Dondoo muhimu kwa wazazi na wazazi watarajiwa

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
1. Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu

2. Mkanye mtoto wako wa kike kuhusu kukubali kupakatwa hovyo, bila kujali ni nani anampakata, hata kama ni mjomba wake.

3. Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.

4. Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
c65ea12f399560fb5252679613391686.jpg


5. Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.

6. Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.

7. Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.

8. Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya fuatilia ujue sababu ni ipi.

SHARE NA MARAFIKI ZAKO pia ongeza nyingine unayoijua.
 
Umesema kweli....mkunje angali mbichi. Akikauka atavunjika

Lakini hii haimaanishi umnyime mtoto uhuru wake akiwa na wenzake. Mfundishe kujisimamia.......siunajua tena balance is key in life
 
Mkuu unataka kutuaminisha kuwa hupati mda wa kuwa na mwanao/wanao kisa kazi?
Ni wazo zuri, ila ki uhalisia halitekelezeki.. imagine mimi tangu nikiwa mdogo baba anatoka asubuhi anarudi usiku everyday na mama nae alikuwa busy nae.. so hapo ingewezekana vip
 
Ni wazo zuri, ila ki uhalisia halitekelezeki.. imagine mimi tangu nikiwa mdogo baba anatoka asubuhi anarudi usiku everyday na mama nae alikuwa busy nae.. so hapo ingewezekana vip
Hapo ndipo penye tatizo sasa, ndio maana hata wewe huoni tatizo maana we mwenyewe ni tatizo.
 
Back
Top Bottom