DPP atoa muongozo kuhusu Watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi kulipa fedha walizotafuna ili kusamehewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Amesema mtuhumiwa mwenyewe ambaye yupo Mahabusu anatakiwa kuandika barua kupitia kwa Mkuu wa gereza na kukiri kosa ndipo ofisi yake itachukua hatua

Amesisitiza kwamba Mtuhumiwa mwenyewe ndiye anatakiwa kuandika barua na sio kuwakilishwa na Wakili kwani Wakili anaweza kubadilika na hata Mtuhumiwa kumkana kwamba hakumtuma kufanya alichokifanya

wacha weeee
....jpg
 
Rais ameshauri jambo zuri lakini DPP anapaswa kutumia sheria kulitekeleza na sio kubabaika na amri za Rais ambazo wakati mwingine zinaweza kuwa sio sahihi sana.

Kuna sheria mpya ya plea bargaining imekuja hivi majuzi. Basi itumike hiyo.

Magufuli mwenyewe alishatoa tahadhari hapo jana, kwamba, ENDAPO SHERIA INARUHUSU basi angependa kuona mahabusu wanakiri na kuachiwa. (endapo sheria inaruhusu).

Sijui huwa wanamuelewa Rais vizuri hawa? au wanatetemeka tetemeka tu?

Ni kazi yako DPP kufahamu endapo sheria inaruhusu na inaruhusu ndani ya mipaka ipi!

Tahadhari.
 
Haya ni maajabu ya karne na hii ni Tanzania pekee inayoweza kufanya hivyo
 
Usimlaumu DPP mkuu, hata wewe ungebabaika kutekeleza Mambo ya kisheria kwa kufuata mkumbo wa kisiasa. Hapa namba moja ni Kama kashatoa amri Ni juu ya DPP kuamua aliwekeje Hilo swala.

Kwa Mara nyingine, muhimili wa mahakama na Sheria umenajisiwa

Back
Top Bottom