Donald Trump amsifu Saddam Hussein

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
160619050840_donald_trump_640x360_getty_nocredit.jpg

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.

Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.

“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.” Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.

130829120722_estatua_sadam_bandera_624x351_getty.jpg

Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”

Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.

Chanzo: BBC
 
Huyu jamaa amekuwa na Matamshi tata sana

Lengo lake sijui nini hasa
 
Hapo nadhani amekosea,na kitamnyima urais,kaisha alert organs nyingi kuwa hafai kuwa rais,kuuwawa sadam ilikuwa far more than we know or he knows.
 
160619050840_donald_trump_640x360_getty_nocredit.jpg

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.

Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.

“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.” Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.

130829120722_estatua_sadam_bandera_624x351_getty.jpg

Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”

Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.

Chanzo: BBC
Ngongo
 
UK Iraq war inquiry admitted today that it was wrong decision to support war on Iraq as well as they regret consiquences aftermath
Hiyo inquiry ilikuwa ni kwa upande wa uk kupeleka vikosi vyake kule,tony blair alikuwa anabuluzwa tu gwalker,hakukuwa na 7bu wao kupeleka vikosi
 
UK Iraq war inquiry admitted today that it was wrong decision to support war on Iraq as well as they regret consiquences aftermath
Kwani mi nimekataa hayo makosa yaliyofanyika kuivamia Iraq.
Mi ninachosema hivii .
Trump utadhani huwa Ana homa ya vipindi, sometime yes sometime no.
 
Sasa comment yake hii ni yes or no !?
 
Kwa hali ya dunia ilivyo leo, hakika Trump anastahili kua Rais wa USA.
 
Baada ya Saddam Hussein kuondolewa Iraq hivi sasa kuna Panya wamesimamisha masikio Iran and Saudia Arabia lakini mwanaume yule alipokuwa hai mashariki ya kati ilikuwa inaeleweka vizurii sio sasa
 
Kumpindua saddamu na gadaf lilikuwa kosa sana,kama itakavyokua kosa kumpindua Assad .
Trump yuko sawa
 
X
160619050840_donald_trump_640x360_getty_nocredit.jpg

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.

Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.

“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.” Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.

130829120722_estatua_sadam_bandera_624x351_getty.jpg

Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”

Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.

Chanzo: BBC
Trump huwa simpendi lakini wakati mwingine anasema ukweli kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom