Dovutwa yupo Eatv

Kilaza

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
3,318
0
wakuu

Namsililiza hapa huyu aliyekuwa Mjumbe wa bunge la katiba na mwenyekiti wa UPDP Fahami Dovutwa katika kipindi cha hotmix cha EATV

licha ya kuwa mtangazaji hana uelewa mzuri wa katiba lakini maswali yote anayoulizwa mzee wetu Dovutwa hajibu sanasana tu na yeye anamuuliza maswali tena mtangazaji

na jibu lake kubwa kwenye karibia kila swali anajibu"Tumeondoa ubaguzi alioupandikiza warioba na tume yake"

lakini kilichonishangaza zaidi ni mzee wetu kuulizwa swali na mtangazaji kuwa "kama wabunge wote wakichaguliwa hawana elimu na katiba pendekezwa inataka mbunge awe waziri na waziri lazima awe na degree itakuwaje" mzee wangu dovutwa akaishia kusema embu mtafute Mama mery amesoma sana kuliko tume yote ya warioba anaweza kukujibu....

mimi nimeshindwa kumuelewa huyu mzee anamatatizo gani ya Akili???

hivi kweli huyu ndiye aliyegombea urais 2010 ..!! Na kuna wananchi wakampigia kura....??

Mwisho wa mjadala akasema atakayetaka kugombea urais kwenye "Genge"lake la UPDP atakuwa ADUI wake wa kudumu kwakua anamzuia yeye kwenda ikulu

kwakweli kama bunge letu "Tukufu"la katiba lilishesheni vihiyo kama hawa Tusitegemee chochote cha maana kutoka kwenye katiba iliyopendekezwa...


.........
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
16,273
2,000
Hili suala la Elimu ni muhimu sana aiseee yaani wakipita wote elimu ya kujua na kusoma tu cjui mawaziri watatoka wapi? Au itafikA sehemu mawaziri wa kubadiri nafasi za mawaziri wanaojiuzuru hawatakwepo.
 

MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,881
2,000
Kilaza bora usingesema ujinga aliosema ili nisijue
 
Last edited by a moderator:

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,221
2,000
Kilaza unatakiwa uwashangae hao EATV kwa kumwingiza studio tahira aisiyejitambua
 
Last edited by a moderator:

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,215
2,000
Anapolipwa mshahara huwa anampa Mama Mary sehemu ya mshahara wake au hamlipi?

Mbona kwenye kazi anakuwa tegemezi hivyo?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,215
2,000
Kilaza unatakiwa uwashangae hao EATV kwa kumwingiza studio tahira aisiyejitambua

Huyo ni mbunge, wa kushangaliwa zaidi ni aliyemteua kuwa mbunge.

Inawezekana EATV nia yao ni kutaka kuonyesha wabunge walivyo watupu.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,215
2,000
Kumbe kuna wabunge huko hawampiti "Le Mutuz"?

Mnataka kuniambia bora hata Lodi Lofa Le Mutuz angeweza kuleta ajira kutoka New York ma'men yu'nowwhatIamsayyyin?
 

Eliah

Member
Jun 8, 2009
32
70
Duh aisee pia nimesikia huyu mzee hiv punde, kwa kifupi dovutwa anapelekeshwa na njaa tu km umemsikia anadai pia chama chao kipewe ruzuku, halafu ajajibu hoja alizoulizwa, japo mtangazaji pia yuko sharo maana alipaswa kumbana aweze kujibu ni aidha kakimbia swali au hajui kabisa kinachoendelea.

Mimi mambo 4 ambayo yananifanya nipigie kura ya hapana ni haya

1. vipindi vya mbunge kukaa madarakani kutokuwa na kikomo
2. kitendo cha wabunge wa zanzibar kuja kutunga katiba inayohusu mambo ya tanganyika
3. viongozi kuweka pesa nje ya nchi
4. elimu ya mbunge nalo ni balaa

kuturaghai kwamba haki za kila kundi zimewekwa halina maana,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom