AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,501
- 189
- Thread starter
-
- #121
RIPOTI YA KAMATI YA BUNGE
YALIYOMO
VIFUPISHO VYA MANENO………………………………………………….iii - iv
1.0 UTANGULIZI...........................................................1
1.1 Hoja ya Kuunda Kamati Teule ......................................................................... 1
1.2 Wajumbe na Hadidu za Rejea.......................................................................... 2
1.3 Utekelezaji wa Majukumu ................................................................................ 4
2.0 UKAME NA TATIZO LA UZALISHAJI UMEME NCHINI .......... 10
2.1 Taarifa za Awali na Hatua za Serikali .......................................................... 10
2.2 Maandalizi ya Zabuni ....................................................................................... 15
2.3 Mchakato wa Zabuni ndani ya TANESCO ..................................................... 18
2.3.1 Vigezo vya Tathmini (Preliminary Evaluation)......................................... 19
2.4 Mchakato wa Zabuni Ndani ya Wizara ......................................................... 25
3.0 MKATABA KATI YA TANESCO NA RICHMOND DEVELOPMENT40
3.1 Madhumuni, Muundo na Muda wa Mkataba................................................ 40
3.2 Malipo ya Kodi.................................................................................................... 43
3.3 Malipo mengine ................................................................................................. 45
3.4 Kuhaulisha Mkataba.......................................................................................... 46
3.5 Fidia kwa Kuchelewa kutekeleza Mkataba................................................. 46
3.6 Ulinganisho na Mikataba Mingine.................................................................. 48
3.7 Uzingatiaji wa Mkataba huu katika kutekeleza Sheria ya CRB na ERB 57
4.0 UTEKELEZAJI WA MKATABA ..................................... 59
4.1 Barua ya Dhamana ya Benki (Letter of Credit) ......................................... 59
4.2 Majadiliano na Makubaliano kuhusu Masharti ya Barua ya Dhamana ya
Benki .................................................................................................................... 63
4.2.1 Maombi ya Masharti ya Barua ya Dhamana ya Benki (Awamu ya
Kwanza)............................................................................................................... 63
4.2.2 Mapendekezo ya Richmond Development Company LLC kutaka
Masharti mengine mapya ya Barua ya Dhamana ya Benki (Awamu ya
Pili)....................................................................................................................... 67
4.3 Mchakato wa Kufungua Barua ya Dhamana ya Benki............................... 70
ii
4.4 Maombi ya Richmond Development Company LLC kubadilisha tena
Masharti ya Barua ya Dhamana ya Benki (Awamu ya Tatu)................... 74
4.5 Kushindwa kwa Richmond Development Company LLC kutimiza
masharti ya Mkataba ........................................................................................ 84
4.6 Mwelekeo Mpya wa Mkataba wa Umeme wa Dharura ............................. 89
4.7 Uhaulishaji wa Mkataba kati ya TANESCO, Richmond na Dowans ........ 95
4.8 Mchakato wa Malipo kwa Dowans Holdings S.A......................................... 97
4.9 Madai na malipo ya Dowans Holdings S.A ya Capacity na Interim
Energy Januari 2006 hadi Oktoba, 2007.................................................. 101
5.0 TAARIFA ZA TAKURU/PPRA .....................................104
5.1 Chimbuko la Uchunguzi................................................................................. 104
5.2 Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) ........... 109
5.3 Taarifa ya TAKURU ......................................................................................... 114
5.4 Vyombo vya Habari – Magazeti .................................................................... 122
6.0 RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC NI KINA NANI? .125
6.1 Utambulisho wake Kisheria .......................................................................... 125
6.2 Hadhi ya Richmond kisheria/kikampuni Marekani ................................. 126
6.3 Hadhi ya Richmond kisheria/ kikampuni Tanzania ................................ 132
6.4 Uwezo wa Richmond Kifedha, Kitaalamu, Kiutendaji ........................... 138
7.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ..................................142
7.1 Hitimisho.........................................................................142
7.2 Mapendekezo ya Kamati Teule ............................................149
7.3 Shukrani..........................................................................164
iii
VIFUPISHO VYA MANENO
$ Alama ya Dola ya Kimarekani
Aggreko Aggreko International Projects Limited
