Dowans lazima walipwe

Hakilipwi kitu hapa, nyie njooni na propaganda zenu za ajabu, eti kuperform, kuperform kitu gani bana?


SASA KAMA TANESCO WALIPOKEA UMEME WA KAMPUNI FEKI WEWE KAMA JAJI UNAAMUAJE?KUILIPA KAMPUNI FEKI ILIYOZALISHA UMEME AU KUWALIPA TANESCO WALIOFURAHIA UMEME WA KAMPUNI FEKI NA KUWAUZIA WATANZANIA MASKINI KWA BEI YA JUU Na TENA KWA MGAO???
RACK U R BRAIN
 

Crap al Pumba
 
Ina maana hii ndio kesi ya wanaharakati au?

 
Dowans watalipwa ila kweli ccm imetufunza adabu watanzania
 
Ah ah, son of soil , umetumwa uje upige debe au? kulipa hatulipi na pia waliotuingiza mkenge tunawashughulikia. Kama noma na iwe noma.
 
Dowans wanapaswa kuwabana richmondi, kwa kuwa richmondi iliingia mkataba nao bila kumuhusisha mdau wa pili yaani tanesco, bila shaka mkataba ambao TANESCO iliingia na dowans ni mkataba batili na wa kulipa siyo tanesco bali richmondi
 
 
Dowans wanapaswa kuwabana richmondi, kwa kuwa richmondi iliingia mkataba nao bila kumuhusisha mdau wa pili yaani tanesco, bila shaka mkataba ambao TANESCO iliingia na dowans ni mkataba batili na wa kulipa siyo tanesco bali richmondi

SOMA RIPOTI YA MWAKYEMBE USIKURUPUKE;DOWANS NA TANESCO WALIINGIA MKATABA HALALI

Kamati Teule haikufanikiwa kupata majibu ya Citibank ila iliambiwa kulikuwa na shinikizo toka Wizarani "kuwa viongozi wa Wizara kama kawaida yao waliishinikiza TANESCO kukubaliana na ombi la Richmond Development Company LLC la kuhamisha mkataba." Ni kutokana na hilo tarehe 21 Disemba, 2006 TANESCO ikaiandikia kampuni ya Richmond kukubali uhaulishaji wa mkataba huo kwenda kwa Dowans kwa barua yenye SEC. 388/12/206 ambapo pamoja na mambo mengine ilitaka "ipate hati ya uthibitisho kutoka Dowans Holdings, S.A ya kuridhia uwajibikaji kamilifu katika kutekeleza Mkataba wa tarehe 23 Juni, 2006, kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC."

Hivyo tarehe 23 Disemba 2006 Mkataba ukaingiwa kati ya TANESCO na Dowans S.A ambao ulikuwa ni kuhamishia mkataba kati ya TANESCO na Richmond kwenda kwa Dowans Holdings S.A.

 
 
No way out the payment must be DONE! Ila kama alivosema mtoa mada waliohusika kutuingiza katika hii Mess waadhibiwe...
 

Mbona umekazana tuwalipe tuwalipe kwani na wewe wanakulipa ngapi?
 
Hebu angalia hii kitu kutoka Thread ya Mwanakijiji ndo labda utaelewa ninasema nini.

Kuna mambo ambayo tuna uhakika nayo na ambayo ni msingi wa hatimaye kukataa kuwalipa Dowans S.A na Dowans Tanzania Limited tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC). Mambo yafuatayo ni ya kuzingatia.


