Ni mrembo wala hilo haliwezifichika,
Nilitupia swaga zikakubalika,
nikaitwa baby moyo ukasuuzika,
Safari ikawadia JF Nikaaga naenda kusaka,
mtoto wiki hapatikani hewani,
moyo ukaanza tapatapa,
ahadi nikatoa kilonga longa kumtumia,
mapenzi yakapamba moto,
nikaitwa baby kila dakika,
kilonga longa nikatuma,
penzi likaanza dorora,
mjini nikarudi, mtoto hewani happatikani,
akipatikana hapokei,
nikakaza moyo sms ya kibuti nikatuma,
kimyaa hakuna majibu nikakausha,
jana mtoto kanitafuta baada ya wiki 3 kukausha,
eti simu alipoteza na namba alisahau,
nikapiga moyo konde nikakausha,
nikitaka tuonane anakuwa mgonjwa
leo kanipigia
''baby ile ishu utanikamilishia lini?''
kengele zikapiga kwa kichwa... Nimekuwa
ATM?
Aje kuchukua kisha asepe tena?
manoah charminglady Nivea Arushaone ladyfurahia mimisa Paloma chit-chat