Alstom Alstom Power Rentals
BoT Bank of Tanzania
BRELA Business Registration and Licensing Authority
CNG Compressed Natural Gas
COD Commercial Operating Date
CRB Contractors Registration Board
CTI Confederation of Trade and Industries
Dba Doing business as
Dk Daktari
Eng. Injinia
ERB Engineers Registration Board
GN Government Notice
GNT Government Negotiation Team
ICC International Chamber of Commerce
IPTL Independent Power Transmission Limited
kWh kilo Watt hour
LC Letter of Credit
LLC Limited Liability Company
Ltd Limited
Mb Mbunge
MDRI Multilateral Debt Relief Initiative
iv
Mhe. Mheshimiwa
MoF Ministry of Finance
MW Mega Watt
PPA Public Procurement Act
PPRA Public Procurement Regulatory Authority
t/a Trading as
TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKURU Taasisi ya Kuzuia Rushwa
TANESCO Tanzania Electric Supply Company Limited
TPDC Tanzania Petroleum Development Corporation
TRA Tanzania Revenue Authority
UCP Uniform Customs Practice
US$ United State Dollar
USc United States cents
1
TAARIFA YA KAMATI TEULE ILIYOUNDWA NA BUNGE LA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 13 NOVEMBA, 2007
KUCHUNGUZA MCHAKATO WA ZABUNI YA UZALISHAJI UMEME WA
DHARURA ULIOIPA USHINDI RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY
LLC YA HOUSTON, TEXAS, MAREKANI MWAKA 2006
1.0 UTANGULIZI
1.1 Hoja ya Kuunda Kamati Teule
Tarehe 13 Novemba, 2007 wakati Bunge likijadili Taarifa ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara kwa Mwaka 2006,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa William H. Shellukindo
(Mb), alitoa hoja ya kuunda Kamati Teule ya kuchunguza mchakato
ulioendeshwa nchini mapema mwaka 2006 wa kumpata mzabuni wa
kuzalisha umeme wa dharura wa MW 100 na kutathmini mkataba
baina ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mshindi wa
zabuni hiyo Richmond Development Company LLC.
Hoja hiyo iliwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa masharti
yaliyowekwa na Kanuni ya 104 (1) ya Kanuni za Bunge, Toleo la
mwaka 2004 inayotamka kwamba:-
2
"Kamati Teule yaweza kuundwa na Bunge kwa
madhumuni maalum, kwa hoja mahususi itakayotolewa
kwa ajili hiyo na kuafikiwa".
1.2 Wajumbe na Hadidu za Rejea
Baada ya hoja hiyo kuafikiwa na Bunge, Spika wa Bunge Mheshimiwa
Samuel J. Sitta, (Mb) aliteua Wabunge wafuatao, kuunda Kamati
Teule kwa mujibu wa Kanuni ya 104 (3) ya Kanuni za Bunge, Toleo
la 2004:
(a) Mhe. Dk. Harrison George Mwakyembe, Mb
(b) Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, Mb
(c) Mhe. Mohamed Habib Juma Mnyaa, Mb
(d) Mhe. Lucas Lumambo Selelii, Mb
(e) Mhe. Herbert James Mntangi, Mb
Tarehe 15 Novemba, 2007 Mhe. Spika aliipa Kamati Teule siku
thelathini kukamilisha kazi yake na Hadidu za Rejea zifuatazo kwa
ajili ya kutekeleza kazi hiyo ya uchunguzi;
1. Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina
nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima
uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na
kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100,
3
2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni
waliyoshinda Richmond ilivyoshughulikiwa kuanzia
Kamati ya Zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha kuwa
sheria, taratibu, miiko na maadili ya zabuni
yanayotawala zabuni za aina hiyo vilifuatwa au vipi,
3. Kutathmini mkataba baina ya Richmond Development
Company LLC na TANESCO ili kujiridhisha kuhusu uhalali
wa masharti ya mkataba huo ukizingatia gharama na
masharti mengine ukilinganisha na masharti yaliyomo
katika mikataba ya aina hiyo iliyoafikiwa na
TANESCO/Serikali,
4. Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa
Richmond kama vile kufunguliwa Letter of Credit na
kupima uhalali wake,
5. Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za TAKUKURU,
PPRA na taarifa zozote nyingine zilizoangalia utaratibu
wa zabuni ya Richmond, na
6. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na
mchakato mzima wa Richmond ili kutoa mapendekezo ya
kuboresha taratibu za zabuni kwa siku zijazo, kwa
maslahi ya Taifa letu.
4
1.3 Utekelezaji wa Majukumu
Mara baada ya kuteuliwa, Wajumbe wa Kamati Teule walimchagua
Mhe. Dk. Harrison George Mwakyembe, (Mb) kuwa Mwenyekiti kwa
mujibu wa Kanuni ya 104 (3) ya Kanuni za Bunge, Toleo la mwaka
2004. Aidha, kwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya 105(3) ya Kanuni
hizo za Bunge, upana wa hadidu rejea na kipindi kifupi cha mwezi
mmoja tu cha kukamilisha kazi hiyo, Kamati Teule ikaona umuhimu
wa kumchagua mmoja wao kutekeleza wajibu wa Makamu
Mwenyekiti kwa lengo la kuboresha ufanisi katika ufuatiliaji wa
karibu wa masuala mbali mbali ndani na nje ya vikao vya Kamati
Teule. Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, (Mb) akachaguliwa
kutekeleza wajibu huo. Vilevile, Mheshimiwa Spika alimteua Ndugu
Anselm Lyatonga Mrema kuwa Katibu wa Kamati Teule akisaidiwa na
Ndugu Emmanuel Mpanda, Lina Kitosi na Nenelwa Mwihambi.
