Double standards kwenye bima za afya, mashirika ya umma yanatumia AAR na zingine binafsi sio NHIF

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,882
6,308
Habari wadau?

Why wafanyakazi wa BOT, TANESCO, TRA wao wanalipiwa bima nzuri za kampuni binafsi na sio NHIF??

Hii ni double standards..

Bila kusahau wafanyakazi wa TANESCO wanapewa units za umeme 700 kila mwezi kwa shilingi elfu 10 tu.

Huku mtanzania maskini anapandishiwa bei za umeme kila kukicha?

Je NHIF ni ya wafanyakazi maskini tu?

Hii sio fair!

halafu wanasema tanesco inapata hasara huku wanajipa umeme wa thamani ya laki mbili kwa shilingi elfu 10 tu... hapo tanesco ina wafanyakazi karibu 5000 huu si ukichaa huu. wakisema hawajui chanzo cha hasara zao...

hili nalo la kumsubiri Donald Trump kweli aseme waafrica hatujui kujiongoza.. na hatuna akili

mtu unamlipa mshahara mamilioni... bado unampa na umeme wa laki mbili au tatu bure.. wakati shirika linajiendesha kwa hasara.. linategemea ruzuku za serikali....

ha ha ha donald trump ni mkweli sana kwamva kuna watu wa iq ndogo sana hasa weusi....

mchawi wa tanesco ni tanesco wenyewe hata waongeze bei ya umeme.. kwa hili la kujipa umeme bure wote hawawezi kuendelea
 
Kwa kweli Mkuu hivi tuseme bila walimu wa msingi kungalikuwapo Ma Engnr na Accountants kweli polen walimu wetu,halafu wenye uwezo wa kujitibia Hosp binafsi ndyo wanapewa AAR makapuku wenye uwezo mdogo NHIF kwa kweli hili liangaliwe upyaa
 
Kwa kweli Mkuu hivi tuseme bila walimu wa msingi kungalikuwapo Ma Engnr na Accountants kweli polen walimu wetu,halafu wenye uwezo wa kujitibia Hosp binafsi ndyo wanapewa AAR makapuku wenye uwezo mdogo NHIF kwa kweli hili liangaliwe upyaa
 
Hii Nchi tunaishi kwa mazoea tu.lakini kuna mengi yanafanyika yanakatisha tamaa.Kama kweli BOT,TRA,TANESCO wanafanya mambo hayo kwa kweli kuna hujuma zinazofanyika ili kudhofisha ustawi wa NHIF. Ukiachia hayo mdau kuna hili swala la mifuko ya jamii, watumishi wake hulipwa mamilioni ya fedha wakati wachangia mwenyewe analipwa kamshahara kadogo .Tumuombe Mungu tu atupe uvumilivu kwani duniani tunapita .
 
Mimi ni rais wa wanyonge!!!
Thubutu!! Gape la walionacho nawasio nacho mpaka kiyama
 
Tanesco wanaomba bei ya umeme iongezwe wakati wao ndio wanachangia shirika kudidimia hivi wafanyakazi wao wanalipwa mshahara halafu bado wanapewa unit za bure nyingi tu halafu ukisikia mashirika yanataka yabinafusishwe wafanyakazi wanakuja juu mara wadai wauziwe hisa utafikiri hayo makampuni waliyarithi kwa wazazi wao, ni kweli mifuko ya hifadhi ya jamii ina tabia ya kujilipa marupurupu makubwa wakati vyanzo vyao vikuu vya mapato ni michango ya wanachama wakati wanachama wakistaafu wanapewa gawio dogo kabisa ila vyama vya wafanyakazi vimekaa kimya kabisa
 
TANESCO ni pepo ndogo hapa nchini. Ukipata ajira Tanesco hesabu umeyakatia "denge"maisha. Bila kusahau majirani wa TRA na BoT. Nyie huko halmashauri endeleeni kuomba. Asanteni.
 
Kila siku tunaomba ili haya yaondoke au ayaone kinyume chake mateso ndio yanaongezeka..mhasibu wa tanesco ana tofauti gani na mhasibu wa halmashauri ya Kakonko?
[HASHTAG]#UsirudieKosa2020[/HASHTAG]
 
tanesco ndio shirika ambalo watanzania wengi hawalipendi...

sababu huduma zenu ni mbovu...

mkitaka tusiwachukie tupeni huduma ya uhakika..

shukuruni sana ni monopoly....ttcl alitesa sana watu miaka hiyo yupo mwenyewe... wamekuja washindani wake nae amejitahidi huduma..

hakuna mtu atakaekupenda kama unatoa huduma mbovu...

hata TFF nayo siipendi sababu haiperform

Kuna mtu TANESCO kakupigia mkeo
sio bure
una chuki binafsi hadi haifichiki

Sasa wakiwa na bima binafsi nayo inakukera?
 
tanesco ndio shirika ambalo watanzania wengi hawalipendi...

sababu huduma zenu ni mbovu...

mkitaka tusiwachukie tupeni huduma ya uhakika..

shukuruni sana ni monopoly....ttcl alitesa sana watu miaka hiyo yupo mwenyewe... wamekuja washindani wake nae amejitah

hakuna mtu atakaekupenda kama unatoa huduma mbovu...

hata TFF nayo siipendi sababu haiperform


Kanywe sumu basi.....
 
Kanywe sumu basi.....

hatunywi sumu ni kutoa feelings zetu hadi mabadiliko yaje...

tuna imani na rais wetu magufuli atasoma malalamiko yetu humu na kuyafanyia kazi... tulianza na mramba ameshawapisha wengine wafanye kazi...

na bado tunaendelea kulalamika mpaka siku tanesco itakapobadilika....

mabadiliko yameanza na mramba.. na nina uhakika tanesco lazima itabadilika kwa kelele zetu mpaka muache kutoa huduma mbovu...


TFF nae ajiandae.... hatuwezi endelea kwa kufurahia watu wasiofanya kazi yao vizuri
 
Back
Top Bottom