Donald Trump apata kura nyingi Republican

Donald Trump apata kura nyingi Republican

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
Bila ya kutarajiwa akiwa ameingia katika nafasi ya juu kwenye uwanja wa siasa za Marekani, bilionea Donald Trump amepata rasmi uteuzi wa chama cha Republican kuwania urais kwa mujibu wa hesabu ya wajumbe iliyofanywana shirika la habari la Associated Press-AP.

Akiwa amebakiwa na wagombea wachache kati ya 17wa chama Republican waliokuwa wakiwania pamoja naye na hivyo kujiondoa mapema mwezi huu katika kinyang’anyiro AP imesema Trump ambaye aliwahi kuendesha kipindi cha televisheni hivi sasa anahakikishiwa kuwa ana wingi wa wajumbe 1,237 wanaohitaji katika mkutano mkuu wa Republican utakaofanyika mwezi Julai ambapo atateuliwa rasmi kuwania urais.

Anatarajiwa huenda akapata mamia ya wajumbe katika uchaguzi wa awali ambao utafanyika June 7. Nina heshima kubwa Trump aliwaambia waandishi wa habari katika jimbo la kaskazini la North Dakota na kuapa kwamba siku za kwanza za urais wake atatengua amri nyingi za kiutendaji ambazo zilitiwa saini na Rais Barack Obama na kulijenga tena jeshi la nchi.

Chanzo: VOA
 
Bora Triump aje awaadibishe hawa watawala wa Africa wenye akili za kuambiwa..!
 
Kuna ushindani mkubwa sana kumshinda mama
 
tusubiri taarifa kamili ya uteuzi huo, trump ana misimamo na itikadi zake ambazo ni ngumu kuzielewa
 
Apite tuu safari za maraisi wa Afrika kwenda na bakuri zitapungua watajikita sana katika kutatua matatizo ya Wananchi..
 
Trump ni mtata kwanza amewagalagaza wapinzani wake wamebaki wana hahaa.
 
Marais Wastaafu akiwemo Bush wamemkana Donald Trump Kwa sababu sizizoeleweka ili kuiaminisha dunia kwamba Trump kumbe wana agenda zao za siri.
 
Hapo tunashagazwa sisi lakini wanafahamiana wao jambo moja kuitawala dunia hivi karibuni Ufunuo 13 :11-18 unaenda kutimia sasa.
 
Marais Wastaafu akiwemo Bush wamemkana Donald Trump Kwa sababu sizizoeleweka ili kuiaminisha dunia kwamba Trump kumbe wana agenda zao za siri.
Hayo yote ni maigizo tu, Trump ni Project iliyoandaliwa na Marekani wenyewe wakiwemo hao akina Bush kwa sababu zao ambazo ni lazima zitimie sasa before 'it's too late'.
Kama wasingemhitaji wala asingefika hapo. Huoni namna wanavyomjengea mazingira 'magumu' halafu wapinzani wake hao wanavyojisalimisha kiajabu ajabu!!
Kama wasingemhitaji Trump, basi Sanders kule Democrat angekuwa ameshajitoa lakini badala yake Sanders ni kama anajengwa katika dakika hizi za mwisho ili kumvuruga na kumyumbisha kabisa Hillary Clinton, huku Trump akizidi kuimarika.
Asiyehitajika hapo ni Hillary Clinton wala si Trump. Endeleeni tu kuanini kuwa Saddam anatengeneza na ameficha silaha za chemical na nyuklia.
 
Hayo yote ni maigizo tu, Trump ni Project iliyoandaliwa na Marekani wenyewe wakiwemo hao akina Bush kwa sababu zao ambazo ni lazima zitimie sasa before 'it's too late'.
Kama wasingemhitaji wala asingefika hapo. Huoni namna wanavyomjengea mazingira 'magumu' halafu wapinzani wake hao wanavyojisakimisha kiajabu ajabu!!
Kama wasingemhitaji Trump, basi Sanders kule Democrat angekuwa ameshajitoa lakini badala yake Sanders ni kama anajengwa katika dakika hizi za mwisho ili kumvuruga na kumyumbisha kabisa Hillary Clinton, huku Trumonakizidi kuimarika.
Asiyehitajika haoo ni Hillary Clinton wala si Trump. Endeleeni tu kuanini kuwa Saddam anatengeneza na ameficha silaha za chemical na nyuklia.
Umeanza vizuri ila hapo chini umevuluga.
 
Back
Top Bottom