Kamati Teule ilianza kazi yake mara moja kwa kukusanya na kusoma
nyaraka mbalimbali za msingi kama vile Mkataba kati ya TANESCO
na Richmond Development Company LLC, Sheria ya Ununuzi wa
Umma (Public Procurement Act) ya Mwaka 2004 na Kanuni zake
(Public Procurement Act (Goods, Works, non-Consultant Services &
Disposal of Public Assets by Tender) Regulations of 2005), taarifa ya
uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU)1 na taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa
Umma (Public Procurement Regulatory Authority-PPRA) kuhusu
1 Wakati huo ikiitwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU)
5
suala hilo. Vilevile, Kamati Teule ilianza kuandaa hati (summons)
kwa mujibu wa vifungu 13 (1) na 14 (1) na (2) vya Sheria ya Haki,
Kinga na Madaraka ya Bunge, 1988 (Sura ya 296) za kuita mashahidi
mbalimbali waliohusika kwa njia moja au nyingine katika mchakato
wa zabuni hiyo ya uzalishaji wa umeme wa dharura.
Hadi kufikia tarehe 15 Disemba jumla ya mashahidi 46 walihojiwa
na maswali 2061 kuulizwa. Pamoja na taarifa zetu tulizozitoa
kupitia vyombo vya habari na kuwataka wenye ushahidi wajitokeze
na kuhakikishiwa kuwa Sheria itawalinda, hakuna shahidi hata
mmoja aliyekuja kwa hiari yake mwenyewe bila kupelekewa hati ya
kuitwa. Aidha, hakuna mtu yeyote aliyeweza kutoa ushahidi wa
kimaandishi ulio wazi zaidi ya wale waliojifanya kuwa na uchungu
kwa kutoa taarifa zisizo na majina, namba za simu wala anwani kwa
madai ya kuogopa kuhatarisha maisha yao.2 Matokeo haya
yanaonesha hali ya uoga na kutojiamini inayowakumba Watanzania
wengi wanapotakiwa kuelezea rasmi yaleyale wanayoyanong'ona
kwa nguvu au kuyazungumza pembeni kwa hamasa kubwa. Kwa
mtindo huu Taifa linaweza kuishia kuwa la walalamishi wasio na
ujasiri wala dhamira ya dhati ya kukemea maovu pale inapobidi.
Mashahidi wengi walioitwa kwa hati hususan kutoka TANESCO,
Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Wizara ya Katiba
na Sheria walionesha hofu, mashaka na hali ya kutojiamini kwa
kutoa majibu yaliyofanana ya kiitifaki-itifaki na yaliyokosa mvuto na
2 Mfano wa barua kama hizo unaambatanishwa.
6
ushawishi wa kawaida mithili ya watu walioketishwa pamoja na
kukaririshwa hoja za kujibu. Kama itakavyoelezwa baadaye, baadhi
ya wataalam wa TANESCO walioikataa Richmond Development
Company LLC mara tatu wakati wa kutathmini zabuni ya umeme wa
dharura, kwa hoja za kitaalam kuwa haifai kwa vigezo vyote
muhimu, walifika mbele ya Kamati Teule wakiwa wapambe nambari
moja wa kampuni hiyo!
Aidha, nyaraka nyingi ambazo Kamati Teule ilizipata toka Serikalini
na taasisi mbali mbali, zilikuwa nakala zilizokosa mtiririko wa
kimasijala. Kamati Teule ilipodai nyaraka halisi kulinganisha na
nakala ilizokuwa nazo, ilipewa majalada yaliyoonesha dalili zote za
kukarabatiwa.
Hali hii ilijitokeza zaidi kwa TANESCO na Wizara ya Nishati na
Madini. Jalada halisi kutoka TANESCO lilichukua siku tatu kuifikia
Ofisi Ndogo ya Bunge likiwa na nyaraka zenye namba zilizokosa
mtiririko stahili. Wizara ya Nishati na Madini ndiyo iliyotia fora kwa
kumtuma Msaidizi wa Katibu Mkuu, Ndugu Julius Sarota tarehe 18
Disemba 2007 akiwa na maagizo ya kuwafungulia Wajumbe wa
Kamati Teule kurasa maalum tu na si nyinginezo hivyo kuinyima
Kamati Teule mtiririko halisi wa mawasiliano. Kamati Teule
haikuridhishwa na utaratibu huo, hivyo ilimtaka Msaidizi huyo wa
Katibu Mkuu aondoke na majalada yake na kumpelekea hati ya
kuitwa Katibu Mkuu, Ndugu Arthur Mwakapugi afike yeye mwenyewe
na majalada hayo.
7
Tarehe 19 Disemba 2007 Katibu Mkuu huyo kwa maneno mengi na ya
kuzunguka alithibitisha kuwa alichokifanya Msaidizi wake yalikuwa
maelekezo ya Wizara.3 Kwa kuzingatia uhaba wa muda wa
kukamilisha kazi ya Kamati Teule na kwamba suala hilo tayari
lilikuwa limechukua siku tatu nzima za Kamati Teule, ugeni wa
Katibu Mkuu huyo katika Wizara hiyo na katika masuala ya Bunge na
uwezekano uliokuwepo kwa Kamati Teule kupata taarifa za ziada
kupitia njia nyingine, Kamati Teule iliamua kusonga mbele na
kumuacha Katibu Mkuu huyo na siri kubwa za Wizara yake.
Pamoja na changamoto hizo, Kamati Teule iliona kuwa ni vyema
baadhi ya Wajumbe waende Houston, Texas, Marekani ili kupata
taarifa za kina na za ziada kuhusu suala hilo. Kamati Teule
inamshukuru sana Mhe. Spika kwa kuzielewa changamoto zilizokuwa
zinaikabili Kamati Teule na kuwawezesha Wajumbe watatu kwenda
Washington DC kukutana na maafisa wa Ubalozi wetu, na Houston
Texas kukutana na wamiliki wa Richmond Development Company
LLC. Wajumbe hao walioondoka Dar-es Salaam kwenda Marekani
tarehe 10 Disemba 2007 ni:
(a) Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, Mb
(b) Mhe. Lucas Lumambo Selelii, Mb
(c) Mhe. Mohamed Habib Juma Mnyaa, Mb, na
(d) Ndugu Anselm L. Mrema (Katibu wa Kamati)
3 Taarifa Rasmi za Bunge, HANSARD ya tarehe 19/12/ 2007 – Mahojiano na Ndugu Mwakapugi.
8
Tarehe 12 Disemba 2007 Kamati Teule ilimwandikia barua Mhe.
Spika kumuomba aiongezee muda kwa sababu kuu mbili: Kwanza,
Wajumbe watatu kati ya watano na Katibu wa Kamati Teule
walikuwa nchini Marekani kuanzia tarehe 10 Disemba 2007
kujiridhisha na taarifa mbalimbali ambazo Kamati Teule imekuwa
ikizipata kuhusu Richmond Development Company LLC. Kwa kuwa
Wajumbe hao walikuwa wanategemea kurejea nchini tarehe 15
Disemba 2007 siku ambayo Kamati Teule ilitakiwa kuwasilisha
taarifa yake kwa Mhe. Spika, na pia taarifa ambazo wangezipata
Marekani zingetakiwa kuingizwa kwenye taarifa ya Kamati Teule na
hata kubadilisha baadhi ya masuala katika taarifa hiyo.
Pili, baada ya uchambuzi wa kina wa ushahidi wa maandishi na wa
mdomo uliotolewa mbele ya Kamati Teule chini ya kiapo, Kamati
Teule iligundua kuwepo kwa mgongano wa ushahidi, hivyo kutia
mashaka juu ya dhamira ya baadhi ya mashahidi. Kamati Teule
iliona umuhimu wa kuwaita tena baadhi ya mashahidi kuthibitisha
kauli zao, na hata kuwachukulia hatua za kisheria baadhi yao ambao
wangeendelea kusema uongo chini ya kiapo ili kulinda heshima ya
Bunge.
Mhe. Spika aliona umuhimu wa kuiongezea Kamati Teule muda,
hivyo tarehe 13 Disemba 2007 akaridhia ombi la Kamati Teule na
kuweka tarehe 31 Disemba 2007 kuwa tarehe ya kuwasilisha taarifa
ya uchunguzi. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku
9
ilipowasilisha taarifa yake kwa Mhe. Spika, Kamati Teule ilikuwa
imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na
kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao
walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7
waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe.
Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati
Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.
Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu
msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company
LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu
mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza
mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo
ya kina ya mradi huu yako sehemu ya sita ya taarifa hii. Mhe.
Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na
Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans
Holdings S.A baada ya mashahidi zaidi ya watano kumtaja kuwa ana
uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwanini
anwani ya posta na anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya
Caspian Construction Company Ltd inatumiwa na Dowans Holdings
S.A. Kamati Teule ilipata majina ya baadhi ya wafanyakazi wa
Caspian ambao pia wanaitumikia Dowans Holdings S.A.
