Don't be Cheap

jay311

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
2,932
2,715
Amekuomba urafiki W-T-F
Mkachati
Umeangalia picha zake
Anaendesha GARI
Anaonekana ni jamaa mwenye uwezo
Umemkubalia urafiki
Amekutumia text inbox
Umemjibu
Amekuomba out
Mkapanga kuonana
Ukajikwatua mwenyewe
Ukajipulizia na marashi ya kunukia vyema
Ukaweka na make-up na weave mpya.
Akakuchukua kwa ajili ya lunch Serena hotel
Akakuagizia na soft drinks
Mkawa na muda mzuri pamoja
Akakushika mkono
Akakufanya uwe unacheka muda wote kwa vituko vyake
Ukampenda
Ikawa kama umemjua kwa miaka
Akakuchukua kwenda kwake
Akaweka mazingira ya wewe kujisikia upo kwako kwa kukuruhusu ulale kitandani kwake
Akakubusu kimahaba
Ukapenda jinsi alivyo romantic, nguvu na ujasiri
Ukajisikia secure ukiwa nae
Ukajua kuwa unachoenda kufanya sio sahihi lakini ukajisikia poa tu
Ukamwambia atumie kinga, akakuambia it's too late.
Ukamkubalia na hukutaka kumsumbua.
Akakuambia anakupenda na hukusita kumwambia unampenda pia.
Baada ya kumaliza akafungua friji na kukunywesha maji ya kunywa. Ukajihisi hapa mume nimepata
Ukajihisi ni mwanamke special
Atakuwa ndio yeye uliyekuwa ukimuota siku zote.
Ukavaa nguo.
Akakuchukua mpaka sehemu zinakopaki taxi
Akakubusu katika shavu.
Nimekuwa na muda mzuri na wewe akakueleza.
Akakupa Tsh 100,000. Ukatabasamu na kumwambia nitakuona kesho.
Akabaki kimya. Taxi uliyopanda ikaondoka.
Ndani ya taxi hukuacha kutabasamu
Ukafika nyumbani kwenu na kumwandikia text watsapp kwamba umefika salama.
Yupo online lakini hakujibu text yako
Ukaamua kumtext tena, hakujibu!
Dakika chache baadae humuoni watsapp unaona kivuli tu. AMEKUBLOCK!!
Siku, wiki, miezi ikapita ukaanza kujisikia homa homa, mchovu, uzito umepungua na utando mdomoni
Ukaenda kituo cha afya
Ukapima
Nusu saa baadae daktari anaingia.
Pole sana dada yangu daktari anakuambia.
Una maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ni mjamzito vile vile.
Mimba, HIV+????
HOW??
Hauelewi
Inakuumiza sana, hauamini.
Unaenda nyumbani.
Ukiwa na hofu kubwa.
Unaona kifo hichi hapa
Unatazama angani, na unauona mwisho wako huu hapa. Unajuta kumuamini mtu kirahisi hivyo.
DON'T BE CHEAP!!!
 
Sasa awe cheap tena kashaukwa ungemuandikia thread ya kutosahau kunywa dawa na kufatilia dozi
 
Jay 311, Usifanye wenye maambukizi ya ukimwi wajihisi kufa kufa.. Si kweli kwamba ukishapata maambukizi unaona kifo hiki hapa.. Hiyo part ya post yako imekaa kiunyanyapaa...

Unaweza kuwa HIV+ na ukaishi ndoto zako, ukazaa mtoto asiye na maambukizi na maisha yakaendelea.

Being HIV+ NEVER MEANS YOUR DREAMS ARE NO LONGER VALID.
 
Ni kweli lakini namaanisha kwa mtu ambaye ndo kajua tu kuwa sasa nimeukwaa.. Yaani hana tena amani japo anaweza kupata amani sijui unanielewa?
 
Ni kweli lakini namaanisha kwa mtu ambaye ndo kajua tu kuwa sasa nimeukwaa.. Yaani hana tena amani japo anaweza kupata amani sijui unanielewa?
Point yako naipata, tatizo ni kwamba interpretation ya watu inaweza kuwa in a negative way.. Maana huwezi jua nani atapitia uzi wako akiwa katika hali gani.. So ungeweza kubuni namna nzuri ya kuonesha kwamba hiyo ni feeling mtu anapata anapogundua ameukwaa ili kuminimize possible risks za mtu anayesoma uzi wako akiamini ndo kinachotokea pindi ugunduapo umeambukizwa...
Plus umeruka part ya counseling wanayopewa na madokta ambayo inasaidia kuepuka hiyo hali ya kutokubaliana na hali halisi.. Badala yake umesema tu ati dk. Anamwambia "pole dada, umeambukizwa HIV"
 
Nashkuru... Samahani kama nitakuwa nimewakwaza wengine
 
Dakika chache baadae humuoni watsapp unaona kivuli tu. AMEKUBLOCK!!
Siku, wiki, miezi ikapita ukaanza kujisikia homa homa, mchovu, uzito umepungua na utando mdomoni
Ukaenda kituo cha afya
Ukapima
Nusu saa baadae daktari anaingia.
Pole sana dada yangu daktari anakuambia.
Una maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ni mjamzito vile vile.
Mimba, HIV+????
HOW??
Hauelewi
Inakuumiza sana, hauamini.
Unaenda nyumbani.
Ukiwa na hofu kubwa.
Unaona kifo hichi hapa
Unatazama angani, na unauona mwisho wako huu hapa. Unajuta kumuamini mtu kirahisi hivyo.
DON'T BE CHEAP!!!
hapa ndipo patamu huko kwingine STAREHE TUU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom