Dovutwa yupo Eatv

Huyo mzee hajielewi kabisa, aendelee kucheza bao tu, siasa wala haina mashiko nae hata kidogo.
 
wakuu

Namsililiza hapa huyu aliyekuwa Mjumbe wa bunge la katiba na mwenyekiti wa UPDP Fahami Dovutwa katika kipindi cha hotmix cha EATV

licha ya kuwa mtangazaji hana uelewa mzuri wa katiba lakini maswali yote anayoulizwa mzee wetu Dovutwa hajibu sanasana tu na yeye anamuuliza maswali tena mtangazaji

na jibu lake kubwa kwenye karibia kila swali anajibu"Tumeondoa ubaguzi alioupandikiza warioba na tume yake"

lakini kilichonishangaza zaidi ni mzee wetu kuulizwa swali na mtangazaji kuwa "kama wabunge wote wakichaguliwa hawana elimu na katiba pendekezwa inataka mbunge awe waziri na waziri lazima awe na degree itakuwaje" mzee wangu dovutwa akaishia kusema embu mtafute Mama mery amesoma sana kuliko tume yote ya warioba anaweza kukujibu....

mimi nimeshindwa kumuelewa huyu mzee anamatatizo gani ya Akili???

hivi kweli huyu ndiye aliyegombea urais 2010 ..!! Na kuna wananchi wakampigia kura....??

Mwisho wa mjadala akasema atakayetaka kugombea urais kwenye "Genge"lake la UPDP atakuwa ADUI wake wa kudumu kwakua anamzuia yeye kwenda ikulu

kwakweli kama bunge letu "Tukufu"la katiba lilishesheni vihiyo kama hawa Tusitegemee chochote cha maana kutoka kwenye katiba iliyopendekezwa...


.........

Usitupeleke huo samahani Sana!! kumjadili HanaFahamu Dovutwa, mchumia tumbo; ni kulidhulumu taifa muda wa uzalishaji Mali na maendeleo, Ni ufisadi! Kuna mambo muhimu zaidi ya kitaifa ya kujadili kwa maslahi ya Watanganyika, sio huyo, samahani Sana.
 
chizi huyo usirudie tena kupoteza mda kumsikiliza chizi mwenye njaa kama mrema na cheyo.
 
Back
Top Bottom