10
2.0 UKAME NA TATIZO LA UZALISHAJI UMEME NCHINI
2.1 Taarifa za Awali na Hatua za Serikali
Kwa takribani miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2002 nchi
yetu ilikumbwa na tatizo la ukosefu wa mvua za kutosha. Athari za
tatizo hilo hasa katika uzalishaji umeme, zilianza kuonekana mwaka
2004, na kufikia mwishoni mwa mwaka 2005 ikawa dhahiri kwamba
nchi ilikuwa inaelekea kwenye janga kubwa la upungufu wa umeme.
Mahitaji ya mitambo ya gesi ya kuzalishia umeme wa dharura
yakajitokeza.
Kutokana na hali hiyo, mwezi Disemba 2005, TANESCO iliiomba
Serikali kufikiria na kuidhinisha mpango wa kukodisha mitambo ya
kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi kutoka kwenye
makampuni yanayofahamika kwa biashara hiyo chini ya Mikataba ya
kuuziana umeme kwa muda usiopungua miezi kumi na mbili.
Tarehe 28 Disemba 2005 Serikali ilikubali ombi hilo na kuiruhusu
TANESCO kuwasiliana moja kwa moja na kampuni ya Songas kuhusu
mahitaji hayo ya dharura ya nchi. Bila kuchelewa TANESCO
wakawasiliana na Songas ambayo ikaanza mara moja kuandaa
makisio ya mradi huo. Tarehe 11 Januari 2006, CDC Globeleq,
kampuni mama ya Songas, iliwasilisha TANESCO makisio ya
kukodisha mitambo ya gesi ya kuzalisha umeme wa MW 74 ambayo
ingefungwa Ubungo na kuanza kuzalisha umeme katikati ya mwezi
Aprili 2006.
11
Tarehe 13 Januari 2006 Bodi ya Zabuni ya TANESCO ilianza kujadili
zabuni hiyo ya CDC Globeleq na siku sita baadaye, yaani tarehe 19
Januari 2006, Bodi hiyo ikathibitisha mapendekezo ya zabuni hiyo
na kuingia katika majadiliano na CDC Globeleq. Tarehe 30 Januari,
2006 Bodi ya Zabuni ya TANESCO iliyakubali mapendekezo ya Kamati
ya Tathmini ya kuingia mkataba wa uzalishaji umeme kwa miaka
mitano au mitatu kama ifuatavyo: (i) miaka mitano kwa bei ya senti
za Kimarekani 3.2/kWh; au (ii) miaka mitatu kwa bei ya senti za
Kimarekani 5.3/kWh. Chini ya mpango huo, mitambo hiyo ya
kuzalisha umeme ingekuwa mali ya TANESCO baada ya kipindi cha
kukodi kumalizika.4
Taarifa hizi pamoja na mapendekezo ya Wizara ya Nishati na Madini
yaliwasilishwa na kujadiliwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri cha
tarehe 10 Februari 2006, yaani siku nne baada ya kuanza mgao wa
umeme kwa mikoa yote ya Tanzania Bara inayounganishwa na Gridi
ya Taifa.
Pamoja na mambo mengine, Baraza la Mawaziri liliiagiza Timu ya
Wataalamu (Technical, Financial and Legal Experts Team) iliyokuwa
inaundwa na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, ishugulikie masuala makuu manne:
4 Waraka wa Baraza la Mawaziri Na. 2/2006
12
(i) ununuzi wa mitambo ya MW 60-100 ambao ungefungwa
Ubungo pamoja na jenereta za mafuta za MW 40 ambazo
zingefungwa Mwanza, Arusha na Moshi kwa kutumia
fedha zilizotegemewa kutoka Mifuko ya Pensheni nchini;
(ii) ukaguzi wa mitambo ya kutoka CDC Globeleq ili
kujiridhisha na hali na ubora wa mitambo hiyo;
(iii) kuitaka CDC Globeleq ikubali kuiuzia Serikali mitambo
hiyo moja kwa moja tangu mwanzo au iikodishe Serikali
kwa bei ambayo Serikali ingeridhika nayo na siyo kwa
kipindi cha miaka mitano bali kipindi kile tu cha
matatizo ya umeme kutokana na ukame;
(iv) kutafuta na kukagua mitambo ya kuzalisha umeme wa
MW 60-100 Ubungo ikiwa ni pamoja na mitambo ya CDC
Globeleq kwa muda mfupi iwezekanavyo ili ipatikane na
kufungwa mara moja kupunguza tatizo la umeme nchini.
Ni dhahiri kuwa kwa maamuzi hayo, Serikali haikutaka kufanya
makosa kwa kuweka mayai yote kwenye kikapu kimoja kutokana na
hali ya kutisha ya upungufu wa nishati ya umeme nchini. Lakini
Kamati Teule imebaini kuwa utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la
Mawaziri haukuwa makini kama inavyoelezwa hapa chini.
