Dotto Bulendu: TEF ni jukwaa lisilo na nguvu yeyote kisheria,hawana nguvu kwa mwandishi wala chombo chochote

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Sikuandika chochote kuhusu sakata la mkuu wa mkoa wa Dsm na Jukwaa la wahariri kwa sababu sikuona kama ni jambo linalotakiwa kuteka mijadala ya nchi hii.

Lakini naomba nitoe maoni yangu kuhusu hili kililotokea baada ya kuona watu wengi wakisononeshwa na kukatishwa tamaa na tasnia hii kwa kile kilichotokea kati ya TEF na Mkuu wa mkoa wa Dsm.

Kwanza niweke wazi,mimi siyo mwanachama wala siyo sehemu ya TEF.

Pili,TEF ni jukwaa la hiari linalojumuisha kikundi kidogo sana cha waandishinwa habari,tena asilimia 99,ya wanaounda TEF ni waandishinwa habari wa vyombo vilivyopo Dsm na wanachama wengi ni kutoka kwenye magazeti.

Tatu,TEF ni jukwaa lisilo na nguvu yeyote kisheria,hawana nguvu kwa mwandishi wala chombo chochote,TEF ni jukwaa la hiyari kama vilivyo vikundi vingine vya hiari mfano Saccoss za misiba.

Nne,hakuna sheria inayomtaka kila mwandishi mhariri wa habari kuwa mwanachama wa TEF,asilimia 95 ya wahariri hususani wa vyombo vya Kielekroniki(Radio na TV),siyo wanachama wa TEF,hususani vyombo vilivyopo nje ya Dsm,binafsi nilishawahi kuwauliza watu wa TEF kwa nini wanatutenga sisi waandishi tulio nje ya Dsm?majibu niliyopewa nayajua mwenyewe.

Tano,Chombo kisipo tekeleza maelekezo ama tamko la TEF hakiwezi pelekwa popote kwa sababu TEF haitambuliki kisheria wala kikatiba,ndiyo maana Star TV,TBC,Channel Ten na EFM walipoamua kutangaza habari za mkuu wa mkoa wa Dsm ,TEF wasingeweza kuwashtaki popote zaidi ya kulalamikia mitandaoni na kutoa matamko yasiyo na athari kwa mwandishi na hata chombo chochote.

Kwa hiyo ndugu zangu,kilichofanyika kwenye sakata la mkuu wa mkoa na TEF,siyo maamuzi wala suala la waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini.

Taaluma ya habari ni tofauti na taaluma nyingine,hii ni taaluma ambayo kwa miaka yote imekuwa inaendeshwa shakalabaghala,ndiyo maana hii ndiyo taaluma ambayo hata mtu ambaye hajawahi kumaliza darasa la saba anaruhusiwa kuwa mtangazaji ama mwandishi kabla serikali haijatunga sheria mwaka jana!.

Kabla ya mwaka jana,taaluma ya uandishi wa habari ilikuwa imefungua milango kwa kila mtu,ilikuwa na hata sasa ukifanya ziara kwenye vyombo vya habari huko utakutana na watu ambao wameishia darasa la saba,lakini ni watangazaji,utakutana na watu hawajasoma kabisa uandishi wa habari lakini ni waandishi na watangazaji wa habari!.

Kitu ambacho huwezi kukikuta kwenye taaluma ya sheria,huwezi kuwa mwanasheria kama hujaenda Shule ya sheria,huwezi kuwa mwalimu kama hujasoma ualimu,huwezi kuwa mhasibu kama hujasoma uhasibu kama hujasomea uhasibu na kuthibitishwa na bodi ya wahasibu!.

Hata kuwa refarii ama kocha wa mpira,bila kusomea,lakini kwenye uandishi wa habari kuna maajabu mengi sana,yaani kuna kundi la watu wanafanya uandishi wa habari lkn hawajawahi hudhuria hata kozi fupi ya wiki mbili ya uandishi wa habari!.

Lazima tujue TEF ni kundi tu la watu lisilotambulika na sheria yeyote nchini linalojumuisha kundi dogo la waandishi wa habari.

Ni mwaka jana serikali ilipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari ambayo pamoja na madhaifu yake,sasa imeifanya tasnia hii kuwa taaluma,sasa ili uwe mwandishinwa habari ni lazima uwe na elimu ya kuanzia stashahada(diploma),ya uandishi wa habari!.

