MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,603
Nimeopoa taarifa hii kutoka maktaba ya HabariLeo. Ni mwaka umepita sasa tangu JK "apigilie msumari wa mwisho Dowans", kwa kuponda maamuzi ya washauri wake. Badala yake, mataizo ya umeme ndio kwanza pamoja na ahadi zote alizotoa. Na kama haitoshi, sasa Dowans ndiyo iliyopigilia msumari wa mwisho JK, TANESCO na uchumi wa Watanzania. Kazi kwetu!
JK APIGILIA MSUMARI WA MWISHO DOWANS (CHANZO: HabariLeo tarehe 2/4/2009).
Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.
"Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.
Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.
"Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.
"Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.
Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.
Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo".
"Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida".