DOWANS! DOWANS! Angalieni hii hotuba ya March 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DOWANS! DOWANS! Angalieni hii hotuba ya March 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DoubleOSeven, Mar 8, 2011.

 1. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii hapa chini ni ya 2009
  Nakumbushia kwamba leo hii bado tupo gizani. Yale ya Babu wa Loliondo yametawala as if tumeacha mambo ya msingi tukashabikia ya kijinga kwelikweli. Anyway, hebu someni hii!  Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

  "Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

  Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

  Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.

  Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

  Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

  Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

  "Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana. Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

  Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla. "Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema.


  source:HabariLeo | JK apigilia msumari wa mwisho Dowans (April 2nd, 2009)
   
 2. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwenyewe ameshasahau....kama vile watanzania tulivyokuwa warahisi kusahau.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ndo maana siku hizi huwa simsikilizi kabisaaa!
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Rais akidanganya tumfanye nini? Kikwete alitudanganya, Ngeleja ametudanganya sasa tuwafanyeje hawa jamani?????
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hakuna tiba ya kifo
   
 6. N

  Njaare JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu umenifurahisha sana kwa kutukumbusha hii ahadi ya JK. Sasa tunawaomba Pinda na Ngeleja watuambie kama rais alighafilika alivyosema uamuzi wa TANESCO ni wa Busara. Au Tanania daima ikanushe kuwa rais hakutamka hayo.
   
 7. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,230
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Tatizo hivi vyombo vyetu vya habari huna navyo havina kumbukumbu, kimsingi ndio vilitakiwa viwe vinawakumbusha wananchi hizo ahadi hewa za Rais wao. lakini wakishatoa habari mpya za zamani wanazifutulia mbali.

  Itapendeza kama akina Mwana halisi watakuwa wanatutolea marudio ya hotuba za JK zinazotoa taarifa kinzani kama hizi ili wananchi wajue ni jinsi gani wana rais Bogasi asiejua anachoahidi na kinachotekelezwa.

  Hadi usawa huu Rashid was right kuwa nchi itaingia gizani na kweli imekuwa. Hapo imethibitisha kuwa mtaalam na mwanasiasa ni watu wawili tofauti sana na siku zote mara nyingi mtawala mwanasiasa huwa ni muongo.
   
Loading...