Hawa ni maaskofu wawili wa Anglikana, mmoja mstaafu na pia amewahi kuwa kiongozi wa Anglikana Tanzania. Huyu ni Askofu Donald Mtetemela na sasa ni mjumbe wa bunge maalumu la katiba. Askofu Valentino Mokiwa yeye ni askofu wa Anglikana jimbo la Dar. Sasa tofauti yao ni kubwa.
Mtetemela ambaye amewahi kushika nafasi kubwa kanisani, ameonyesha udhaifu hasa alipochangia bungeni kuhusu kauli ya Lipumba. Alionekana wazi kama ni mtu mwenye mapenzi na CCM, japo yeye anasema yupo neutral, si kweli.
CCM wamempuuza Warioba, Mtetemela hakuongea. Kuna matusi yalikuwa yanaporomoshwa bungeni, hakukemea. Mwenzake, Askofu Mokiwa, akiwa anazungumza kwenye ibada ya Pasaka, hakuwa mnafiki. Aliponda waziwazi wote walioikejeli na kuidharau tume ya katiba. Huyu ndiye kiongozi mathubuti nasubutu kusema.