Siku hiyo hiyo ya tarehe 10 Februari 2006, Wizara ya Nishati na
Madini, badala ya kuwatumia ujumbe sahihi CDC Globeleq kuwa
Serikali inataka wapunguze kipindi cha ukodishaji mitambo,
washushe zaidi bei yao ya umeme na wawe tayari kuzalisha umeme
13
ifikapo Mei 2006, ilipeleka ujumbe tofauti kabisa kuwa Serikali
inafuta mpango wa kukodisha mitambo kutoka kwao. Sehemu ya
barua hiyo iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu
Arthur Mwakapugi, ikijibu barua iliyoandikwa na CDC Globeleq
kwenda kwa Waziri Mkuu, inasema:
"I wish to inform you that despite the progress you have so
far made in effecting the project, the Government has
decided to cancel the leasing of the plant and instead will be
provide (sic) funds to TANESCO to procure, install and
commission a similar plant".5 (Napenda kukufahamisha kuwa
licha ya maendeleo mazuri mliyoyafanya katika kutekeleza
mradi, Serikali imeamua kufuta ukodishaji wa mtambo na
badala yake itaipatia TANESCO fedha za kununulia, kufunga na
kuzindua mtambo wa aina hiyo hiyo).
Pamoja na kumhoji aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kipindi
hicho Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha, (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Ndugu Arthur Mwakapugi kwa muda mrefu na katika siku nne tofauti,
Kamati Teule imeshindwa kupata majibu ya uhakika kwa maswali
yake manne:
(i) Je, kulikuwa na kikao kingine cha Baraza la Mawaziri siku hiyo
hiyo ya tarehe 10 Februari, 2006 kilichotengua maamuzi yake
ya awali ya siku hiyo hiyo?
5 Barua kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Kumb. Na. CBD.286/397/01 ya tarehe
10/02/06.
14
(ii) Ikiwa jibu ni hapana, kwa nini Wizara ilipeleka CDC Globeleq
ujumbe tofauti na ule ilioagizwa na Baraza la Mawaziri?
(iii) Kwa nini Wizara isitume barua hiyo baada ya kushindwa
kuwashawishi CDC Globeleq kubadilisha masharti yao?
(iv) Maamuzi kama hayo, siku nne ndani ya mgao wa umeme wa
nchi nzima na katika kipindi ambacho Serikali haikuwa na
mkakati mbadala uliokuwa umeiva kama wa CDC Globeleq,
yalikuwa kweli maamuzi makini ya kunufaisha Taifa?6
Kutokana na msimamo huo mpya wa Wizara, TANESCO ikaachana na
mpango wa kukodisha mitambo na kuelekeza nguvu zake kwenye
kununua mitambo mipya ya kuzalishia umeme. Hivyo, tarehe 20
Februari 2006, TANESCO iliwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini mpango wa ununuzi wa moja kwa moja kutoka
kwa watengenezaji wa mitambo ya kuzalishia umeme
wanaofahamika duniani chini ya utaratibu unaotambuliwa kama
international shopping chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya
mwaka 2004 na Kanuni zake.
Hatua hiyo ikafuatiwa na kikao cha Waziri wa Nishati na Madini na
watendaji wa Wizara na TANESCO tarehe 21 Februari 2006 ambacho
Waziri alikitumia kusisitiza kuwa mpango wa Serikali si kukodisha
mitambo bali kununua. Hivyo akaiagiza TANESCO kutangaza mara
moja zabuni ya kununua mitambo mipya au iliyotumika ya kuzalishia
6 Taarifa Rasmi za Bunge, HANSARD za tarehe 4, 7, 10 na 19/12/07.
15
umeme ama sivyo hatua kali za kinidhamu zingechukuliwa dhidi ya
viongozi wa shirika.7
Waziri alitaka tangazo la zabuni lichapishwe magazetini siku ya
Alhamisi tarehe 23 Februari 2006 na kuwapa TANESCO masharti
yafuatayo kwa zabuni hiyo: (i) ifunguliwe baada ya siku 10 (yaani
tarehe 6 Machi 2006); (ii) tathmini ya zabuni ifanyike kwa siku mbili
(tarehe 7 - 8 Machi 2006). Aidha, Waziri alitaka Kamati ya
Kutathmini Zabuni iongozwe na TANESCO lakini iwe na wajumbe
wengine kutoka Hazina, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Mifuko ya Pensheni na Wizara ya Nishati na Madini.8
2.2 Maandalizi ya Zabuni
Tarehe 22 Februari 2006 TANESCO iliomba idhini ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kutangaza zabuni hiyo kwa
muda wa siku 10 badala ya siku 45 zinazoainishwa katika Kanuni za
Ununuzi.9 Tarehe hiyo hiyo ya 22 Februari 2006, PPRA ikaijibu
TANESCO kwa kuitahadharisha kuwa utaratibu huo utakuwa kinyume
cha taratibu na Kanuni za ununuzi. Muda wa siku 10 hautoshi
kuitisha zabuni ya kimataifa na kuweza kupata wazabuni wenye sifa
zinazohitajika.