  1. Wakati Karamagi anawasiliana na Kazaura kuulizia kama mkataba wa Richmond/TANESCO unaruhusu kuhamishika alikuwa tayari na taarifa kuwa Richmond walikuwa tayari wameshahamisha mkataba kwenda Dowans, SA Oktoba 14,2006 (mwezi mmoja na nusu kabla)
  2. Majibu ya TANESCO siku ile ile kwenda kwa Kazaura ikitaja uwepo wa kifungu cha 15.12 kwenye mkataba kinachozuia kuhaulisha mkataba bila ya ridhaa ya maandishi toka kwa TANESCO inatuonesha kuwa TANESCO walikuwa hawajui kuwa Richmond walikuwa tayari wamehamisha mkataba wao kwenda Dowans Holdings S.A Oktoba 14, 2006
  3. TANESCO wakiwa wamepewa jina la kampuni iliyokusudiwa kuhamishiwa mkataba ya Dowans S.A wanawasiliana na wawakilishi wa kampuni hiyo ili kupata taarifa za uwezo na uhalisia wa kampuni hiyo kuweza kuchukua mkataba. Na wanawaandikia barua Citibank ili iwasadie kufanya uchunguzi wa uhalisia na uwezo wa kampuni hiyo. Barua hiyo inaandikwa Novemba 8, 2006. Barua hiyo aidha haijibiwi au hakuna ushahidi wa kuwepo kwa majibu yake.
  4. Novemba 9, 2006 kampuni ya Richmond wanawaandikia barua rasmi TANESCO kuwajulisha nia yao ya kutaka kuhamisha mkataba kwenda kampuni nyingine wakitumia haki yao ya kifungu cha 15.12 cha Mkataba. Hii ndiyo barua ambayo inawafikia TANESCO Disemba 4, 2006. Hapa kuna jambo la kutafakari kidogo. Kwanini barua iliyoandikwa Novemba 9, 2006 iwafikie TANESCO Disemba 4, 2006? Yawezekana iliandikwa baada ya kugundua kuwa mkataba umeshahamishwa kwa Dowans S.A Oktoba 14, 2006 lakini TANESCO hawakuwa na taarifa hivyo walihitaji kutengeneza mazingira ya taarifa?
  5. Pendekezo la nne hapo juu linaonekana lina ukweli kwa sababu ni tarehe 28 Novemba, 2006 ndipo Karamagi anaulizia kama mkataba unaruhusu kuhamishika; na anapoambiwa kuwa haiwezekani isipokuwa kwa ridhaa ya pande zote mbili chini ya kifungu 15.12 ndipo siku sita baadaye (Disemba 4, 2006) barua iliyoandikwa Novemba 9, 2006 inafika TANESCO ikiwa na nia ya ya kuhamisha mkataba chini ya haki za 15.12. Barua hiyo ya Richmond ilisema kuwa kampuni iliyokusudiwa ilikuwa ni Dowans S.A na kuwa kampuni hiyo mpya itajitambulisha yenyewe kwa TANESCO.
  6. Novemba 14, 2006 Dowans S.A inawaandikia TANESCO ikijitambulisha kuwa ndiyo kampuni ambayo imekusudiwa kurithi mkataba wa Richmond na TANESCO. Wakati Dowans S.A inaandika barua hii tayari ilikuwa imeshaingia mkataba na Richmond Oktoba 14, 2006. Lilikuwa jukumu la Richmond na Dowans S.A kuitaarifu TANESCO kuwa mkataba umekwishachukuliwa. Hilo hata hivyo lingekuwa kinyume na kifungu cha 15.12. Dowans iliandika barua kana kwamba ilikuwa haijachukua mkataba huo bado na hivyo kudanganya ili kupata faida ya aina fulani kinyume na sheria yetu ya Mikataba ya 2002. Kuna mambo ambayo TANESCO ingeweza kujua kuhusu kampuni ya Dowans lakini suala la kuwa ilikuwa tayari imekwishaingia mkataba lilikuwa ni suala la kujulishwa na Richmond au Dowans wenyewe. Ni sawasawa na mtu ambaye kwa muda wote wa uchumba na hatimaye siku ya harusi anafunga ndoa akiamini kuwa anayefunga naye ndoa hakuwa tayari amefunga ndoa na mtu mwingine ambayo ilikuwa bado halali kisheria. Ndoa inaweza kufungwa lakini endapo ikaja kujulikana kuwa yule mwingine alificha ukweli kuwa tayari alikuwa katika ndoa halali basi ile ndoa ya pili inafutiliwa mbali (annulled) kwani haikuwahi kuwepo.
  7. Barua ya Dowans ya Disemba 8, 2006 inaondoa shaka kabisa kuwa Dowans waliwaficha TANESCO ukweli kuwa tayari kampuni ya Costa Rica ilikuwa tayari imekwisha funga “ndoa” na Richmond kuchukua mkataba wake na TANESCO bila ridhaa ya kimaandishi na TANESCO. Barua hii kwa mujibu wa hukumu ya ICC (kifungu cha 517) iliomba kibali cha kuhamisha mkataba na kutoa taarifa mbalimbali kuhusu kampuni hiyo na kampuni ya Portek Group.

MY TAKE:
Sasa Swali ni hili: Mkataba kati ya Richmondi na Tanesco unatamka wazi kwamba Huwezi kuhamisha majukumu ya mkataba kwenda kwa kampuni nyingine bila kumhusisha partner mwingine(ambaye this time ni Tanesco), ukifanya hivyo unakuwa umevunja mkataba.

Sasa ishu hapa ni hii, kwa kuwa Richmond "Unilaterally" waliamua kuingia mkataba na Dowans bila kuihusisha Tanesco ni dhahiri kwamba mkataba baina ya Richmond na Tanesco ulishakuwa Void tangu siku hiyo waliposaini kimya kimya!, na hivyo ni dhahiri huwezi kuhamisha mkataba Void halafu ukataka uonekane ni mkataba valid mbele ya Sheria, basi Tanesco hawawajibiki kuilipa Dowans, bali Richmond ndo wanapaswa kumlipa Dowans!.
 
No way out the payment must be DONE! Ila kama alivosema mtoa mada waliohusika kutuingiza katika hii Mess waadhibiwe...

duu..... huyu nae anaitwa leftbrain....yule chizi mwingine ni nani tena... GB

products zenu zinafanana kama majina yenu..... pumba
 
Ah ah, son of soil , umetumwa uje upige debe au? kulipa hatulipi na pia waliotuingiza mkenge tunawashughulikia. Kama noma na iwe noma.

Mimi nimemstukia zamani, wameishaambiwa kuwa Jamii Forums ikichakachuliwa tu watalipana. Data zote zinatoka hapa. sasa wanajaribu kutuchanganya. Halipwi mtu. Ukiona mtu anasema "Upende usipende" ujue ni walewale. ndiyo lugha zao hizo. Je wanataka kutuambia akina Sita na Mwakyembe ambao ni wanasheria hawajui ukweli? Kama kampunu ni hewa, itakuja kushika mali kwa uhalali gani? Kwanza tunataka kujua uhalali wake mengine yatafuata baadae.
 
NCHI HII INA HELA NYINGI SANA!!!!!?????
Wewee tusubiri uamuzi wa mahakama kuu. Acha kuchakachua akili za watz.
 
No way out the payment must be DONE! Ila kama alivosema mtoa mada waliohusika kutuingiza katika hii Mess waadhibiwe...
Wenzetu wa West Africa esp Ghana wana utaratibu kuwa mtu akifa basi hawaziki kwa haraka mpaka wahakikishe ya kwamba familia anayoiacha marehemu i salama (basi kama ni nyumba itajengwa na watoto watatafutiwa fedha za kusomea, kula nk). Wanafanya hivyo makusudi kuwa mara tu utakapo harakisha kumzika marehemu ni kawaida ya wanadamu kusahau kila kitu instantly. Bearing this in mind I think it is not right to hasten Dowans payment until we're sure beyond reasonable doubts that every single truth has been unearthed. If and only if we get our facts right then we can pay or not pay Dowans and hang responsible culprits. Nothing more nothing less.
 

hatutawalipa leo kesho wala baadae, hatutawalipa milele, hiyo ya kuja kulipa eti baadae na riba ni sisi wenyewe tukiamua, na tukiamua vilevile hatutawalipa pia..wee unaogopaaa..hatulipi kamwe, na take my words, wakilipa hii ngawira hapakaliki hapa....msione watu tuko kimya mkadhani mafala..si mmena misri, yemen na tunisia..bongo inakuja..tunahitaji watu wachache tuu wa kulianzisha then tunamwagika street wote mpaka wakome..we already have enough number of pipo who are willing to start a movement...
 
Kombi ya dowans haijabalance inabidi wareseat!, hapewi mtu feki hapa!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…