Habari zenu wadau
Juzi tulikuwa tunazungumza na mpenzi wangu katika maongezi kuna story nikawa namsimulia then nilipomaliza akaniambia "hivi we utajisikiaje endapo mtu unaempenda anakudanganya"?nilichomuuliza ni kuwa unadhani nilichokuwa nakwambia nakudanganya? Akabisha basi nikamwambia mama mi sio stupid hivyo nisielewe unachomaanisha.
Basi ilo neno stupid mwanamke kang'aka akaniambia kama unaona mi nakuona wewe mjinga basi samahani naomba tuachane
Akakata simu then akazima
Toka juzi mpaka leo hapokei simu yangu wala hajibu sms zangu.
Jamani hivi hili nalo ni kosa la watu kuachana kweli?
Huyo anakuepusha shari huko siku za usoni, na wewe zima simu halafu uanze mbele.Habari zenu wadau
Juzi tulikuwa tunazungumza na mpenzi wangu katika maongezi kuna story nikawa namsimulia then nilipomaliza akaniambia "hivi we utajisikiaje endapo mtu unaempenda anakudanganya"?nilichomuuliza ni kuwa unadhani nilichokuwa nakwambia nakudanganya? Akabisha basi nikamwambia mama mi sio stupid hivyo nisielewe unachomaanisha.
Basi ilo neno stupid mwanamke kang'aka akaniambia kama unaona mi nakuona wewe mjinga basi samahani naomba tuachane
Akakata simu then akazima
Toka juzi mpaka leo hapokei simu yangu wala hajibu sms zangu.
Jamani hivi hili nalo ni kosa la watu kuachana kweli?
Wakati mwingine watu wanaachana kwa mambo ya kipumbavu mno!!! Nimeshaona ndoa inavunjika kisa sufuria ya ugali. Sufuria ya ugali ikazaa ugomvi mkubwa mpaka amani kupotea ndani ya nyumba na mwisho ndoa kuvunjika. Kama unampenda kiasi hicho mfuate kwake/kwao au kazini/chuoni mkae chini ili muongee kwa kituo kama atakuwa tayari kukupa nafasi hiyo, vinginevyo kuna njemba nyingine imeshakuwekea kauzibe...WE URIE TU!
upo sahihi katika mzozo wowote ule lazima kuwe na short term causes na long term causes so ktk mazingira hayo lazima kutakuwa kuna vijisababu vingine vimejificha