Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,917
- 30,259
DOWN MEMORY LANE...
Kushoto Salim Himid na Sal Davis (Shariff Salim Abdallah)
Hii ni historia ya Msikiti Mkuu wa Paris ambao wenyewe wanauita Grande Mosquee de Paris na ni msikiti wenye mengi sana ya kukumbukwa.
Nimeswali msikiti huu mara mbili mwaka wa 1993 na mwaka wa 2011.
Sala moja ya mwaka wa 2011 ilikuwa Sala ya Ijumaa.
Wangazija wako wengi sana Pairis na huu ni msikiti wao,
Mwaka wa 2011 nilikuwa Paris na rafiki yangu na Salim Himid na yeye ndiye aliyenipeleka kuswali Ijumaa.
Salim Himid is an extremely intelligent person yaani ni mmoja wa watu ambao Allah kawajalia akili ambayo si za kawaida na nimefahamishwa hili na jamaa zake.
Kabla ya kufahamiana na Salim nilipata siku moja kukutana na kaka yake Dr. Said Himid.
Dr. Himid alikuwa amekuja Dar es Salaam na tukakutana kwenye mwaliko wa futari kwa jamaa yake mmoja.
Dr. Said Himid wakati wake alitokea mwanafunzi wa kwanza katika mitihani ya Cambridge.
Salim Himid amezaliwa Zanzibar akasoma Ufaransa akawa Foreign Minister Comoro chini ya uongozi wa Ali Solih.
Inawezekana Salim Himid alikuwa Mzanzibari wa kwanza kushika nafasi ya juu Ngazija au mmoja wa Wazanzibar walioshika nafasi muhimu kisiwani hapo.
Salim anasema Kingazija, Kiingereza, Kifafaransa, Kiarabu na Kiswahili vizuri bila wasiwasi.
Serikali ya Ali Solih ilipopinduliwa na Bob Denard mamluki kutoka Afrika ya Kusini. Salim akafungwa ingawa alikuwa hayuko serikalini baada ya kutofautiana na Solih.
Salim Himid alipotoka jela akaenda exile Paris.
Salim Himid na Salim Abdallah aka Sal Davis nimewapiga picha katika Barza yetu Lumumba Avenue.
Walikuwa wanakutana takriban baada ya zaidi ya miaka 40.
Salim mara ya mwisho kamuona Sal Davis ilikuwa mwaka wa 1963 kabla ya mapinduzi,
Salim akamkumbusha kitu Sal alichokuwa amesahau na Sal akapiga mshangao akasema, ''Nilisahau kabisa wewe una kumbukumbu kubwa sana.''
Salim alimwambia Sal Davia kuwa mara ya mwisho kamuona ilikuwa mwaka wa 1963 alipofanya show Zanzibar katika Ukumbi wa Said Khalifa.
Salim akiusudu muziki wa Sal.
Akamwambia baada ya show Sal alikwenda kwenye gari lililokuwa nje ya ukumbi linauza Hall's Ice Cream, kulikuwa na microphone na loud speaker na Sal akaimba nyimbo moja ya Perry Como vijana wenzake wakiwa wamelizunguka gari lile.
Sal Davis miaka ile alikuwa star mkubwa aliyeanza career yake Uingereza akiwa kijana mdogo hajafikisha hata miaka 20.
Baada ya 1963 mapinduzi Salim akaondoka kwenda France kutafuta elimu akisafiri overland akivuka mpaka mmoja hadi mwingine hadi akafika Cairo kabla ya kuvuka bahari kuingia Ulaya.
Anasema alipofika Cairo akakuta Mohamed Abduwahab mwimbaji maarufu wa Misri enzi hizo ametoa nyimbo ambayo ilivuma Misri yote.
Nyimbo hii ilikuwa kipigwa kwenye radio taxi drivers wanaegesha taxi zao pembeni wakiongeza sauti za radio zao ndani ya magari yao kusikiliza.
Hii ilikuwa miaka ya 1960s wakati wa Gamal Abdel Nasser na siasa za Arab Nationalism zilikuwa juu kabisa.
Iko siku nilikuwa nasafiri na Egypt kutoka Dar es Salaam naelekea London.
Ndege yetu inaondoka sita ya usiku lakini kwa bahati mbaya ikawa na hitilafu ikabidi tuondoke siku ya pili mchana kwa hiyo kufika Cairo ndege yetu ya kuunganisha ikawa iemshaondoka ikabidi tuwekwe hoteli sehemu moja inatwa Heliopolis hadi siku ya pili mchana.
Tulipokuwa tuna-check in pale hotelini nikawa naona kwenye TV Mohamed Abdulwahab anapiga muziki wake na ikisha nyimbo hii inaingia nyingine.
Kumbe siku ile ndiyo alikuwa amefariki na TV stations na FM Radio zote zilikuwa katika maombolezo.
Nilikuwa na Salim Paris nikitokea Berlin kila siku asubuhi alikuwa akinifuata hotelini kwangu kunitembeza mjini na mie sikumwacha akawa njia nzima na kutwa nzima ananisomesha mambo yaliyopita Zanzibar, Comoro na Ufaransa na katika duru za siasa na diplomasia katika mambo aliyoshuhudia kwa macho yake mwenyewe.
Ugomvi wangu na Salim kila akija Dar es Salaam tikikaa na kuzungumza ni kuwa hajakubali kuandika.
Sijui kwa nini anafanya ajizi.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Salim Himid na Seif Shariff Ngazija
Picha: Kushoto Salim Himid na Sal Davis wakiwa Barzani Lumumba Avenue, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Salim Himid na Seif Shariff Ngazija, Sal Davis akiwa Ujerumani na Mwandishi nje ya Grande Mosquee de Paris 1993.