Kawe Alumni
JF-Expert Member
- Mar 20, 2019
- 8,685
- 11,988
Hizo picha ungezitolea MaelezoWyatt...
Ukoloni ulikuja na changamoto nyingi sana.
Leo hii katika umri wangu wa uzee nikiangalia nyuma naona zaidi kuliko
nilivyokuwa naoana nilipokuwa kijana.
Uoni huu si wa macho bali ni kuangalia kwa ndani ya nafsi.
Nimezaliwa tayari nimekuta wazee wangu wengi wamechotwa sana na
Uzungu na wakau-perfect hata kuwashinda Wazungu wenyewe.
Mtoto aliyezaliwa katika mazingira kama haya hawazi kusalimika kwa
urahisi.
Napata akili nasikia muziki unaopigwa nyumbani kwetu ni wa Loius
Armstrong, Alma Cogan, Victor Sylvester, Septet Habanero na kidogo
Salum Abdallah, Kiko Kids na Cuban Marimba Cha Cha Band na Mwenda
Jean Bosco kuwataja wachache.
Afro Americans walikuwa na ushawishi mkubwa lakini zaidi si kwa wazee .
wetu ila kwetu sisi ambao kwao ni kizazi cha pili.
Tukisikiliza muziki wa Wilson Picket, James Brown, Aretha Franklin,
Helen Shapiro, Cliff Richard na Elvis Presley.
Sal Davis alikuwa ''all rounder,'' aliweza kupiga mchanganyiko wa muziki
wa Kimarekani na muziki wa Ulaya na hata staili za kwao Mombasa.
Nimeandika maisha ya Sal Davis bado kuchapa kitabu lakini unaweza
kusoma maisha yake hapo chini kwenye hii link:
FROM THE PAGES OF THE EAST AFRICAN MAGAZINE: SAL DAVIS
Sal Davis: The man who brought the roaring 60s to swinging Dar By MOHAMED SAID Sal Davis at Chef Pride Lumumba Street I HA...mohamedsaidsalum.blogspot.com
View attachment 1176734
Unataka sasa kujua asili yangu...
Sidhani kama kuna watu wanataka kujua baba yangu nani, mama yangu
nani, nk.
Ila nitakueleza kuwa historia yetu iko Dar es Salaam sasa miaka 100 na
mimi nimejifunza historia hii na naweza kwenda nyuma vizazi saba ingawa
sasa na wajukuu zangu tushafika vizazi tisa wote Waafrika weusi kutoka
Tanganyika na Belgian Congo.