7 Muhtasari wa kikao cha tarehe 21/02/06.
8 Angalia Na.7
9 Barua Kumb. Na.DST/18/49 ya tarehe 22/02/06
16
Mamlaka ikaishauri TANESCO kuwa badala ya kutumia njia ya
kutangaza zabuni ya kimataifa (international competitive
tendering) itumie njia mbadala ya ununuzi wa kimataifa
(international shopping) ambapo makampuni mengi
yanayotengeneza mitambo ya kuzalisha umeme yanaalikwa na
"kuyashindanisha kwa kuyaomba yawasilishe zabuni zao badala ya
kutangaza kwani utaratibu huo ungesaidia kuondoa makampuni ya
kati yasiyohusika na uzalishaji umeme".10
Tarehe hiyo hiyo 22 Februari, 2006 TANESCO ikaiarifu Wizara kuhusu
ushauri wa PPRA. Wizara iliukataa ushauri huu na kuiagiza TANESCO
kutekeleza agizo la Waziri bila kukosa kwa kuitangaza zabuni hiyo.
Zabuni hiyo ikatangazwa kwa utaratibu wa ndani tarehe 23 Februari
2006. Hatua hiyo iliishitua PPRA ambayo iliiandikia barua TANESCO
kuelezea kushangazwa kwake na hatua ya shirika hilo kukaidi
ushauri wa kitaalamu na wa kisheria. PPRA ikasisitiza kuwa, njia
pekee kwa TANESCO kupata wazabuni wazuri na wenye sifa stahili
katika kipindi kifupi ni kutumia utaratibu iliyoupendekeza wa
international shopping.11
Hali ya uzalishaji umeme nchini iliendelea kuwa tete na kulazimu
kikao cha Baraza la Mawaziri kufanyika tarehe 23 Februari 2006, na
kuagiza utaratibu wa haraka (fast track) wa kukodi mitambo ya
kuzalishia umeme wa dharura ufanyike. Baraza liliagiza kuwa,
10 Barua Kumb. Na. PPRA/TANESCO/41/16 22/02/06
11 Barua Kumb. Na. PPRA/TANESCO/41/18 ya 23/02/06
17
katika kutekeleza maamuzi haya, Sheria ya Ununuzi wa Umma ya
mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005 zizingatiwe. Pamoja na
msisitizo huo wa Baraza la Mawaziri, Wizara ya Nishati na Madini
ikaendelea kuishinikiza TANESCO kufuata maagizo ya Wizara na si
vinginevyo.
Jumapili tarehe 26 Februari 2006 TANESCO ikionyesha dhahiri
kusukumwa tu na Wizara, ikaiandikia tena barua PPRA kuelezea
kuwa sasa imeagizwa na Serikali kuitangaza zabuni hiyo magazetini,
hivyo mamlaka hiyo ya udhibiti wa ununuzi wa umma itoe idhini ya
kutangaza zabuni ya kimataifa kwa siku chache kuliko zilizowekwa
na sheria.12 TANESCO huku ikijua kabisa kuwa PPRA isingeweza
kuipata na kuijibu barua hiyo Jumapili, ikatangaza zabuni hiyo
magazetini tarehe 27 Februari 200613 na kuwataka wazabuni
wawasilishe zabuni zao tarehe 6 Machi 2006 yaani siku 10 baada ya
kuchukua nyaraka za zabuni tarehe 24 Februari 2006.
Tarehe 1 Machi 2006 PPRA ikaijibu TANESCO kuwa pamoja na
kuendelea na zabuni hiyo, isingekuwa rahisi kwa Shirika hilo la
umeme la Taifa kupata mzabuni anayefaa katika kipindi hicho kifupi
cha siku 10. Hata hivyo PPRA ikaitaka TANESCO kuufuatilia utaratibu
mzima wa zabuni hiyo kwa karibu ili kuhakikisha kuwa taratibu
12 Barua Kumb. Na.DST/18/50 ya tarehe 26/02/06
13 Gazeti la DAILY NEWS tarehe 27/02/06
18
zinafuatwa, ili kuepusha malamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa
wazabuni.14
Pamoja na kuipongeza PPRA kwa kuonesha subira ya hali ya juu,
uwazi na ukweli wa kitaaluma, Kamati Teule ilishindwa kubaini
chanzo cha ujasiri wa kiburi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini
kiasi cha kupindisha maamuzi ya Baraza la Mawaziri kama
tulivyoona pamoja na kukaidi ushauri wa Mamlaka zilizopo kisheria.
