuri naye.
 
Mkurugenzi wa makosa ya jinai amesema atawashughulikia vikali wale wote wanatuma vijineno vya uzushi mitandaoni sambamba na wale wanaopost picha za ngono.

Chanzo: Uhuru!
Usitutishe,Usitutishe,Usitutishe
 
Back
Top Bottom