neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
SERIKALI imeendelea kuwang’ang’ania wakurugenzi wa Kampuni ya Kusimamia shughuli za Upatu, kwa mtindo wa Kupanda Mbegu na Kuvuna Fedha (DECI), kwa kutaka kutai sha mali zenye thamani ya Sh bilioni 14.1 zilizopatikana kupitia kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amefungua maombi namba 45/2019 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Wakurugenzi wa DECI ambao ni Mchungaji Jackson Mtares, Dominic Kigendi, Thimotheo Loiting’ye na Samwel Mtares.
Maombi hayo yamesikilizwa mbele ya Jaji Stephen Magoiga, ambapo anaiomba Mahakama kutaisha mali ikiwemo nyumba, magari, viwanja na fedha. Mganga akishirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Shedrack Kimaro na Theophil Mutakyawa, alidai ushahidi wa kwamba mali hizo zilitokana na DECI wanao, kwa sababu inaonesha kuwa fedha zilizokusanywa na kuingia kwenye akaunti ya kanisa ni za kampuni hiyo na wajibu maombi, hawajapinga suala hilo.
Alidai wajibu maombi hao walikutwa na hatia katika kesi namba 109/2009 kwa makosa ya kuchezesha biashara ya upatu na kwamba bila kukusanya fedha kutoka kwa wanachama hao, kusingekuwa na mashitaka hayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambayo iliwatia hatiani.
Pia alidai kuwa wajibu maombi katika kiapo chao, hawajaonesha biashara ambazo DECI walikuwa wakiziendesha mpaka kupata mali hizo mbali na biashara ya upatu na kwamba fedha zilizoingia kwenye akaunti ya Mchungaji Mtares ni za DECI. Akiwasilisha sababu za maombi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro alidai maombi hayo yameambatanishwa na hati ya kiapo pamoja na vielelezo 21.
Kwamba mashitaka hayo ya kuendesha biashara ya upatu ni moja kati ya makosa mazito, kama ilivyoainishwa na Mahakama ya Rufani. “Mahakama ya Rufani ilielekeza yafunguliwe maombi Mahakama Kuu kuomba mali ambazo zimetokana na makosa hayo kutaishwa hivyo haya ni maombi maalum kama ilivyoelekezwa na mahakama hii kubwa,” alidai Kimaro.
Alidai kuwa wahalifu hawawezi kuachwa kunufaika na mali ambazo zimetokana na uhalifu, hivyo wanaomba kuzitaisha ili wahusika wasinufaike nazo. “Ni rai yetu mali ambazo DPP anaomba zitaishwe ni matunda ya uhalifu yaliyofanywa na wajibu maombi. Ushahidi unaonesha kwamba mali hizo zimetokana na uhalifu kama ilivyoelezwa na Mchungaji Mtares ambaye alieleza kuwa kampuni hiyo ilipata fedha kutoka kwa wanachama wa DECI na kwamba hakukuwa na kipato kingine zaidi,” alieleza.
Kimaro alidai DECI ilikuwa ikipokea fedha kutoka kwa wanachama na hakukuwa na uzalishaji mwingine zaidi ya huo. Alidai kuwa hata katika hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi, hawajaonesha ushahidi kwamba DECI ilikuwa na shughuli nyingine hivyo wanaomba kutaisha mali zote kwa sababu wahusika walikiri kwamba mali zilitokana na upatu huo.
Pia alidai kuwa kama mali hizo ni za wajibu maombi walipaswa kutoa ushahidi kwa sababu kwenye kiapo chao walidai hawazitambui hivyo wanaomba zitaishwe. “Hata kwenye suala la fedha, Mchungaji alieleza kuwa fedha ziliwekwa kwenye akaunti za benki mbalimbali ni za wenye akaunti lakini ukweli ni kwamba fedha hizi zilitokana na makusanyo kutoka kwa wanachama na uendeshaji wa upatu,” alidai.
Akipinga maombi hayo, Wakili wa wajibu maombi, Majura Magafu alidai kuwa wanapinga maombi hayo kuwepo mahakamani kwa sababu ni dhahiri kwamba wajibu maombi wa kwanza hadi wane walikutwa na hatia katika makosa mawili ya jinai na kupewa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria.
Alidai haina maana kwamba kila mtu anayetiwa hatiani basi lazima mali zake zitaishwe na ndio sababu Mahakama ya Rufani alitoa maelekezo katika hukumu yake ya Septemba 7,2018 katika rufaa namba 2/2018 iliyofunguliwa na DPP dhidi ya wajibu maombi, kwamba akitaka mali za wahusika afanye maombi mahakamani. Magafu alidai maombi hayo yameletwa mahakamani ili waweze kujiridhisha kwamba mali zinazodaiwa kumilikiwa na watuhumiwa walizipata kwa njia ya ulaghai.