2.3 Mchakato wa Zabuni ndani ya TANESCO
Ili kupata muda zaidi wa zabuni ililazimu muda wa zabuni
kuongezwa hadi tarehe 20 Machi 2006 ambapo jumla ya wazabuni
ishirini na sita (26) walinunua nyaraka za zabuni zilizouzwa kwa
fedha isiyorejesheka (non refundable) ya Dola za Kimarekani 100.
Ni wazabuni wanane (8) tu ndio waliorudisha nyaraka za zabuni hiyo
kama ifuatavyo:
(i) M/S Aggreko International Projects Ltd ya Uarabuni,
(ii) M/S Quantus ya Ujerumani,
(iii) M/S APGUM Co. Ltd ya Ujerumani,
(iv) M/S Globeleq Ltd ya Kanada,
(v) M/S Real Energy Projects ya Uingereza,
(vi) M/S Renco SPA ya Italia,
(vii) M/S Richmond Development Company LLC ya Marekani, na
(viii) M/S GAPCO(T) Ltd ya Tanzania.
14 Barua Kumb. Na. PPRA/TANESCO/41/21 ya tarehe 01/03/06
19
Zabuni zikafunguliwa. Wazabuni wote waliorudisha nyaraka zao za
zabuni waliwakilishwa kwenye ufunguzi. TANESCO ikaunda Kamati
ya Kutathmini Zabuni iliyokuwa na wajumbe 12, kati yao wanane
walitoka TANESCO, wawili kutoka kampuni ya ushauri ya Lahmeyer
International, mmoja kutoka Wizara ya Fedha na mwingine Wizara
ya Nishati na Madini. Kamati hiyo ilipewa wiki moja tu kumaliza kazi
yake na kuiwasilisha taarifa ya tathmini kwenye Bodi ya Zabuni ya
TANESCO tarehe 28 Machi, 2006.
2.3.1 Vigezo vya Tathmini (Preliminary Evaluation)
Kamati ya Tathmini ilitumia vigezo vifuatavyo kupima uwezo wa
mzabuni:
(i) Muda wa kuleta mtambo na kuanza kazi,
(ii) Dhamana ya zabuni (Tender Security),
(iii) Kipindi cha mchakato wa Zabuni (Tender Validity),
(iv) Uwepo wa mitambo na uwezekano wa kusafirishwa,
(v) Uzoefu wa mzabuni kutekeleza na kuendesha mitambo ya aina
hiyo,
(vi) Kibali cha mtengenezaji wa mitambo,
(vii) Uwezo wa kupata mkopo,
(viii) Mapato (turnover)
(ix) Uzoefu na sifa za kiufundi za mzabuni,
20
(x) Viambatisho vya idhini ya kisheria vya kuweza kutoa maamuzi
ya mwisho (Power of Attorney)
(xi) Hati iliyotiwa saini ya mwakilishi wa kisheria wa mzabuni,
(xii) Hati iliyotiwa saini ya mwakilishi wa kisheria wa mtengenezaji
wa mitambo,
(xiii) Hati ya nchi anayotoka mzalishaji wa mitambo,
(xiv) Uwepo wa maelezo ya lazima ya kiufundi,
(xv) Barua ya dhamana kwa ajili mahitaji ya kiufundi na ubora wa
bidhaa inayotolewa na mtengenezaji wa mitambo,
(xvi) Ujazaji fomu ya zabuni kikamilifu,
(xvii) Mchanganuo wa bei/gharama ya umeme,
(xviii) Uhakika kuwa wakala/ kuwa na uwezo wa kufanya
matengenezo na kuwa na vipuri, na
(xix) Muda wa kukodisha mitambo.
Matokeo ya uchambuzi wa zabuni zote nane yalionesha kuwa hakuna
mzabuni hata mmoja aliyetimiza au kukidhi vigezo vya zabuni
vilivyowekwa (non responsive). Kutokana na hali mbaya ya
uzalishaji umeme nchini, Kamati ya Tathmini ikalazimika kuondoa
zaidi ya nusu ya vigezo na kuvibakiza tisa tu ilivyoviona kuwa ni
muhimu sana kwa ngazi ile ya uchambuzi ili kumpata mshindi katika
kundi hilo la wazabuni wanane. Vigezo vilivyobakizwa ni:

21
(iii) Uwepo wa mtambo tayari kuletwa Tanzania,
(iv) Uzoefu wa mzabuni kutekeleza miradi/ kuendesha mitambo ya
aina hiyo,
(v) Uzoefu na sifa za kitaaluma/ kiufundi za mzabuni