Sheria hii sasa inakwenda kuunda chombo maalum kinachokwenda kuwa na nguvu kwa waandishi,hiki kinaundwa kisheria tofauti na TEF ambayo haijaundwa chini ya sheria yeyote!.

TEF inachoweza kufanya ni kukupa msaada wa kukutafutia mwanasheria kama utaingia kwenye tatizo,TEF hawana nguvu yeyote kushughulikia matatizo ya waandishi nchini.

Leo katibu asilimia 75,ya waandishi wa habari nchini wanafanya kazi bila mikataba,kundi kubwa la waandishi ni waathirika wa mfumo mbovu unaosimamia tasnia ya habari,waandishi wengi hawana mishahara,pesa wanayopata ni semina na makongamano ama wanapolipwa na wanaowafanyia story,TEF hawawezi hata siku moja kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa na mishahara na mikataba!.

Kwenye tasnia hii waandishi wa habari asilimia kubwa wanafanya kazi za kujitolea,hawana mikataba, baadhi ya waandishi nchi hii wanafikisha mpaka miezi tisa hawajalipwa mishahara,lakini majina yao kila siku yapo kurasa za mbele za magazeti,wanasikika redioni,wanaoonekana Luningani ila wana mawazo ya maisha magumu.

Waandishi wengi kwenye tasnia yetu,wamenyanyaswa na baadhi waajiri,wanafukuzwa kama baba ama baba mwenye nyumba anavyomfukuza dada wa kazi ama kaka wa shambani,TEF hawawezi fanya lolote kwa sababu TEF ni jukwaa la hiari linalojumuisha wahariri wachache.

Nchi hii ina vituo vya redio 142,humo kuna wahariri,lakini naamini asilimia 99.9,siyo wanachama wa TEF,ina vituo vya TV karibu 32,sidhani kama wahariri wote wamo TEF.

Naandika haya ili kuweka rekodi sawa,sakata la TEF na Mkuu wa mkoa wa Dsm haliihusu tasnia ya habari na waandishi wote wa habari.

TEF ni tofauti kabisa na TLS inayotambulika kisheria na kikatiba,TEF ni tofauti na CWT,ni tofauti na NBAA,TEF haifanani na jukwaa ama jumuiya yeyote kutoka taaluma zingine!.

Kifupi baada ya miaka michache naaamini tasnia hii itakuwa kaa sawa,ubabaishaji ndani ya tasnia,umwinyi na unyanyasaji wanaofanyiwa baadhi ya waandishi na waajiri wao itafikia ukomo!.
 
MKUU KWANI NI NANI ALIYESEMA TEF NI CHOMBO CHA KISHERIA? AU TEF WAMEMLAZIMISHA MTU KUANDIKA/KUTOANDIKA HABARI?

NDIYO MANA HATA MWENYEKITI WA TEF ALIVYOSEMA KUWA RC HABARI ZAKE ZIANDIKWE, WAANDISH HAWAJARIDHIKA NA HAWAKUANDIKA.

UNASEMA HAWATETEI MASLAHI YA WAFANYAKAZI KAMA MISHAHARA NA MIKATABA, KWANI TEF NI CHAMA CHA WAFANYAKAZI?

LILE NI JUKWAA LILILOUNDWA KWA HIYARI KWA LENGO LA KUBADILISHANA MAWAZO, UZOEFU KATIKA TASNIA YA HABARI

UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA MSMAMO WA KUTOANDIKA HABARI ZA RC NI WA WANAHABARI WENYEWE NA NDYO MANA VIONGOZ WA TEF WAMESHINDWA KUREVOKE

Halafu syo kila chombo kinaundwa kwa sheria ya nchi.. VINGNEVYO TUNGEKUWA NA MRUNDIKANO WA SHERIA.
 
Ni sawa si chombo cha kisheria lakini habari Bashite hatujasikia kwenye vyombo vingi vya habari tokea watoe tamko la kutokuandika habari zake
 
Hypocrite!.... angesema haya wakati ule tU tukio limetokea, na hatua ambazo TEF ilichukua ningemuelewa. Lakini kuongea saivi wakati tumeona mkuu wa nchi ameamua kuingilia (kutatua???) tatizo na TEF kuwa submissive to RC ni upumbavu.

Kingine hajatoa maelezo kuwa kilichofanyika pale Clouds ni sawa au la sababu huwezi mhukumu mwenzio bila kusema alichofanya ni sahihi au la
 
Back
Top Bottom